024-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Uongo Unaruhusiwa Katika Kupatanisha Waliogombana Na Vitani
Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 24:
Uongo Unaruhusiwa Katika Kupatanisha Waliogombana Na Vitani
عَنْ أُمَّ كُلْثُومٍ بِنْتَ عُقْبَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم) يَقُولُ: ((لَيْسَ الْكَذَّابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خَيْرًا)) متفق عليه.
وفي رواية مسلم زيادة قَالَتْ: وَلَمْ أَسْمَعْهُ يُرَخِّصُ فِي شَيْءٍ مِمَّا يَقُولُ النَّاسُ إلاَّ فِي ثَلاَثٍ: تَعْنِي الْحَرْبَ، والإصْلاَحَ بَيْنَ النَّاس، وَحَدِيثَ الرَّجُلِ امْرَأَتَهُ وَحَدِيث الْمَرْأَةِ زَوْجَهَا
Imepokelewa kutoka kwa Ummu Kulthuum bint ‘Uqbah (رضي الله عنها) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hajasema uongo yule mwenye kusuluhisha baina ya watu akawa anasambaza [habari ya] kheri, au anasema kheri)). [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika riwaayah ya Muslim kuna ziada inayosema: Akasema “Wala sikumsikia akiruhusu chochote katika uongo wanaosema watu isipokuwa katika mambo matatu.” Yaani katika vita, kusuluhisha baina ya watu, mwanamume kuzungumza na mkewe na mke kuzungumza na mumewe.”
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Uislamu umeharamisha kusema uongo isipokuwa katika hali tatu zilizotajwa.
Rejea Hadiyth namba (86).
2. Umuhimu wa kuweko amani baina ya jamii ya Kiislamu kiasi kwamba kusema uongo ambao ni dhambi kubwa umehalalishwa kwayo.
Rejea Hadiyth namba (94).
3. Fadhila za kusuluhisha waliokhasimikiana ni kubwa mno. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾
Hakuna khayr katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha swadaqah, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka radhi za Allaah, basi Tutampa ujira adhimu. [An-Nisaa (4: 114)]
4. Umuhimu wa mapatano na amani baina ya mke na mume na jamii kwa ujumla Rejea: An-Nisaa (4: 128), Al-Anfaal (8: 1) Al-Hujuraat (49: 10).
Rejea pia Hadiyth namba (29),
5. Uislamu ni Dini ya amani, na kuamkiana kwa maamkizi ya Kiislamu ni sababu mojawapo ya kuleta amani na kumwingiza Muislamu Peponi. Rejea Hadiyth namba (42), (72).
.