Saladi Ya Komamanga Pilipili Boga Tango
Saladi Ya Komamanga Pilipili Boga Tango
Vipimo na Namna ya Kutayarisha
Majani ya saladi (lettuce) osha chuja maji - 1 msongo (bunch)
Komamanga chambua - 2
Pilipili boga (Capsicum) la kijani osha katakata vipande kwa urefu kama picha – 1
Pilipili boga la rangi ya manjano – 1
Pilipili boga la rangi ya orengi – 1
Matango osha, katakata vipande virefu refu - 2
Namna Ya Kutayarisha:
- Katika bakuli jengne changanya vitu vyote isipokuwa majani ya saladi. Bakisha kidogo chembe za komamanga.
- Chukua bakuli jengine la kuweka mezani, panga majani ya saladi pembezoni.
- Weka mchanganyiko wa pilipili boga, tango na komamanga katikati ya bakuli.
- Mwagia komamanga zilobakia upambe vizuri ikiwa tayari kuliwa
