000-Maswali 200 Na Majibu Ya 'Aqiydah: Utangulizi Wa Mtunzi

 

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

000-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah Utangulizi Wa Mtunzi

 

 

بِسْمِ الله الرَّحْمنِ الرَّحيم

 

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١﴾

AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia viza na nuru; kisha wale ambao wamekufuru wanawasawazisha wengine na Rabb wao.

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ ﴿٢﴾

Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udongo kisha Akahukumu muda maalumu, na uko Kwake muda maalumu uliokadiriwa, kisha nyinyi mnatilia shaka.

 

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾

Na Yeye ni Allaah mbinguni na ardhini; Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu; na Anajua yale mnayoyachuma [Al-An’aam: 1-3]

 

 

Na nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Peke Yake Hana mshirika na Ambaye ni:

 أَحَدٌالصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

Mmoja Pekee. (Allaah) ni Aliyekamilika sifa za utukufu Wake Mkusudiwa haja zote. Hakuzaa na wala Hakuzaliwa. Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye. [Al-Ikhlaasw]

 

 بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ

Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Anapokidhia jambo basi huliambia Kun! Basi nalo huwa. [Al-Baqarah: 116-117]

 

 وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾

Na Rabb wako Anaumba na Anachagua Atakavyo. Haikuwa wao wana khiari yoyote. Subhaana-Allaah Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale yote wanayomshirikisha. [Al-Qaswasw: 68]

 

لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ

Haulizwi (Allaah) kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa. [Al-Anbiyaa: 23]

 

وأشهد أن سيدنا ونبينا محمدا عبده ورسوله أرسله بالهدى ودين الحق ليظهره على الدين كله ولو كره المشركون، صلى الله عليه وسلم وعلى آله وصحبه الذين قضوا بالحق وبه كانوا يعدلون، وعلى التابعين لهم بإحسان الذين لا ينحرفون عن السنة ولا يعدلون بل إياها يقتفون وبها يتمسكون وعليها يوالون ويعادون وعندها يقفون، وعنها يذبون ويناضلون وعلى جميع من سلك سبيلهم وقفا أثرهم إلى يوم يبعثون.

 

Na nashuhudia ya kwamba Sayyidinaa na Nabiy wetu, Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mja na Rasuli Wake. Amemtuma kwa Risala na Mwongozo na Dini ya haki ili Aidhihirishe juu ya dini zote japo watachukia washirikina.

 

Rahmah na amani za Allaah ziwe juu yake, pamoja na Ahli zake na Swahaba zake ambao walihukumu kwa haki  na kwa Dini hiyo walikuwa waadilifu. Na At-Taabi’iyna (waliowafuata) kwa ihsaan mpaka Siku ya Mwisho, ambao walikuwa hawaendi kinyume na Sunnah, bali kwa Sunnah hizo walizifuata na kuzifanyia kazi, pamoja na kushikamana nazo. Na waliwapenda wanazozifanyia kazi, na kuwachukia kwa wenye kuzipuuza, na kwa Sunnah hizo walizilinda na kuzitetea, na wote waliofuata nyayo zao mpaka Siku ya kufufuliwa.

 

أما بعد فهذا مختصر جليل نافع، عظيم الفائدة جم المنافع، يشتمل على قواعد الدين، ويتضمن أصول التوحيد الذي دعت إليه الرسل وأنزلت به الكتب ولا نجاة لمن بغيره يدين، ويدل ويرشد إلى سلوك المحجة البيضاء ومنهج الحق المستبين شرحت فيه أمور الإيمان وخصاله، وما يزيل جميعه أو ينافي كماله، وذكرت فيه كل مسألة مصحوبة بدليلها, ليتضح أمرها وتتجلى حقيقتها ويبين سبيلها، واقتصرت فيه على مذهب السنة والاتباع وأهملت أقوال أهل الأهواء والابتداع، إذ هي لا تذكر إلا للرد عليها، وإرسال سهام السنة عليها، وقد تصدى لكشف عوارها الأئمة الأجلة، وصنفوا في ردها وأبعادها المصنفات المستقلة مع أن الضد يعرف بضده ويخرج بتعريف ضابطه وحده، فإذا طلعت الشمس لم يفتقر النهار إلى استدلال، وإذ استبان الحق واتضح فما بعده إلا الضلال ورتبته على طريقة السؤال ليستيقظ الطالب وينتبه، ثم أردفه بالجواب الذي يتضح الأمر به ولا يشتبه وسميته. "أعلام السنة المنشورة، لاعتقاد الطائفة الناجية المنصورة" والله أسأل أن يجعله ابتغاء وجهه الأعلى، وأن ينفعنا بما علمنا، ويعلمنا ما ينفعنا نعمة منه وفضلا إنه على كل شيء قدير وبعباده لطيف خبير، وإليه المرجع والمصير وهو مولانا فنعم المولى ونعم النصير.

 

Amma Ba’ad, huu ni Mukhtasari mzuri wenye kunufaisha, na wenye faida kubwa, umesheheni manufaa yenye kukusanya juu ya misingi ya Dini. Pia una misingi ya Tawhiyd iliyolinganiwa na Rusuli wote. Na kwa misingi hiyo vitabu vilishushwa. Na wala hafaulu mtu kinyume na misingi hiyo ambayo ndio yenye kumuongoza katika hoja ya wazi, na Manhaj Swahiyh ya haki. Nimeweka wazi mambo ya Iymaan na yanayohusiana nayo, na nimetaja mas-ala yote sambamba na dalili za nasw ili kuweka wazi zaidi uhakika wa misingi hiyo na kubainisha njia zake. Na nimetosheka kwa hoja na mwenendo wa Ahlus-Sunnah wal-Ittibaa’[1]  Nimeacha kauli za watu wa matamanio na uzushi, pamoja na kuwapinza (radd) na kuwapelekea Sunnah Swahiyh zilizobainishwa na Wanazuoni watukufu kwa ajili ya kujibu hoja zao na kuzitupilia mbali kwa kutunga vitabu mbalimbali. Kwa hakika upinzani kujulikana kwa hoja zake, na kutoa dalili kwa taarifu ya udhibiti wake na mpaka wake. Na jua likitoka huna haja ya kutafuta mchana, na haki inapodhihiri na kufunuka hakuna baada yake isipokuwa ni upotevu.

 

Na nimepanga kwa njia ya maswali ili mwanafunzi aamke na kuzinduka, kisha nimeweka majibu yake ambayo yatakuwa wazi bila kumchanganya mwanafunzi au msomaji na nikakiita:  "Miongozo ya Sunnah Swahiyh kwa ‘Aqiydah ya Atw-Twaaifah An-Naajiyah Al-Manswuwrah.[2]

 

Namuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Ajaalie kazi hii kuwa ya kutaka Radhi Zake, Atunufaishe kwa elimu, na Atufundishe yanayotufaa, na kutunufaisha kwa neema Zake na fadhila Zake, kwani yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Qadiyr (Muweza) wa kila kitu,  ni Latwiyf, Mjuzi wa yaliyofichika na ya Dhahiri  na kwake Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) marejeo. Yeye Ndiye Mola Msaidizi wenu, basi Mola Mzuri Alioje, na Mnusuraji Mzuri Alioje!

 

 

 

 

[1] Watu wa Sunnah na ufuataji wa aliyokuja nayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

[2] Kundi lilookoka na kunusuriwa.

 

 

Share