003-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya ‘Abdu (Mja)?
200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
003-Nini Maana Ya ‘Abd (Mja)?
Swali:
ما معنى العبد؟
Nini maana ya ‘Abd (Mja)?
Jibu:
ج: العبد إن أريد به المعبد أي المذلل المسخر فهو بهذا المعنى شامل لجميع المخلوقات من العوالم العلوية والسفلية من عاقل وغيره ورطب ويابس ومتحرك وساكن وظاهر وكامن ومؤمن وكافر وبر وفاجر وغير ذلك الكل مخلوق لله عز وجل مربوب له مسخر بتسخيره مدبر بتدبيره ، ولكل منها رسم يقف عليه وحد ينتهي إليه وكل يجري لأجل مسمى لا يتجاوزه مثقال ذرة ( ذلك تقدير العزيز العليم ) تدبير العدل الحكيم ، وإن أريد به العابد المحب المتذلل خص ذلك بالمؤمنين هم عباده المكرمون ، وأولياؤه المتقون ، الذين لا خوف عليهم ولا هم يحزنون.
‘Abdu ikiwa linakusudiwa mwenye kutezwa nguvu au mtumwa, litakuwa na maana ya vyote vilivyoumbwa mbinguni na ardhini, vyenye akili na visivyo na akili, vibichi na vikavu, vyenye kutembea na kusimama, vyenye kuonekana au kujificha, mwenye kuamini na asiyeamini, mwema na muovu, na vinginevyo. Vyote hivyo ni viumbe vya Allaah (سبحانه وتعالى) vyenye kulelewa Naye, na vyenye kudhalilishwa Kwake, vyenye kupangwa kwa mpangilio Wake, vyote vyenye kuwa katika mipaka Yake, na kila vyote kupita katika makadirio Yake ambavyo havichupi mipaka Yake japo chembe. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٣٨﴾
Hiyo ni takdiri ya Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote. [Yaasiyn: 38]
Mpangaji kwa uadilifu, Mwingi wa hekima. Na likikusudiwa mja, mpenzi, mwenye kunyenyekea, hivyo atanasibishwa katika kundi la Waumini, miongoni mwa waja Wake Allaah (سبحانه وتعالى) waliokirimiwa na katika vipenzi Vyake wenye taqwa, ambao hawana khofu wala huzuni.