004-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: 'Ibaadah Ni Nini?
200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
004-‘Ibaadah Ni Nini?
Swali:
ماهي العبادة؟
‘Ibaadah ni nini?
Jibu:
العبادة هي: اسم جامع لكل مايحبه الله ويرضاه من الأقوال والأعمال الظاهرة والباطنة والبراءة مما ينافي ذلك ويضاده
Neno ‘Ibaadah ni: Jina lenye kukusanya kila jambo Alipendalo Allaah (سبحانه وتعالى) na kuliridhia, miongoni mwa kauli za wazi na za ndani, na kuepukana na yale Asioyaridhia na matakwa Yake.
