11-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Neno La Tawhiyd Ni Miongoni Mwa Maneno Ayapendao Allaah Na Rasuli

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

11-Neno La Tawhiyd Ni Miongoni Mwa Maneno Ayapendayo Allaah

Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

 

 

 

 

 

Kutoka kwa Samurah bin Jundub (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) ambaye amesema:

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((أَحًبُّ الْكَلامِ إِلَى اللَّهِ أَرْبَعٌ: سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلا إِلَهَ إِلا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، لا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Bora ya maneno kwa Allaah ni manne: Subhaana-Allaah, walhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar, wa laa hawla wa laa quwwata illaa biLLaah - Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahikii Allaah, na  hapana muabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa.… si vibaya kuanza kwa lolote katika hayo))  [Muslim]

 

Na Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu):

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((لأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، والحَمْدُ للهِ، وَ لاَ إَلَهَ إلاَّ اللهُ، واللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إَلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ))

Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kusema kwangu: Subhaana-Allaah, WalhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar- Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana muabudiwa wa haki  ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa.… ni bora kwangu kuliko kila kilichoangaziwa na jua))   [Muslim]

 

Na Hadiyth ya ya Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu):

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((إِنَّ أَفْضَلَ الدُّعَاءِ: الْحَمْدُ لِلَّه، وَأَفْضَلُ الذِّكْرِ: لاَ إلَهَ إِلاَّ الله))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Bora ya du’aa ni mtu kusema: AlhamduliLLaah- Himdi Anstahiki Allaah, na dhikri bora ni: laa ilaaha illa-Allaah - hapana muabudiwa wa haki ila Allaah)) [At-Tirmidhiy, ibn Maajah. Al-Haakim na ameisahihisha na ameiwafiki Adh-Dhahaby na angalia: Swahiyh Al-Jaami (1/362) [1104]

 

Na maneno hayo yana thawabu nzito, mbele ya Allaah na ndiyo ’amali zinazotangulia na kubakia Aakhirah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾

Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Rabb wako, kwa thawabu na matumaini.  [Al-Kahf: 46]

 

Akataja Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuhusu Aayah hiyo kuwa miongoni mwa 'amali zilokusudiwa ni kusema pia: Subhaana Allaah, wal-HamduliLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar[Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

Share