014 - Ibraahiym
إِبْرَاهِيم
014-Ibraahiym
014-Ibraahiym: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa.[1] Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwatoe watu kutoka kwenye viza kuwaingiza katika nuru[2] kwa Idhini ya Rabb wao, waelekee katika njia ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ ﴿٢﴾
2. Naye ni Allaah Ambaye ni Vyake vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na ole kwa makafiri kwa adhabu kali.
الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ ﴿٣﴾
3. Ambao wanasitahabu uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah, na wanazuia Njia ya Allaah, na wanaitafutia upogo. Hao wamo katika upotofu wa mbali.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ فَيُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٤﴾
4. Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake ili awabainishie (Risala). Basi Allaah Humpotoa Amtakaye na Humhidi Amtakaye. Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا أَنْ أَخْرِجْ قَوْمَكَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَذَكِّرْهُم بِأَيَّامِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ﴿٥﴾
5. Na kwa yakini Tulimpeleka Muwsaa akiwa pamoja na Aayaat (Ishara, Miujiza, Dalili) Zetu (Tukimwambia): Itoe kaumu yako kutoka kwenye viza kwenda katika nuru, na wakumbushe Siku za Allaah.[3] Hakika katika hayo kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa kila mwingi wa kusubiri na kushukuru.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ أَنجَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ وَيُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٦﴾
6. Na pindi Muwsaa alipoiambia kaumu yake: Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, Alipokuokoeni kutokana na watu wa Firawni walipokusibuni adhabu mbaya, na wakiwachinja watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu. Na katika hayo ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Rabb wenu.
وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ وَلَئِن كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ﴿٧﴾
7. Na pindi Alipotangaza Rabb wenu: Ikiwa mtashukuru, bila shaka Nitakuzidishieni (Neema Zangu), na mkikufuru, basi hakika Adhabu Yangu ni kali.
وَقَالَ مُوسَىٰ إِن تَكْفُرُوا أَنتُمْ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا فَإِنَّ اللَّـهَ لَغَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٨﴾
8. Na Muwsaa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote walioko ardhini, basi hakika Allaah Ni Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ ۛ وَالَّذِينَ مِن بَعْدِهِمْ ۛ لَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا اللَّـهُ ۚ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرَدُّوا أَيْدِيَهُمْ فِي أَفْوَاهِهِمْ وَقَالُوا إِنَّا كَفَرْنَا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ وَإِنَّا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَنَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ ﴿٩﴾
9. Je, haijakufikieni khabari ya wale wa kabla yenu; watu wa Nuwh, na ‘Aad na Thamuwd, na wale wa baada yao? Hakuna Awajuao isipokuwa Allaah. Rusuli wao waliwajia kwa hoja bayana, nao wakarudisha mikono yao katika vinywa vyao[4] na wakasema: Hakika sisi tumeyakanusha yale mliyotumwa nayo, na hakika sisi tumo katika shaka kutokana na mnayotuitia kwayo na tunayashuku.
قَالَتْ رُسُلُهُمْ أَفِي اللَّـهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَدْعُوكُمْ لِيَغْفِرَ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرَكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ قَالُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا تُرِيدُونَ أَن تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا فَأْتُونَا بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿١٠﴾
10. Wakasema Rusuli wao: Je, kuna shaka kuhusiana na Allaah, Muanzilishi wa mbingu na ardhi? Anakuiteni ili Akughufurieni madhambi yenu na Akuakhirisheni mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Wakasema: Nyinyi si chochote isipokuwa ni watu tu kama sisi, mnachotaka ni kutuzuia tu na yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu. Basi tuleteeni uthibitisho bayana.
قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِن نَّحْنُ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَمَا كَانَ لَنَا أَن نَّأْتِيَكُم بِسُلْطَانٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾
11. Wakasema Rusuli wao: Sisi si chochote isipokuwa ni watu tu kama nyinyi, lakini Allaah Anamfadhilisha Amtakaye miongoni mwa Waja Wake. Na haitupasi sisi kuwaleteeni uthibitisho isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Na kwa Allaah watawakali Waumini.
وَمَا لَنَا أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانَا سُبُلَنَا ۚ وَلَنَصْبِرَنَّ عَلَىٰ مَا آذَيْتُمُونَا ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُتَوَكِّلُونَ ﴿١٢﴾
12. Na tuna nini (sisi) hata tusitawakali kwa Allaah na hali Amekwishatuongoza njia yetu? Na kwa yakini tutasubiri juu ya maudhi yenu kwetu. Na kwa Allaah watawakali wanaotawakali.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِرُسُلِهِمْ لَنُخْرِجَنَّكُم مِّنْ أَرْضِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۖ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ لَنُهْلِكَنَّ الظَّالِمِينَ ﴿١٣﴾
13. Wakasema wale waliokufuru kuwaambia Rusuli wao: Lazima tutakutoeni katika ardhi yetu, au mtarudi kwa nguvu katika dini yetu. Basi Rabb wao Akawafunulia Wahy kwamba: Hakika Tutawahiliki madhalimu.
وَلَنُسْكِنَنَّكُمُ الْأَرْضَ مِن بَعْدِهِمْ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَافَ مَقَامِي وَخَافَ وَعِيدِ ﴿١٤﴾
14. Na bila shaka Tutakuwekeni maskani katika ardhi baada yao. Haya ni kwa yule anayekhofu kusimamishwa mbele Yangu na akakhofu Maonyo Yangu.
وَاسْتَفْتَحُوا وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ﴿١٥﴾
15. Na wakaomba ushindi (kwa Allaah), na akapita patupu kila (aliyejifanya) jabari, mkaidi.
مِّن وَرَائِهِ جَهَنَّمُ وَيُسْقَىٰ مِن مَّاءٍ صَدِيدٍ ﴿١٦﴾
16. Nyuma yake kuna Jahannam, na atanyweshwa maji ya usaha.
يَتَجَرَّعُهُ وَلَا يَكَادُ يُسِيغُهُ وَيَأْتِيهِ الْمَوْتُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَمَا هُوَ بِمَيِّتٍ ۖ وَمِن وَرَائِهِ عَذَابٌ غَلِيظٌ ﴿١٧﴾
17. Atayagugumia kwa tabu na atakurubia asiweze kuyameza yakashuka kooni, na yatamjia mauti kutoka kila upande, naye hatokufa hata kidogo. Na nyuma yake kuna adhabu nzito.[5]
مَّثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ ۖ أَعْمَالُهُمْ كَرَمَادٍ اشْتَدَّتْ بِهِ الرِّيحُ فِي يَوْمٍ عَاصِفٍ ۖ لَّا يَقْدِرُونَ مِمَّا كَسَبُوا عَلَىٰ شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٨﴾
18. Mfano wa wale waliomkufuru Rabb wao, amali zao ni kama jivu linalopeperushwa kwa nguvu za upepo siku ya dhoruba. Hawatoweza kupata chochote katika yale waliyoyachuma. Huo ndio upotofu wa mbali.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿١٩﴾
19. Je, huoni kwamba Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Akitaka Atakuondosheleeni mbali na Alete viumbe vipya.
وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ بِعَزِيزٍ ﴿٢٠﴾
20. Na hilo halina uzito wowote kwa Allaah.
وَبَرَزُوا لِلَّـهِ جَمِيعًا فَقَالَ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا مِنْ عَذَابِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۚ قَالُوا لَوْ هَدَانَا اللَّـهُ لَهَدَيْنَاكُمْ ۖ سَوَاءٌ عَلَيْنَا أَجَزِعْنَا أَمْ صَبَرْنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٍ ﴿٢١﴾
21. Na watahudhuria wote mbele ya Allaah. Wanyonge watawaambia wale waliotakabari: Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu (tukikutiini), basi je, nyinyi mtaweza kutuondolea chochote katika Adhabu ya Allaah? Watasema: Kama Allaah Angetuhidi, bila shaka tungelikuongozeni. Ni sawasawa kwetu tukipapatika au tukisubiri, hatuna mahali pa kukimbilia.
وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّـهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدتُّكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ ۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنفُسَكُم ۖ مَّا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنتُم بِمُصْرِخِيَّ ۖ إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِن قَبْلُ ۗ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٢﴾
22. Na shaytwaan atasema litakapokidhiwa jambo: Hakika Allaah Alikuahidini ahadi ya haki (na Ameitimiza), nami nilikuahidini kisha nikakukhalifuni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu isipokuwa nilikuiteni mkaniitikia. Basi msinilaumu, bali laumuni nafsi zenu. Mimi siwezi kukusaidieni kukuokoeni wala nyinyi hamuwezi kunisaidia kuniokoa. Hakika mimi nilikanusha yale mliyonishirikisha zamani. Hakika madhalimu watapata adhabu iumizayo.[6]
وَأُدْخِلَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ ۖ تَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ﴿٢٣﴾
23. Na wataingizwa wale walioamini na wakatenda mema, Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo kwa Idhini ya Rabb wao. Maamkizi yao humo yatakuwa ni Salaam.
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ ﴿٢٤﴾
24. Je, huoni vipi Allaah Amepiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri,[7] mizizi yake imethibitika imara na matawi yake yanafika mbinguni.
تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٥﴾
25. Unatoa mazao yake kila wakati kwa Idhini ya Rabb wake. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu ili wapate kukumbuka.
وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٍ ﴿٢٦﴾
26. Na mfano wa neno baya ni kama mti mbaya uliong’olewa juu ya ardhi hauna uimara.
يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ﴿٢٧﴾
27. Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhira.[8] Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ﴿٢٨﴾
28. Je, huoni wale waliobadilisha Neema ya Allaah kwa kufru, na wakawafikisha watu wao nyumba ya mateketezo?
جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا ۖ وَبِئْسَ الْقَرَارُ ﴿٢٩﴾
29. Jahannam wataiingia na kuungua, na ubaya ulioje mahala pa kutulia!
وَجَعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلُّوا عَن سَبِيلِهِ ۗ قُلْ تَمَتَّعُوا فَإِنَّ مَصِيرَكُمْ إِلَى النَّارِ ﴿٣٠﴾
30. Na wakamfanyia Allaah walinganishi ili wapoteze (watu) na Njia Yake. Sema: Stareheni! Kwani hakika mahali penu pa kurudia hatimaye ni motoni.
قُل لِّعِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا يُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خِلَالٌ ﴿٣١﴾
31. Waambie (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Waja Wangu ambao wameamini: Wasimamishe Swalaah na watoe katika yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri kabla haijafika Siku ambayo hakutakuweko biashara wala urafiki wa kweli.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ﴿٣٢﴾
32. Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi, na Akateremsha maji kutoka mbinguni, Akatoa kwayo mazao kuwa ni riziki kwenu. Na Akakutiishieni majahazi ili yapite baharini kwa Amri Yake. Na Akakutiishieni mito.
وَسَخَّرَ لَكُمُ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ دَائِبَيْنِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ﴿٣٣﴾
33. Na Akakutiishieni jua na mwezi vinavyozunguka daima dawamu na Akakutiishieni usiku na mchana.
وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ الْإِنسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ ﴿٣٤﴾
34. Na Akakupeni kila mlichomuomba. Na mkihesabu Neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni.[9] Hakika binaadam ni mwingi wa dhulma, mwingi wa kukufuru.
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا الْبَلَدَ آمِنًا وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ ﴿٣٥﴾
35. Na Ibraahiym aliposema: Ee Rabb wangu! Ujaalie mji huu (Makkah) uwe wa amani, na Uniepushe na wanangu kuabudu masanamu.[10]
رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ۖ وَمَنْ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٦﴾
36. Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza watu wengi. Basi atakayenifuata, huyo yuko nami, na atakayeniasi, basi hakika Wewe Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾
37. Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu (Al-Ka’bah), ee Rabb wetu ili wasimamishe Swalaah. Basi Zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru.
رَبَّنَا إِنَّكَ تَعْلَمُ مَا نُخْفِي وَمَا نُعْلِنُ ۗ وَمَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِن شَيْءٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٣٨﴾
38. Rabb wetu! Hakika Wewe Unajua tunayoyaficha na tunayoyadhihirisha. Na hakifichiki kitu chochote kwa Allaah katika ardhi wala katika mbingu.
الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٩﴾
39. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Amenitunukia juu ya umri mkubwa wangu Ismaa’iyl na Is-haaq. Hakika Rabb wangu bila shaka Ni Mwenye Kusikia duaa yangu.
رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ﴿٤٠﴾
40. Rabb wangu! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swalaah pamoja na dhuria wangu. Rabb wetu! Nitakabalie duaa yangu.
رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾
41. Rabb wetu! Nighufurie mimi na wazazi wangu wawili[11] na Waumini Siku itakayosimama hesabu.
وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّـهَ غَافِلًا عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ ۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ ﴿٤٢﴾
42. Na wala usidhanie kabisa kwamba Allaah Ameghafilika na yale wanayoyatenda madhalimu. Hakika Anawaakhirisha kwa ajili ya Siku ambayo macho yatakodoka.
مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لَا يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ ۖ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ ﴿٤٣﴾
43. Watoke haraka haraka (makaburini), wakiwa wamenyanyua vichwa vyao juu, macho yao hayapepesi na nyoyo zao ni tupu (kwa kiwewe na huzuni).
وَأَنذِرِ النَّاسَ يَوْمَ يَأْتِيهِمُ الْعَذَابُ فَيَقُولُ الَّذِينَ ظَلَمُوا رَبَّنَا أَخِّرْنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ نُّجِبْ دَعْوَتَكَ وَنَتَّبِعِ الرُّسُلَ ۗ أَوَلَمْ تَكُونُوا أَقْسَمْتُم مِّن قَبْلُ مَا لَكُم مِّن زَوَالٍ﴿٤٤﴾
44. Na waonye watu Siku itakayowafikia adhabu, na wale waliodhulumu waseme: Rabb wetu! Tuakhirishe mpaka muda mdogo ili tuitikie Wito Wako na tuwafuate Rusuli. (Wataambiwa): Je, kwani hamkuwa mmeapa kabla kwamba hamtokuwa wenye kuondoshwa (duniani?).
وَسَكَنتُمْ فِي مَسَاكِنِ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ وَتَبَيَّنَ لَكُمْ كَيْفَ فَعَلْنَا بِهِمْ وَضَرَبْنَا لَكُمُ الْأَمْثَالَ ﴿٤٥﴾
45. Na mkakaa katika maskani za wale waliodhulumu nafsi zao na ikakubainikieni vipi Tulivyowafanya, na Tukakupigieni mifano mingi?
وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِندَ اللَّـهِ مَكْرُهُمْ وَإِن كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ﴿٤٦﴾
46. Na kwa yakini wamefanya mipango ya makri zao, na kwa Allaah kuna (rekodi ya) makri zao japokuwa makri zao haziwezi kuondosha milima.
فَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّـهَ مُخْلِفَ وَعْدِهِ رُسُلَهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤٧﴾
47. Basi usidhanie kabisa kwamba Allaah Ni Mwenye Kukhalifu Ahadi Yake kwa Rusuli Wake. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza.
يَوْمَ تُبَدَّلُ الْأَرْضُ غَيْرَ الْأَرْضِ وَالسَّمَاوَاتُ ۖ وَبَرَزُوا لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿٤٨﴾
48. Siku ardhi itakapobadilishwa kuwa ardhi nyingine[12] na mbingu pia, na (viumbe wote) watahudhuria kwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika.
وَتَرَى الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ مُّقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ ﴿٤٩﴾
49. Na utawaona wahalifu Siku hiyo wamezongoreshwa katika minyororo.
سَرَابِيلُهُم مِّن قَطِرَانٍ وَتَغْشَىٰ وُجُوهَهُمُ النَّارُ﴿٥٠﴾
50. Mavazi yao ni ya lami na moto utafunika nyuso zao.
لِيَجْزِيَ اللَّـهُ كُلَّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٥١﴾
51. Ili Allaah Alipe kila nafsi yale iliyoyachuma. Hakika Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.
هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ﴿٥٢﴾
52. Hii (Qur-aan) ni ubalighisho wa Risala kwa watu, na ili waonywe kwayo, na ili wapate kujua kwamba hakika Yeye Ni Muabudiwa wa haki Mmoja Pekee, na ili wakumbuke (na wawaidhike) wenye akili.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Viza Na Nuru (Mwanga):
a-Maana Ya Kiza Kilugha:
Ni kutokuweko nuru (mwanga) kama vile kiza cha usiku katika hali ya kutokuweko taa au nyota, au mwezi wa kutoa mwanga kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ
“Au nani Anayekuongozeni katika viza vya nchi kavu na bahari?” [An-Naml (27:63)]
b) Maana Ya Kiza Kiistilahi:
Ni kufru, shirki, unafiki, bid’ah, ujahili, maasi, na kila aina ya upotofu na kadhaalika. Na maelezo yake yanafuatia.
c-Maana Ya Nuru (Mwanga) Kilugha:
Ni mwanga unaodhihirisha vitu kuonekana wazi kama mwanga wa mchana, au mwanga wa taa zinapowashwa usiku.
d-Maana Ya Nuru Kiistilahi:
Ni imaan, taqwa, utiifu, na kila aina ya hidaaya
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn amesema:
[Tafsiyr Suwrah Al-An’aam (6:1)]
Sababu ya kutajwa dhwulumaat (viza) kwa wingi, ni kama walivyosema ‘Ulamaa kwamba kwa sababu vyanzo vyake ni vingi; vinaweza kuwa ni nafsi ya mtu, au hawaa (matamanio), au shaytwaan, taghuti na kadhaalika. Na ndio maana adhwulumaat ikatajwa kwa wingi. Na hivyo inampelekea mtu katika viza vya kufru, shirki, unafiki, bid’ah, ujahili, maasi, na kila aina ya upotofu.
Ama An-Nuwr (mwanga), chanzo chake ni njia moja tu iliyonyooka, nacho ni Kitaabu cha Allaah kinachoongoza katika Swiraatw Al-Mustaqiym (Njia Iliyonyooka). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾ صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ﴿٥٣﴾
“Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh (Qur-aan) kutokana na Amri Yetu. Hukuwa unajua nini Kitabu wala imaan, lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa Waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. Njia ya Allaah Ambaye ni Vyake Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! Kwa Allaah Pekee yanaishia mambo yote.” [Ash-Shuwraa (42:52-52)]
Rejea Suwrah Ibraahiym (13:1-2) kwenye maelezo bayana na faida nyenginezo. Na pia rejea Al-An’aam (6:122).
Amesema Ibnul-Qayyim Al-Jawziyyah (رحمه الله):
“Njia ya haki ni moja, kwani inarejea kwa Allaah Mfalme wa Haki, na njia za baatwili (ubatilifu) ni nyingi. Na hii ni moja katika miujiza ya Qur-aan, kutajwa viza kwa wingi, na Nuru kwa umoja. Hii ina maana kwamba neno viza linajumuisha kila aina ya giza; njia zote potofu zinazoelekea gizani, na hiyo Nuru inaashiria njia moja tu iliyonyooka.” [Badaai’u Al-Fawaaid]
Kumetajwa viza kwa wingi na Nuru kwa umoja katika Aayah kadhaa. Kwanza katika Suwrah hii ya Ibraahiym Aayah namba (1) na Aayah namba (5). Rejea pia Al-Baqarah (2:257), Al-Maaidah (5:16), Al-An’aam (6:1), Ar-Ra’d (13:16), An-Nuwr (24:40), Al-Ahzaab (33:43), Faatwir (35:20), Al-Hadiyd (57:9), Atw-Twalaaq (65:11).
Na duaa imethibiti ya kuomba mtu kutolewa kutoka katika viza na kuingizwa katika Nuru:
حَدَّثَنَا تَمِيمُ بْنُ الْمُنْتَصِرِ، أَخْبَرَنَا إِسْحَاقُ، - يَعْنِي ابْنَ يُوسُفَ - عَنْ شَرِيكٍ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، عَنْ أَبِي الأَحْوَصِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنَّا لاَ نَدْرِي مَا نَقُولُ إِذَا جَلَسْنَا فِي الصَّلاَةِ وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَدْ عَلِمَ فَذَكَرَ نَحْوَهُ . قَالَ شَرِيكٌ وَحَدَّثَنَا جَامِعٌ، - يَعْنِي ابْنَ شَدَّادٍ - عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، بِمِثْلِهِ قَالَ وَكَانَ يُعَلِّمُنَا كَلِمَاتٍ وَلَمْ يَكُنْ يُعَلِّمُنَاهُنَّ كَمَا يُعَلِّمُنَا التَّشَهُّدَ " اللَّهُمَّ أَلِّفْ بَيْنَ قُلُوبِنَا وَأَصْلِحْ ذَاتَ بَيْنِنَا وَاهْدِنَا سُبُلَ السَّلاَمِ وَنَجِّنَا مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَجَنِّبْنَا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَبَارِكْ لَنَا فِي أَسْمَاعِنَا وَأَبْصَارِنَا وَقُلُوبِنَا وَأَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ وَاجْعَلْنَا شَاكِرِينَ لِنِعْمَتِكَ مُثْنِينَ بِهَا قَابِلِيهَا وَأَتِمَّهَا عَلَيْنَا "
Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitufundisha maneno mengine lakini hakuyafundisha kama alivyokuwa akitufundisha Tashahhud:
اللَّهُمَّ أَلِّفْ بَيْنَ قُلُوبِنَا وَأَصْلِحْ ذَاتَ بَيْنِنَا وَاهْدِنَا سُبُلَ السَّلاَمِ وَنَجِّنَا مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَجَنِّبْنَا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَبَارِكْ لَنَا فِي أَسْمَاعِنَا وَأَبْصَارِنَا وَقُلُوبِنَا وَأَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ وَاجْعَلْنَا شَاكِرِينَ لِنِعْمَتِكَ مُثْنِينَ بِهَا قَابِلِيهَا وَأَتِمَّهَا عَلَيْنَا
Ee Allaah! Unganisha baina ya nyoyo zetu, na Suluhisha yaliyo baina yetu, na Tuongoze njia za amani, na Tuokoe kutokana na viza Utuingize katika Nuru, na Tuepushe machafu ya dhahiri na ya siri, na Tubarikie katika kusikia kwetu na kuona kwetu, nyoyo zetu, na wake zetu, na vizazi vyetu, na Tupokelee tawbah zetu, hakika Wewe ni At-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye Kurehemu), na Tujaalie kuwa wenye kushukuru neema Zako, wenye kuzielezea kwa uzuri, wenye kuzipokea (kwa shukrani), na Zitimize kwetu. [Abuu Daawuwd, Al-Haakim kasema: Swahiyh kwa sharti ya Muslim, na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/265) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad (490)]
[3] Siku Za Allaah:
Ayyaamu "أَيَّامٌ", kwa lugha ya kiarabu ni masiku. Lakini masiku kama haya hayamaanishi siku tu, bali ni siku za kumbukumbu ambazo matukio muhimu ya kihistoria yanatokea au yalitokea. Na katika Aayah hii, masiku yaliyokusudiwa ni Neema za Allaah kama walivyosema Ibn ‘Abbaas, Mujaahid, Qataadah na wengineo: Ni Neema za Allaah za kila aina Alizowaneemesha Bani Israaiyl na kheri nyingi Alizowapa kama kuwafunika kwa mawingu na kuwateremshia Al-Manna na As-Salwaa. Rejea Al-Baqarah (2:57). Na pia kuwafanyia ihsaan na kuwaokoa kutokana na Firawni Alipotenganisha bahari wakavuka na akaghariki adui yao Firawni.
[4] Kurudisha Mikono Yao Katika Vinywa Vyao:
Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana katika maoni mbalimbali kuhusu kauli hiyo. Kuna waliosema: Wakaiuma mikono yao kwa hasira na kiburi cha kutotaka kuamini na kukanusha haki. Na hii inaonyesha hasira za makafiri, na kutoweza kwao kuvumilia baada ya kusikia ujumbe wa Rasuli wao. Na hii inathibitishwa na kauli inayoendelea katika Aayah hii tukufu ambapo makafiri hao wanasema wazi kwamba hawakubali Risala ya Rasuli wao na wanaitilia shaka. Hiyo ni aina ya kibri kama kibri cha kuweka vidole vyao masikioni na kujigubika kwa nguo zao wasione wasisikie. Rejea pia Nuwh (71:7).
[5] Makafiri Wataadhibiwa Bila Ya Kufa:
Mwenye kiburi atajaribu kumeza usaha na damu na vinginevyo vinavyotiririka mara kwa mara kutoka kwa watu wa motoni, na hataweza kumeza kwa uchafu wake, kuunguza kwake na uchungu wake. Na adhabu kali ya kila aina itamjia kwenye kila kiungo katika mwili wake. Hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika. Na baada ya adhabu hii, atapatiwa adhabu nyingine yenye kuumiza. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na adhabu za makafiri motoni zimetajwa katika Suwrah kadhaa zikiwemo Al-Kahf (18:29), Muhammad (47:15), Swaad (38:55-57), Asw-Swaaffaat (37:62-68), Ar-Rahmaan (55:43-44), Ad-Dukhaan (44:43-48), Al-Haaqqah (69:30-37), Al-Waaqi’ah (56:41-44), pia Al-Waaqi’ah (56:51-56) na Suwrah nyenginezo.
[6] Shaytwaan Huwapotosha Watu Kisha Huwakanusha Na Kuwageuka!:
Rejea pia Al-Anfaal (8:48) ambako Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja jinsi shaytwaan anavyokanusha upotoshaji wake baada ya mambo kuwa magumu. Rejea pia Al-Israa (17:64).
Na hivi ndivyo ilivyo, kawaida ya shaytwaan, kuwa huwapotosha wanaadam duniani kisha pindi mambo yanapokuwa magumu au adhabu inapohakiki au inapofika Siku ya Qiyaamah huwakanusha na kuwageuka.
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anatahadharisha waja Wake na adui huyu katika Aayah kadhaa; miongoni mwazo ni: Al-Baqarah (2:208), (268), An-Nisaa (4:119-120), Al-An’aam (6:112), Al-Israa (17:53), (64), An-Nuwr (24:21), Al-Furqaan (25:29), Faatwir (35:5-6), Yaasiyn (36:60), Az-Zukhruf (43:36-39), (62), Al-Hashr (59:16-17).
[7] Mti Mzuri:
Mti uliokusudiwa katika Aayah hii na inayoifuatia ni mtende kama ilivyothibiti katika Hadiyth:
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Tulikuwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akauliza: “Niambieni kuhusu mti unaofanana na (au) ulio kama Muislamu, ambao majani yake hayaanguki wakati wa majira ya joto, wala wakati wa majira ya baridi, na hutoa matunda yake kila mara kwa idhini ya Rabb wake.” Ibn ‘Umar akasema: Niliufikiria kuwa ni mtende, lakini niliona vibaya kujibu nilipoona Abuu Bakr na ‘Umar hawakujibu. Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Ni mtende.” Tulipoondoka, nilimwambia ‘Umar: Ee baba yangu! Wa-Allaahi nilihisi kuwa ni mtende. Akasema: Kwa nini basi hukutaja? Nikasema: Nilikuoneni kimya, nikaona vibaya kusema kitu. Akasema ‘Umar: Ungelisema, ingelikuwa bora kwangu kuliko kadhaa na kadhaa. (Yaani ningelikuwa na fakhari zaidi kuwa wewe mwanangu ndiye uliyeweza kujibu pekee). [Al-Bukhaariy]
[8] Al-Qawl Ath-Thaabit: Kauli Thabiti Duniani Na Aakhirah:
Imekusudiwa Shahaada ya Uislamu katika Maswali matatu atakayoulizwa mtu kaburini:
Amesimulia Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muislamu akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba:
لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه
Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah.
Basi hiyo ndiyo maana ya Kauli ya Allaah:
يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ
“Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah.” [Ibraahiym (14:27) Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo]
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
014-Asbaabun-Nuzuwl: Ibraahiym Aayah 27: يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ
[9] Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى) Haiwezekani Kuzihesabu Zote:
Rejea pia An-Nahl (16:5), Luqmaan (31:20), Al-Muuminuwn (23:17).
Neema za kwanza kwa Muislamu ni:
(i) Uislamu kwa kuwa Allaah Katuvua kutoka ukafiri. Hii ni neema kubwa kwani wangapi bado juu ya kuusikia Uislamu, hawajaweza kuukubali Uislamu.
(ii) Kuwa na imaan: Kuamini nguzo sita za imaan, na kuziitakidi na kutenda matendo ya Muumini.
(iii) Kutumwa kwetu Nabiy na Rasuli wa mwisho kabisa, Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye, amekuja kuwa ni mwongozo kwetu kutuongoza vipi kuishi katika dunia, na vipi kutaamuli na wanaadam wenzetu. Allaah (سبحانه وتعالى) Hakutuacha tu bila ya kutuletea Rasuli wa kutubainishia yaliyo ya haki ili tuyafuate na tutekeleze, na kutubainishia yaliyo ya batili ili tujiepushe nayo na haya yote ni kwa ajili ya kubakia katika Al-‘Aafiyah (usalama wa kila aina katika Dini yetu na maisha ya duniani na ya Aakhirah).
(iv) Kuteremshiwa Kitabu cha mwisho; Qur-aan Adhimu ambacho ni mwongozo kwetu, tunapata mawaidha, tulizo za nyoyo, shifaa (poza) kutokana na maradhi ya moyo yaliyotajwa ndani ya Qur-aan kama kutukinga na shirki, ukafiri, unafiki na kadhaalika. Pia Qur-aan ni shifaa na tiba maradhi ya mwili. Na ndani ya Qur-aan, pia kuna kanuni za kuishi katika hii dunia ili tuishi kama wanaadam kinyume na vile wanavyoishi wananyama. Na kuweza kutimiza Uislamu wetu ili kubakia katika Ridhaa ya Allaah.
(v) Sunnah zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Mfano Sunnah za ibaada ambazo tunapata ujira kuzitekeleza kwake. Pia, Sunnah nyenginezo za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambazo, kwazo, zinatufunza jinsi ya kuishi na wanaadam wenzetu, na tunapata maslahi ndani yake na tunabakia katika usalama na amani katika jamii. Na juu ya hivyo, kutekeleza kwake ni kujichumia thawabu za kujenga Aakhirah yetu.
(vi) Kujaaliwa uwepo wa Swahaba wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambao tunapata mafunzo mengi mema kutokana na sifa zao.
(vii) Kuthibiti imara katika Dini na khasa katika Manhaj ya Salaf Swaalih (Wema waliotangulia).
Ama neema nyenginezo, ni kama Anavyosema Allaah (عزّ وجلّ) kwamba hawezi mtu kuziorodhesha hesabuni! Basi mwanaadam ajaribu kutafakari angalau aweze kufikia utambuzi wa neema chache mno miongoni mwa neema nyingi za Allaah (سبحانه وتعالى) ili aweze kumshukuru.
Neema zinazoonekana na ambazo hazionekani. Rejea Luqmaan (31:20). Basi na ajaribu mtu kuzitafakari katika mgawanyo ufuatao:
Umbile La Mwanaadam:
Kuanzia viungo vya mwanaadam vinavyoonekana kama mikono ya kufanyia kazi na ya kulia chakula. Miguu ya kuendea shughulini mwake na kwengineko. Viungo vya kichwa; macho ya kuonea, masikio ya kusikia, mdomo ambao humo mna meno ya kutafunia chakula na ulimi wa kuonjea chakula na kuongelea, pua ya kunusia harufu na kuvutia pumzi na kadhaalika.
Vile vile, viungo visivyoonekana kwa macho ya kawaida; viungo vilivyomo ndani ya mwili wa mwanaadam kama moyo, mishipa yote ya mwili, viungo vinavyotumika katika mfumo wa umeng'enyaji wa chakula. Ubongo wenye akili ambayo ni neema kubwa mno kuwa na akili timamu na kipaji. Almuradi ni neema adhimu jinsi Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyouumba mwili wa mwanaadam na jinsi kila viungo hivyo vinavyofanya kazi kuendesha uhai wa mwanaadam:
فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ ﴿١٤﴾
“Basi Amebarikika Allaah Mbora wa wenye kuumba.” Rejea Al-Muuminuwn (23:12-14), na pia Ghaafir (40:64), At-Tiyn (95:4).
Rejea pia Al-Israa (17:70) kwenye faida kuhusu jinsi binaadam alivyokirimiwa na kufadhilishwa.
Neema Zisizoonekana:
Imaan, taqwa ambazo zimo moyoni mwa mwanaadam, na mengineyo yote ya ghaibu ya duniani na ya Aakhirah. Rejea Al-Baqarah (2:3). Na katika neema za ghaibu za Aakhirah, ni neema za Jannah (Peponi), na neema kubwa kabisa huko ni kumwona Allaah (عزّ وجلّ). Rejea Yuwnus (10:26), na Al-Qiyaamah (75:22-23). Neema hizo na nyenginezo, zimetajwa katika Suwrah mbali mbali, na hapa si mahali pake kuzitaja zote, wala haiwezekani kuorodhesha zote!
Neema Za Ardhini, Baharini, Angani Na Katika Falaki:
Rejea Yaasiyn (36:38) kwenye maelezo bayana ya faida tele.
Na katika Qur-aan, neema za aina hizi zimetajwa katika Suwrah na Aayah mbalimbali. Mfano Suwrah An-Nahl ambayo inajulikana pia kama Suwrah Ya Neema, humo Allaah (عزّ وجلّ) Ametaja Neema tele za ardhini, baharini, angani na falakini! Rejea An-Nahl (16:4-16).
Pia, neema kama hizo na nyenginezo zimetajwa mwanzoni mwa Suwrah An-Nabaa (78:6-16). Pia Rejea Al-Furqaan (25:45-49), Suwrah ‘Abasa (80:18-32), na kwengineko; hapa si mahali pake kuzitaja zote, wala haiwezekani kuorodhesha zote!
Basi Hizo zote zilizotajwa hapo juu na katika rejea za Suwrah hizo, ni neema chache mno kati ya Neema nyingi za Allaah (عزّ وجلّ).
Na wanaadam wachache wenye kumshukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema kumhusu Nabiy Daawuwd (عليه السّلام):
اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾
“Tendeni enyi familia ya Daawuwd kwa shukurani! Na wachache miongoni mwa Waja Wangu ni wenye kushukuru.” [Sabaa (34:13)]
Na tujifunze shukurani ya Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام) kama alivyoomba:
رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ ﴿١٩﴾
Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru Neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Niingize kwa Rehma Yako katika Waja Wako Swalihina [An-Naml (27:19)]
Kadhaalika shukurani za mja mwema aliyeomba:
رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿١٥﴾
Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru Neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Nitengenezee dhuria wangu. Hakika mimi nimetubu Kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu. [Al-Ahqaaf (46:15)]
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida na mwongozo wa kumshukuru Allaah (عزّ وجلّ):
01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kutaja Jina La Allaah Mwanzoni na Kumaliza Kwa Kumshukuru
Vipi Kumshukuru Allaah Kwa Neema Zake Nyingi Zisizohesabika
Je, Unamshukuru Allaah ('Azza wa Jalla) Ipasavyo Kwa Neema Zake Nyingi Zisizohesabika?
Rejea pia Adhw-Dhwuhaa (93:11) kwenye faida kuhusu kukiri Neema za Allaah, kushukuru, na kuomba kuhifadhiwa na kuzidishiwa Neema za Allaah (عزّ وجلّ).
[10] Ujenzi Wa Ka’bah Na Duaa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) :
Kuanzia Aayah hii ya (14:35) hadi (14:41), panazungumziwa kuhusu kujengwa Al-Ka’bah na duaa za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) alizoomba. Rejea pia Al-Baqarah (2:127-129).
[11] Duaa Ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Kwa Wazazi Wake:
Duaa hiyo ya kuwaombea wazazi wake pia ni kabla ya kumbainikia kwamba wao ni adui wa Allaah. [Tafsiyr As-Sa’diy, Tafsiyr Al-Muyassar]
[12] Siku Ya Qiyaamah Watu Watafufuliwa Na Kukusanywa Katika Ardhi Tofauti Na Ya Dunia:
Amesimulia Sahl bin Sa’d (رضي الله عنه) : Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah katika ardhi nyeupe yenye wekundu kama vile mkate safi (uliotengenezwa kwa unga safi kabisa).” Sahl akaongeza kusema: Ardhi hiyo haitakuwa na alama kwa mtu yeyote (kuitumia). [Al-Bukhaariy na Muslim]