Kamba Wa Kuchomwa Katika Mkaa BBQ
Kamba Wa Kuchomwa Katika Mkaa BBQ
Mahitajio |
Utayarishaji |
Kipimo
|
Kamba wakubwa |
osha chuja maji |
2 kilo |
Pilipili boga/Capsicum |
katakata vipande kiasi |
5- 10 |
Nyanya/tungule ndogo ndogo |
osha tu weka kando |
15-20 |
Ukwaju wa brauni |
roweka, kamua |
2 vikombe vya chai |
chumvi |
|
kiasi |
pilipili nyekundu ya unga |
|
1 kijiko cha supu |
pilipili mbichi ya kijani/ya shamba |
saga |
7 |
Bizari ya pilau/cummin |
ilosagwa |
2 vijiko vya chai |
Vijiti vya BBQ |
|
kiasi |
Namna Ya Kupika:
- Weka kamba katika bakuli.
- Changanya ukwaju, chumvi, pilipili zote, bizari katika kibakuli.
- Tia sosi ya ukwajui katika kamba changanya vizuri, acha kando kuwaroweka wakolee vizuri. Weka kiasi muda wa masaa mawili au zaidi.
- Chomeka kamba katika vijiti kwa kuweka baina yake tungule/nyanya na kipande cha pilipili boga
- Choma katika mkaa huku unarashia sosi ilobakia katika bakuli.