Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Wajibu Wa Kumkirimu Mwalimu Wako
Wajibu Wa Kumkirimu Mwalimu Wako
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Aliulizwa mmoja katika waliotangulia:
"Kwanini unamkirimu Mwalimu wako kuliko unavyomkirimu au kushinda ukarimu kwa baba yako?
Akajibu:
Hakika Baba yangu ni sababu ya maisha yangu haya yenye kwisha (Dunia)!
Na Mwalimu wangu ni sababu ya maisha yangu yaliyobakia (Aakhirah)."
Maneno ya busara na ya hali halisi mfano wa haya, aliyasema vilevile Mwanachuoni, Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah).