Ibaadah Tatu Usiache Maishani Mwako: 2-Wasiya Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Swalaah Ya Dhwuhaa
'Ibaadah Tatu Usiache Kutenda Maishani Mwako
Wasiya Wa Pili Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Swalaah ya Dhwuhaa
Imetajwa pia katika Hadiyth ya Abu Ad-Dardaai kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemuusia naye mambo matatu kama aliyomuusia Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu), nayo ni: Swiyaam (kufunga) siku tatu, kuswali Swalaah ya Dhwuhaa na kuswali Swalaah ya Witr kabla ya kulala:
وعَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رضي الله عنه قَالَ : "أَوْصَانِي حَبِيبِي صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِثَلَاثٍ لَنْ أَدَعَهُنَّ مَا عِشْتُ : بِصِيَامِ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ، وَصَلَاةِ الضُّحَى وَبِأَنْ لَا أَنَامَ حَتَّى أُوتِرَ" رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu Ad-Dardaai (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: “Ameniusia mpenzi wangu Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam mambo matatu nisiyaache maishani mwangu; Swiyaam (kufunga) siku tatu kila mwezi na Swalaah ya Dhwuhaa na nisilale mpaka niswali Witr” [Muslim]
Swalaah ya Dhwuhaa – Fadhila zake, idadi ya Rakaa zake na wakati wake:
عـَن أبي ذَرٍّ رضي الله ُ عنه ، عن النـَبي ِّ صلـَّى الله عليه وسلم قال: ((يـُصـْبـِحُ عـَلى كـُلِّ سـُلامى مـِنْ أحـَدِكـُمْ صـَدَقةُ: فـَكُل تـَسْبـِيحـَةِ صـَدَقةٌ ،وَ كُل تـَحمِيدة صـَدَقةٌ ، وكُلُ تـَهْـليْلةٌ صـَدَقـَةٌ، وكُلُّ تـَكْبِيْرةِ صـَدقةٌ ، وأمرٌ بالمـَعرُوف صـَدقةٌ ، ونـَهىٌ عـَنِ المـُنْكرِ صـَدقةٌ ويـُجْزئ مـِنْ ذلكَ رَكـْعتـَانِ يـَركَعُهُما مـنَ الضـُّحى)) رواه مسلم
Kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kila kiungo cha mwili wa mmoja wenu kinahitajika kutolewa swadaqah inapofika asubuhi. Na kila tasbiyh (Subhaana Allaah) ni swadaqah kila tahmiyd (AlhamduliLLaah) ni swadaqah na kila tahliyl (La Ilaaha Illa Allaah) ni swadaqah na kila takbiyr (Allaahu Akbar) ni swadaqah na kuamrisha mema ni swadaqah na kukataza maovu ni swadaqah na itamtosheleza (mtu) kwa Rakaa mbili za Adhw-Dhwuhaa)) [Muslim]
Na pia,
عنْ أَبِي بُرَيْدَةَ :"سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((فِي الْإِنْسَانِ سِتُّونَ وَثَلَاثُ مِائَةِ مَفْصِلٍ فَعَلَيْهِ أَنْ يَتَصَدَّقَ عَنْ كُلِّ مَفْصِلٍ مِنْهَا صَدَقَةً قَالُوا فَمَنْ الَّذِي يُطِيقُ ذَلِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ النُّخَاعَةُ فِي الْمَسْجِدِ تَدْفِنُهَا أَوْ الشَّيْءُ تُنَحِّيهِ عَنْ الطَّرِيقِ فَإِنْ لَمْ تَقْدِرْ فَرَكْعَتَا الضُّحَى تُجْزِئُ عَنْكَ)) صحيح ، المشكاة ( 1315 ) ، الإرواء (2 / 213 )
Abu Buraydah amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah akisema: “Bin-Aadam ana viungo miatu na siitini [360] anapaswa kwa kila kiungo kimoja akitolee swadaqah.” Wakasema: Nanai atakayeweza hivyo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Kufukia kamasi (au kohozi) katika Masjid au kuondosha kitu cha madhara njiani. Usipoweza basi Rakaa mbili za Adhw-Dhwuhaa zinatosheleza hayo.” [Sunan Abi Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika: Swahiyh Al-Miskhaat (1315), Al-Irwaa (2/213)]
Na pia,
عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ و أَبِي ذَرٍّ رضي الله عنهما عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ أَنَّهُ قَالَ : ((ابْنَ آدَمَ ارْكَعْ لِي مِنْ أَوَّلِ النَّهَارِ أَرْبَعَ رَكَعَاتٍ، أَكْفِكَ آخِرَهُ)) رواه الترمذي (437) ، وصححه الشيخ الألباني .
Imepokelewa kutoka kwa Abu Ad-Dardaai na Abu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Allaah ‘Azza wa Jalla Amesema: ((Ee mwanadamu Swali kwa ajili mwanzo wa mchana Rakaa nne, Nitakuwa tosha yako wakati wa mwisho wake (Utakuwa katika kinga ya Allaah mpaka jioni))) [At-Tirmidhiy 475, Abu Daawuwd 1289 na Shaykh Al-Albaaniy katika Al-Irwaaul-Ghaliyl 1465].
Idadi Ya Rakaa zake:
Kauli za ‘Ulamaa kuhusu idadi zake:
Kauli ya kwanza: Wingi wa Rakaa zake kwa mujibu wa madhehebu Maalikiyyah, Shafiiyyah, na Hanaabilah ni rakaa nane; ushahidi wao ni Hadiyth ya:
عـَن أُمِّ هـَانئ رضي الله عنها قالت : ذَهَبتُ إلى رسول ِ الله ِ صلى الله عليه وسلم عام الفـَتْح فـَوَجـَدْتُهُ يـَغْتـَسِل فـَلـَمَّا فـَرَغَ مـِنْ غـُسْلِه صَـلى ثـَمانيَ رَكَعاتٍ ، وذَلكّ الضـُّحى" ـ متفق عليه
Ummu Haaniy (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: “Nilikwenda (nyumbani) kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwaka ulipofunguliwa mji wa Makkah nikamkuta anajiosha, alipomaliza aliswali rakaa nane na hiyo ni Adhw-Dhwuhaa.”
Kauli ya pili: Ni kauli ya jamhuri ya ‘Ulamaa. Wao wamesema Swalaah ya Dhwuhaa haina idadi maalumu kwa ushahidi wa Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa):
كَان رسولُ الله ِ صـَلى الله عليه وسلم يـُصـَلْي الضُّحـَى أرْبـَعاً، ويـَزيدُ ما شـَاءَ الله ـ رواه مسلم
Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Adhw-Dhwuhaa nne na huongeza Maa Shaa Allaah (Anavyomwezesha Allaah)” [Muslim]
Wakati wake:
Wakati wa Swalaah ya Dhwuhaa unaanzia robo saa mara baada ya kuchomoza kwa jua, mpaka kabla ya kuingia kwa wakati wa Adhuhuri, yaani kama robo saa hivi ili usije kuingia wakati wa makruwh (uliochukiza kuswaliwa). Lakini wakati ulio bora kabisa ni pale jua limeshaanza kuwaka na mchanga umeshashika moto kwa dalili ifuatayo:
عَنْ زَيْدِ بْنِ أَرْقَمَ قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى أَهْلِ قُبَاءَ وَهُمْ يُصَلُّونَ فَقَالَ : ((صَلاةُ الأَوَّابِينَ إِذَا رَمِضَتْ الْفِصَالُ )) رواه مسم
Kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka akawaona watu wa Qubaa wanaswali akasema: ((Swalah ya Al-Awwaabiyn ni wakati ngamia wachanga wananyanyua miguu yako)) [Muslim].
Imeitwa Swalaah ya Al-Awwaabiyn kwa sababu ya umoto wa mchanga uliopigwa na jua kali.
Swalaah inayojulikana kama ni Swalaatul-Ishraaq au shuruwq (Swalaah baada ya kuchomoza jua) pia inaingia katika Swalaah ya Dhwuhaa isipokuwa Swalaah hii inasaliwa mapema katika wakati wake maalumu nao ni baada ya kuchomoza jua kwa maelezo yake na fadhila zake kama ilivyothibiti katika Hadiyth yaifuatayo:
من حديث أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه ((مَنْ صَلَّى الْغَدَاةَ فِي جَمَاعَةٍ ثُمَّ قَعَدَ يَذْكُرُ اللَّهَ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ ، ثُمَّ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ ، كَانَتْ لَهُ كَأَجْرِ حَجَّةٍ ، وَعُمْرَةٍ ، تَامَّةٍ ، تَامَّةٍ ، تَامَّةٍ)) رواه الترمذي (586).
Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jamaa kisha akakaa anamdhukuru Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Rakaa mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhiy 586 na kaisahihisha Al-Albaaniy]