12-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Vitabu Vya Mbinguni Vimeteremshwa Kuamrisha Tawhiyd
Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd
12-Vitabu Vya Mbinguni Vimeteremshwa Kuamrisha Tawhiyd
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿١﴾
Hawakuwa wale waliokufuru miongoni mwa Ahlil-Kitaabi na washirikina wenye kujitenga na hali waliyonayo mpaka iwafikie hoja bayana.
رَسُولٌ مِّنَ اللَّـهِ يَتْلُو صُحُفًا مُّطَهَّرَةً ﴿٢﴾
Rasuli kutoka kwa Allaah anawasomea Sahifa zenye kutakaswa.
فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ ﴿٣﴾
Ndani yake humo mna maandiko yaliyonyooka sawasawa.
وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿٤﴾
Na hawakufarikiana wale waliopewa kitabu isipokuwa baada ya kuwajia hoja bayana.
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾
Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al-Bayyinah: 1-5]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾
Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na dhuriya, na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, Na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr. [An-Nisaa: 163]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
الم ﴿١﴾
Alif Laam Miym.
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴿٢﴾
Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu.
نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾
Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na AkateremshaTawraat na Injiyl.
مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾
Kabla (ya kuteremshwa Qur-aan), iwe ni mwongozo kwa watu na Akateremsha pambanuo (la haki na batili). Hakika wale waliokufuru Aayaat za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kuangamiza. [Aal-‘Imraan: 1-4]
Na Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ﴿١﴾
Alif Laam Raa. Kitabu ambacho Aayaat Zake zimetimizwa barabara, kisha zikafasiliwa waziwazi kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.
أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ﴿٢﴾
Kwamba: “Msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi (Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mwonyaji kwenu na mbashiriaji.” [Huwd: 1-2]
Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kutokana na Hadiyth ya Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu):
((الْأَنْبِيَاءُ إِخْوَةٌ مِنْ عَلَّاتٍ، وَأُمَّهَاتُهُمْ شَتَّى، وَدِينُهُمْ وَاحِد))
((Manabii ni ndugu kwa baba na mama zao ni mbalimbali, na Dini yao ni moja)) [Muslim]
Wanasema ‘Ulamaa kutokana na Hadiyth hii kuwa, asli ya iymaan ya Manabii wote ni moja, na Shariy’ah zao ni tofauti, lakini wote wanaungana na kuafikiana wote kwa Tawhiyd yao ambayo ni moja.