Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Tujifakharishe Na Nembo Za Kiislamu Tusiige Wamagharibi Kusema Byebye!
Tujifakharishe Na Nembo Za Kiislamu, Tusiige Wamagharibi
Kuamkiana Kwa "Assalaamu 'Alaykum" Badala Ya "Bye-bye"
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Muhammad bin Swaalih Al-'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Na baya zaidi walifanyalo baadhi ya wapumbavu ambao wamekatwa pumzi na nguvu za kimada za ki-Magharibi (wazungu) hadi wakafikia kuona kuwa:
- Maendeleo
- Kupiga hatua mbele
(hakupatikani) ila kwa kuwaiga wao hata katika zile nembo za dini.
- Maendeleo
- Kupiga hatua mbele
(hakupatikani) ila kwa kuwaiga wao hata katika zile nembo za dini.
Hadi inafikia baadhi yao (wanapoagana) wanasema, 'bye bye' badala ya kusema, 'Assalaamu 'Alaykum'!
Na huenda wanawafundisha watoto wao kusema hivyo kama tulivyowasikia kiuhakika watoto wakisema hivyo pindi akiondoka (mmoja wao), au wakiachana, (huagana) kwa kusema, 'bye bye'!
Hayaji haya isipokuwa kutoka kwa mafunzo ya wazazi wao ambao ni:
- Dhaifu wa Nafsi.
- Dhaifu wa kiutu na kitabia (kishakhswiyah).
- Dhaifu wa Nafsi.
- Dhaifu wa kiutu na kitabia (kishakhswiyah).
Muislamu anapaswa awe mtukufu (mwenye nguvu, imara, hayumbi) kwa:
- Uislamu wake na Dini yake
- Na ajifakharishe anapoitekeleza shariy'ah ya Dini yake.
- Kwa nafsi yake.
- Kwa waja wa Allaah.
- Uislamu wake na Dini yake
- Na ajifakharishe anapoitekeleza shariy'ah ya Dini yake.
- Kwa nafsi yake.
- Kwa waja wa Allaah.
Kisha tambua kuwa kishariy'ah ni:
- Mdogo kumsalimia mkubwa.
- Wachache kuwasalimia wengi.
- Aliye juu ya kipando/usafiri anamsalimia mwenye kutembea kwa miguu.
- Anayetembea anamsalimia aliyekaa.
- Mdogo kumsalimia mkubwa.
- Wachache kuwasalimia wengi.
- Aliye juu ya kipando/usafiri anamsalimia mwenye kutembea kwa miguu.
- Anayetembea anamsalimia aliyekaa.
Endapo itapatikana kutekelezeka Sunnah hii, basi hilo ni bora zaidi.
[Nuwru 'Alaa Ad-Darb, mkanda wa 338]