092-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Makatazo ya Kuapa Pasi Na Allaah, Kujiua, Kutekeleza Nadhiri Kwa kitu Asichokimiliki, Kumlaani Muumin
Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 92
Makatazo ya Kuapa Pasi Na Allaah, Kujiua,
Kutekeleza Nadhiri Kwa kitu Asichokimiliki, Kumlaani Muumin
عن أَبِي زَيْد بْنِ ثَابِت بن الضَّحاك الأنْصاريِّ (رضي الله عنه) وَهُوَ مِنْ أَهْل بَيْعَةِ الرِّضْوَانِ، قَال: قَال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ بِمِلَّةٍ غَيْرِ الإِسْلاَمِ كَاذِبًا مُتَعَمِّداً فَهُوَ كَمَا قَالَ، وَمَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِشَيْءٍ عُذِّبَ بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَيْسَ عَلَى رَجُلٍ نَذْرٌ فِي شَيْءٍ لاَ يَمْلِكُهُ، وَلَعْنُ الْمُؤْمِنِ كَقَتْلِهِ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abu Zayd bin Thaabit bin Adh-Dhwahaak Al-Answaariy (رضي الله عنه) naye ni katika walioshuhudia Bay’atur Ridhwaan amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم ) amesema: ((Atakayeapa yamini kwa mila isiyokuwa ya Uislamu kwa uongo na makusudi, basi atakuwa ni kama alivyoapa. Na anayejiua kwa kitu, ataadhibiwa nacho Siku ya Qiyaamah. Wala haimpasi mtu kutekeleza nadhiri ya kitu asichokimiliki. Na kumlaani [kumwapiza] Muumin ni sawa na kumuua)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Tahadhirisho la kuapa pasi na Allaah (سبحانه وتعالى), kwani ni shirki na kufru kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَال: ((مَنْ حَلَفَ بِغَيْرِ اللَّهِ فَقَدْ كَفَرَ أَوْ أَشْرَك)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ وَصَحَّحَهُ الْحَاكِمُ
Na Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeapa kwa asiye Allaah, amekufuru au amefanya shirki)) [At-Tirmidhiy na ameikiri ni Hasan, na Al-Haakim ameikiri ni Swahiyh, na Abu Daawuwd, na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy]
Rejea pia Hadiyth namba (5).
2. Haramisho la kujiua na tahadharisho la adhabu yake kwamba afanyae hivyo, atakariri kujiua Siku ya Qiyaamah kwa njia ile ile aliyojiulia duniani:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ تَرَدَّى مِنْ جَبَلٍ فَقَتَلَ نَفْسَهُ، فَهْوَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ، يَتَرَدَّى فِيهِ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ تَحَسَّى سَمًّا فَقَتَلَ نَفْسَهُ، فَسَمُّهُ فِي يَدِهِ، يَتَحَسَّاهُ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِحَدِيدَةٍ، فَحَدِيدَتُهُ فِي يَدِهِ، يَجَأُ بِهَا فِي بَطْنِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا)) البخاري ومسلم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Yeyote atakayejitupa kutoka mlimani na kujiua, atatupwa ndani ya moto milele. Atakayekunywa sumu na kujiua, basi atatupwa motoni na huko atakuwa akiinywa hiyo sumu milele. Atakayejiua kwa kipande cha chuma, atatiwa motoni akiwa na kipande hicho cha chuma akijitwanga nacho tumboni kwake humo motoni milele))]. [Al-Bukhaariy na Muslim]
3. Kutekeleza nadhiri ya kitu asichomiliki mtu ni dhulma na kukhini haki ya mwenyewe.
4. Haramisho la kumlaani (kumwapiza) Muumin kitendo ambacho kimefananishwa na mauaji. Haya ni katika madhambi makubwa. Hii inadhihirisha kuwa Uislamu unampendelea mtu usalama na amani daima.
5. Kulaani kitu, au wakati au mnyama au mtu kwa ujumla kumekatazwa katika Hadiyth kadhaa, na kwamba laana humrudia mtu mwenyewe ikiwa haistahiki kulaani kitu. Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ (صَلَى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: يُؤْذِينِي ابْنُ آدَمَ يَسُبُّ الدَّهْرَ، وَأَنَا الدَّهْرُ أُقَلِّبُ الْلَّيْلَ وَالنَّهَارَ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah Ta’aalaa Amesema: Bin Aadam ananiudhi, kwani anatukana dahari [wakati au zama], na hali Mimi ni Ad-Dahr [Namiliki kila kitu na uwezo], Nageuza usiku na mchana)). [Al-Bukhaariy]
6. Allaah (سبحانه وتعالى) Amelaani watu kadhaa katika Qur-aan; wanaokata undugu, madhalimu na wengineo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ۚ أُولَـٰئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ الْأَشْهَادُ هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ﴿١٨﴾
Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia uongo Allaah. Hao watahudhurishwa mbele ya Rabb wao, na mashahidi watasema: “Hawa ndio wale waliomzulia uongo Rabb wao!” Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu. [Huwd (11: 18)]
Rejea pia: Al-Baqarah (2: 88, 159, 161), Aal-‘Imraan (3: 87), Al-Ahzaab (33: 57), Muhammad (47: 23), An-Nisaa (4: 52).
7. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amelaani watu kadhaa katika Ahaadiyth, mfano ((Anayekula ribaa, anayeilipia na anayeiandika na anayeishuhudia)). [Muslim]