05-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Mwenyewe Ameshuhudia Tawhiyd

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

05-Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Mwenyewe Ameshuhudia Tawhiyd

 

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amethibitisha Tawhiyd Mwenyewe katika Aayah kadhaa; baadhi yake zifuatazo:  

 

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

Allaah Ameshuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.  [Aal-‘Imraan: 18]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa):  

 

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

 Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.  [Al-Baqarah: 163]

 

 

Alipompa Nabiy Muwsaa Ujumbe Alisema:

 

 

إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي﴿١٤﴾

  “Hakika mimi ni Allaah hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi niabudu, na simamisha Swalaah kwa ajili ya kunidhukuru.”  [Twaahaa: 14]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ ﴿٩٢﴾

“Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja; Nami ni Rabb wenu, basi niabuduni.”    [Al-Anbiyaa: 92]

 

 هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ﴿٢٢﴾

Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri, Yeye Ndiye Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye ukubwa na uadhama, Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha.

 

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾

Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.   [Al-Hashr: 22-24]

 

 

Share