001-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Jambo Gani La Mwanzo Linalopasa Waja
200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
001-Jambo Gani La Mwanzo Linalopasa Waja
Swali:
ما أول ما يجب على العباد؟
Jambo gani la mwanzo linalopasa waja?
Jibu:
ج: أول ما يجب على العباد معرفة الأمر الذي خلقهم الله له ، وأخذ عليهم الميثاق به وأرسل به رسله إليهم وأنزل به كتبه عليهم ، ولأجله خلقت الدنيا والآخرة والجنة والنار وبه حقت الحاقة ووقعت والواقعة وفي شأنه تنصب الموازين وتتطاير الصحف وفيه تكون الشقاوة والسعادة وعلى حسبه تقسم الأنوار (ومن لم يجعل الله له نورا فما له من نور).
Jambo la mwanzo linalopasa kwa waja ni: Kujua kusudio la Allaah (سبحانه وتعالى) la kuwaumba wao. Kuchukua ahadi nzito kutoka kwao, kuwatumia Rusuli, kuwashushia kwayo vitabu Vyake. Na kwa ajili yake dunia na Aakhirah imeumbwa, na Jannah na Moto, na imehakiki la kuhakiki na litatokea la kutokea na jambo hilo Mizani zitawekwa, na Swahifa zitatawanywa, na kutakuwa na huzuni na furaha, na kwa mnasaba huo kutagawanywa Nuru.
وَمَن لَّمْ يَجْعَلِ اللَّـهُ لَهُ نُورًا فَمَا لَهُ مِن نُّورٍ
Na ambaye Allaah Hakumjaalia Nuru, basi hawi na Nuru [An-Nuwr 24:40]