06-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Imethibitika Mwanzoni na Mwishoni Wa Uhai Wa Binaadamu
Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd
06-Tawhiyd Imethibitika Mwanzoni na Mwishoni Wa Uhai Wa Binaadamu
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
وَهُوَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ وَالْآخِرَةِ ۖ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٧٠﴾
Naye ni Allaah, Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye. Ni Zake Pekee Himidi za mwanzoni (duniani) na za Aakhirah. Na hukumu ni Yake Pekee, na Kwake Pekee mtarejeshwa. [Al-Qaswasw: 70]
Mwanzoni kabla ya uhai:
هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾
Yeye Ndiye Aliyekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan: 6]
Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٦﴾
Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, kisha Akamfanya humo mkewe na Akakuteremshieni katika wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo Ndiye Rabb wenu Ana ufalme, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, basi vipi mnageuzwa? [Az-Zumar: 6]
Mwishoni:
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا ﴿٨٧﴾
Allaah; hapana muabudiwa wa haki ila Yeye. Bila ya shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah haina shaka ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah? [An-Nisaa: 87]