Imaam Al-Albaaniy: Ugeni Wa Ahlus-Sunnah

 

 Ugeni Wa Ahlus-Sunnah

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Amesema Al-Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah):

 

Iwapo utazungumza kuhusiana na Tawhiyd, watakupinga (na kukuacha) watu wa Shirk.

 

Na iwapo utazungumza kuhusiana na Sunnah, watakupinga (na kukuacha ) watu wa bid'ah.

 

Na iwapo utazungumza kuhusiana na kufuata dalili na hoja, watukupinga (na kukuacha) watu walioshikamana na (Ta'aswub) kasumba za kimadhehebu na watu wa bid'ah na Masufi na ujinga.

 

Na iwapo utazungumza kuhusiana na kuwatii Viongozi wenye mamlaka, na kuwaombea du'aa na kuwanasihi, na (pia ukazungumzia) 'Aqiydah ya Ahlus-Sunnah, watakupinga (na kukuacha) Khawaarij na Watu wa Makundi (Wanaharakati).

 

Na iwapo utazungumzia kuhusu Uislamu na mafungamano yake kwa Maisha ya Mwana Aadam watakupinga Wasiotaka shariy'ah za Dini na Maliberali na mfano wao ambao wanataka kuitenganisha Dini na Maisha ya Mwana Aadam.

 

Ugeni (unaonekana katika jamii) mkubwa walionao Ahlus-Sunnah (Kila kundi linawapinga) na kuwaacha.

 

Wametupiga vita kwa njia zote wametupiga vita matangazo na kwa njia za mawasiliano (media) za kusikika (maradio), za kutazamwa (matelevisheni) na za kuandikwa (magazeti) n.k.

 

Hadi imefikia, jamaa wa karibu na marafiki wanampiga vita 'Mgeni' huyu Mwenye kushikamana na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah (Hadiyth) za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na pamoja na yote hayo...

 

Sisi ni wenye furaha na huu 'Ugeni', na tunajifakharisha nao, kwa sababu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kawasifia hawa 'Wageni' kwa kusema:

"Ulianza Uislamu katika hali ya Ugeni, na utarejea mgeni kama ulivyoanza, basi furaha ni kwa wale Wageni." Akaulizwa, ni nani hao Wageni ee Mjumbe wa Allaah? Akajibu: "Ni wale watengenezao vizuri pindi wanapoharibu watu."

 

 [As-Silsilat Asw-Swahiyhah, Hadiyth namba 1273]

 

Share