Suwrah Gani Kusoma Katika Swalaah Ya Tahajjud Na Witr?
Suwrah Gani Kusoma Katika Swalaah Ya Tahajjud Na Witr?
SWALI:
Salaam Aleiqum,
Ningependelea kujua ni sura gani hasa zilizosuniwa katika sala ya witri? Ukiwacha Sabih.
Ahsante
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kuhusu Swalaah ya Witr, ilikuwa ni Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali Raka'ah mbili mbili usiku na kumalizia kwa Raka'ah tatu za Witr na kufikia jumla ya Raka'ah zote kuwa kumi na moja kama ilivyokuja katika Hadiyth ifuatayo:
عن عائشة رضي الله عنها قال: "ما كان يزيد في رمضان ولا غيره على إحدى عشرة ركعة، يصلي أربعًا، فلا تسأل عن حسنهن وطولهن، ثم يصلي أربعًا، فلا تسأل عن حسنهن وطولهن، ثم يصلي ثلاثًا" البخاري و مسلم
Imepokelewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa) “Hajapata kuzidisha katika Ramadhwaan wala miezi mingine zaidi ya Raka'ah kumi na moja, akiswali nne, wala usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha akiswali nne wala usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha akiswali tatu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na kuhusu Suwrah alizokuwa akisoma katika Swalatul-Witr zimethibiti katika Hadiyth hii ifuatayo:
Hadiyth kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa) alikuwa akisoma katika Raka'ah ya mwanzo ya (Swalaah) Witr
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
na Raka'ah ya pili
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
na Raka'ah ya tatu
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ
na
Mu ‘awwidhataan
Yaani;
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ
Na,
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ
[At-Tirmidhiy]
Na Allaah Anajua zaidi