016 - An-Nahl
النَّحْل
016-An-Nahl
016-An-Nahl: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَتَىٰ أَمْرُ اللَّـهِ فَلَا تَسْتَعْجِلُوهُ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١﴾
1. Amri ya Allaah (ya Qiyaamah au adhabu) inakuja (karibu), basi msiihimize. Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa Uluwa kutokana na wanayomshirikisha nayo.
يُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ بِالرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ أَنْ أَنذِرُوا أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ﴿٢﴾
2. Anateremsha Malaika wakiwa na Ruwh[1] (Wahy) kwa Amri Yake juu ya Amtakaye miongoni mwa Waja Wake, wakiwaambia: Onyeni kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, basi Nicheni.
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ تَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣﴾
3. Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Ametukuka kwa Uluwa kutokana na yale wanayoshirikisha.
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ﴿٤﴾
4. Amemuumba binaadam kutokana na tone la manii, tahamaki yeye ni mbishani fasaha wa maneno.
وَالْأَنْعَامَ خَلَقَهَا ۗ لَكُمْ فِيهَا دِفْءٌ وَمَنَافِعُ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٥﴾
5. Na wanyama wa mifugo Amewaumba. Mnapata kwao (sufi, ngozi za kutia) ujotojoto na manufaa (mengineyo), na miongoni mwao mnawala.[2]
وَلَكُمْ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسْرَحُونَ﴿٦﴾
6. Na mnapata humo burudiko wakati mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka machungani asubuhi.
وَتَحْمِلُ أَثْقَالَكُمْ إِلَىٰ بَلَدٍ لَّمْ تَكُونُوا بَالِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ الْأَنفُسِ ۚ إِنَّ رَبَّكُم ْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿٧﴾
7. Na wanabeba mizigo yenu kupeleka nchi msizoweza kuzifikia isipokuwa kwa mashaka mazito ya kuwalemeeni. Hakika Rabb wenu bila shaka Ni Mwenye Huruma mno, Mwenye Kurehemu.
وَالْخَيْلَ وَالْبِغَالَ وَالْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً ۚ وَيَخْلُقُ مَا لَا تَعْلَمُونَ﴿٨﴾
8. Na farasi na baghala na punda ili muwapande na wawe mapambo. Na Anaumba msivyovijua.
وَعَلَى اللَّـهِ قَصْدُ السَّبِيلِ وَمِنْهَا جَائِرٌ ۚ وَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ﴿٩﴾
9. Na ni Jukumu la Allaah kubainisha njia (ya haki), na ziko miongoni mwazo za kupotoka. Na kama Angetaka Angekuhidini nyote.
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً ۖ لَّكُم مِّنْهُ شَرَابٌ وَمِنْهُ شَجَرٌ فِيهِ تُسِيمُونَ﴿١٠﴾
10. Yeye Ndiye Aliyeteremsha kutoka mbinguni maji.[3] Kwayo mnapata ya kunywa, na pia ya miti ambayo mnalishia.
يُنبِتُ لَكُم بِهِ الزَّرْعَ وَالزَّيْتُونَ وَالنَّخِيلَ وَالْأَعْنَابَ وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿١١﴾
11. (Kadhalika) Anakuotesheeni kwayo mimea, na mizaytuni na mitende na mizabibu, na kila (aina ya) mazao. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotafakari.
وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ وَالنُّجُومُ مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿١٢﴾
12. Na Amekutiishieni usiku na mchana, na jua na mwezi. Na nyota zimetiishwa kwa Amri Yake. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotia akilini.
وَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ﴿١٣﴾
13. Na (Ametiisha pia) Alivyoviumba katika ardhi vya rangi tofauti. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaokumbuka.
وَهُوَ الَّذِي سَخَّرَ الْبَحْرَ لِتَأْكُلُوا مِنْهُ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُوا مِنْهُ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى الْفُلْكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿١٤﴾
14. Naye Ndiye Ambaye Ametiisha bahari ili mle kutoka humo nyama laini safi, na mtoe humo mapambo mnayoyavaa, na utaona merikebu zikipasua maji humo, (Ameitiisha) ili mtafute katika Fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.
وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَارًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٥﴾
15. Na Ameweka katika ardhi milima iliyosimama imara ili isiyumbeyumbe nanyi, na (Akaweka) mito na njia ili mpate kujua mwendako.
وَعَلَامَاتٍ ۚ وَبِالنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ﴿١٦﴾
16. Na alama za kutambulisha, na kwa nyota wao wanaojiongoza (njia).[4]
أَفَمَن يَخْلُقُ كَمَن لَّا يَخْلُقُ ۗ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿١٧﴾
17. Je, (Allaah) Anayeumba ni sawa na asiyeumba? Je, basi hamkumbuki?
وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٨﴾
18. Na kama mkihesabu Neema za Allaah basi hamtoweza kuziorodhesha hesabuni.[5] Hakika Allaah bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ﴿١٩﴾
19. Na Allaah Anajua mnayoyafanya siri na mnayoyadhihirisha.
وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ﴿٢٠﴾
20. Na wale wanaowaomba badala ya Allaah hawaumbi kitu chochote, bali wao wanaumbwa.
أَمْوَاتٌ غَيْرُ أَحْيَاءٍ ۖ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ﴿٢١﴾
21. Ni wafu si wahai, na hawatambui lini watafufuliwa.
إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ فَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٌ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ﴿٢٢﴾
22. Mwabudiwa wenu wa haki ni Ilaah (Allaah) Mmoja. Basi wale wasioamini Aakhirah nyoyo zao zinakanusha nao wanatakabari.
لَا جَرَمَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْتَكْبِرِينَ﴿٢٣﴾
23. Hapana shaka kwamba Allaah Anajua wanayoyafanya kwa siri na wanayoyadhihirisha. Hakika Yeye Hapendi wanaotakabari.
وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۙ قَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿٢٤﴾
24. Na pale wanapoambiwa: Nini Ameteremsha Rabb wenu (kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)? Husema: Hekaya za watu wa kale.
لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ﴿٢٥﴾
25. Ili wabebe mizigo (ya madhambi) yao kwa ukamilifu Siku ya Qiyaamah, pamoja na mizigo ya wale waliowapoteza bila ya kujua. Tanabahi! Uovu ulioje wanayoyabeba!
قَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى اللَّـهُ بُنْيَانَهُم مِّنَ الْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ السَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٢٦﴾
26. Walikwishafanya makri wale wa kabla yao, na Allaah Akayasukua majengo yao kwenye misingi, sakafu zikawaporomokea juu yao, na ikawajia adhabu kutoka pande wasizozitambua.
ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تُشَاقُّونَ فِيهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِنَّ الْخِزْيَ الْيَوْمَ وَالسُّوءَ عَلَى الْكَافِرِينَ﴿٢٧﴾
27. Kisha Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atawahizi na Atasema: Wako wapi washirika Wangu ambao mlikuwa kwa ajili yao mnapingana kuwahasimu (Rusuli na Waumini)? Watasema waliopewa ilimu: Hakika hizaya leo na uovu ni juu ya makafiri.
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا السَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوءٍ ۚ بَلَىٰ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾
28. Ambao Malaika huwafisha wakiwa wamejidhulumu nafsi zao, watasalimu amri (watasema): Hatukuwa tukitenda uovu wowote. (Wataambiwa): Hapana! Hakika Allaah Anayajua vyema mliyokuwa mkitenda.
فَادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٢٩﴾
29. Basi ingieni milango ya Jahannam mdumu humo. Ni uovu ulioje makazi ya wanaotakabari!
وَقِيلَ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا مَاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا خَيْرًا ۗ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ ۚ وَلَنِعْمَ دَارُ الْمُتَّقِينَ﴿٣٠﴾
30. Na wanapoambiwa wale waliokuwa na taqwa: Nini Ameteremsha Rabb wenu? Husema: Kheri. Kwa wale waliofanya ihsaan katika dunia hii watapata hasanah (mazuri). Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi. Na uzuri ulioje nyumba ya wenye taqwa!
جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْزِي اللَّـهُ الْمُتَّقِينَ﴿٣١﴾
31. Jannaat (bustani) za kudumu milele wataziingia inapita chini yake mito. Watapata humo wayatakayo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowalipa wenye taqwa.
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾
32. Wale ambao Malaika wanawafisha katika hali njema watawaambia: Salaamun ‘Alaykum (amani iwe juu yenu), ingieni Jannah kwa sababu ya yale mliyokuwa mkitenda.
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ أَمْرُ رَبِّكَ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٣٣﴾
33. Je, wanangojea lolote isipokuwa wawafikie Malaika (kuwatoa roho) au ije Amri ya Rabb wako (ya adhabu). Hivyo ndivyo walivyofanya wale wa kabla yao. Na Allaah Hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.
فَأَصَابَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٣٤﴾
34. Basi yakawasibu maovu ya waliyoyatenda, na yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
وَقَالَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا عَبَدْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ نَّحْنُ وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ فَهَلْ عَلَى الرُّسُلِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿٣٥﴾
35. Na wale washirikina walisema: Kama Angelitaka Allaah tusingeliabudu chochote badala Yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeliharamisha chochote bila Yeye Kuturuhusu. Hivyo ndivyo walivyofanya wale wa kabla yao. Basi je, kuna lolote juu ya Rusuli isipokuwa kufikisha Ujumbe kwa ubainifu?
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللَّـهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ ۚ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٣٦﴾
36. Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaghuti.[6] Basi miongoni mwao wako ambao Allaah Amewahidi, na miongoni mwao wako ambao umewathibitikia upotofu. Basi nendeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.[7]
إِن تَحْرِصْ عَلَىٰ هُدَاهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَن يُضِلُّ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٣٧﴾
37. Ukiwa na hima ya kwamba wahidike (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Allaah Hamhidi Aliyemtakia kupotea. Na hawatopata wenye kuwanusuru.
وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ لَا يَبْعَثُ اللَّـهُ مَن يَمُوتُ ۚ بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٨﴾
38. Na wakaapa kwa Allaah, viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba: Allaah Hatomfufua aliyekufa. Sivyo hivyo! Bali Ahadi Yake ni haki (Atafufua wote), lakini watu wengi hawajui.
لِيُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ كَانُوا كَاذِبِينَ﴿٣٩﴾
39. Ili Awabainishie yale wanayokhitilafiana, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo.
إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَيْءٍ إِذَا أَرَدْنَاهُ أَن نَّقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴿٤٠﴾
40. Hakika Kauli Yetu kwa kitu Tunapokikusudia, Tunakiambia: Kun! (Kuwa) Basi kinakuwa!
وَالَّذِينَ هَاجَرُوا فِي اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٤١﴾
41. Na wale waliohajiri kwa ajili ya Allaah baada ya kudhulumiwa, kwa hakika Tutawapa makazi mazuri duniani. Na bila shaka ujira wa Aakhirah ni mkubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua.
الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٤٢﴾
42. (Hao ndio) Wale waliovuta subira na wakatawakali kwa Rabb wao.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۚ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٤٣﴾
43. Na Hatukutuma (Rasuli) kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni wanaume Tunawafunulia Wahy. Basi ulizeni watu wenye ukumbusho[8] ikiwa nyinyi hamjui.
بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾
44. (Tumewatuma) Kwa hoja bayana na Vitabu vya Hukumu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari.
أَفَأَمِنَ الَّذِينَ مَكَرُوا السَّيِّئَاتِ أَن يَخْسِفَ اللَّـهُ بِهِمُ الْأَرْضَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٤٥﴾
45. Je, wameaminisha wale waliopanga makri za uovu kwamba Allaah Hatowadidimiza katika ardhi au haitowafikia adhabu kutoka wasipotambua?
أَوْ يَأْخُذَهُمْ فِي تَقَلُّبِهِمْ فَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ﴿٤٦﴾
46. Au (Allaah) Hatowakamata wakiwa katika harakati zao na wao wasiweze kukwepa?
أَوْ يَأْخُذَهُمْ عَلَىٰ تَخَوُّفٍ فَإِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿٤٧﴾
47. Au (Allaah) Hatowakamata katika hali ya khofu ya kusubiri adhabu? Hakika Rabb wako bila shaka Ni Mwenye Huruma mno, Mwenye Kurehemu.
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ﴿٤٨﴾
48. Je, hawaoni vile vitu Alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinasogea huku na kule, kuliani na kushotoni, vikimsujudia Allaah[9], na huku wao (wenye vivuli) wananyenyekea?
وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ﴿٤٩﴾
49. Na ni Allaah Pekee vinamsujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo, na Malaika, nao hawatakabari.
يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩﴿٥٠﴾
50. Wanamkhofu Rabb wao Aliye juu yao[10], na wanafanya yale wanayoamrishwa.
وَقَالَ اللَّـهُ لَا تَتَّخِذُوا إِلَـٰهَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ﴿٥١﴾
51. Na Allaah Anasema: Msijichukulie waabudiwa wawili, hakika Yeye Ndiye Mwabudiwa wa haki Mmoja Pekee, basi niogopeni Mimi tu.
وَلَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَهُ الدِّينُ وَاصِبًا ۚ أَفَغَيْرَ اللَّـهِ تَتَّقُونَ﴿٥٢﴾
52. Na ni Vyake vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi, na ni Yeye Pekee Astahikiye kuabudiwa na kutiiwa daima. Je, basi mtamcha asiyekuwa Allaah?
وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ ۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فَإِلَيْهِ تَجْأَرُونَ﴿٥٣﴾
53. Na Neema yoyote mliyo nayo, basi ni kutoka kwa Allaah. Kisha inapokuguseni dhara, mnamlilia Yeye tu kuomba msaada.
ثُمَّ إِذَا كَشَفَ الضُّرَّ عَنكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنكُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ﴿٥٤﴾
54. Kisha Anapokuondosheeni dhara tahamaki kundi miongoni mwenu wanamshirikisha Rabb wao.
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ﴿٥٥﴾
55. Ili waje wakanushe (Neema) Tulizowapa. Basi stareheni kidogo, mtakuja kujua.
وَيَجْعَلُونَ لِمَا لَا يَعْلَمُونَ نَصِيبًا مِّمَّا رَزَقْنَاهُمْ ۗ تَاللَّـهِ لَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَفْتَرُونَ﴿٥٦﴾
56. Na wanawawekea (waabudiwa wao) wasiojua (wanayofanyiwa), fungu katika ambavyo Tumewaruzuku. Ta-Allaahi![11] Bila shaka mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatunga (ya uongo).
وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ الْبَنَاتِ سُبْحَانَهُ ۙ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ﴿٥٧﴾
57. Na wanamfanyia Allaah kuwa ana mabinti! Utakasifu ni Wake! Na wao wawe na (wana wa kiume) wanaowatamani.[12]
وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِالْأُنثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ﴿٥٨﴾
58. Na anapoletewa khabari mmoja wao ya kuzaliwa mtoto wa kike, uso wake husawijika na kujawa majonzi na ghamu.
يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِن سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ﴿٥٩﴾
59. Anajificha asikutane na watu kutokana na khabari mbaya aliyoletewa. Je, abaki naye kwa fedheha au amfukie ardhini (mzimamzima)? Tanabahi! Uovu ulioje wanayohukumu!
لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ مَثَلُ السَّوْءِ ۖ وَلِلَّـهِ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٦٠﴾
60. Wale wasioamini Aakhirah wana mfano mbaya (wa upungufu), lakini Allaah Ana Sifa Kamilifu Tukufu Kabisa. Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٦١﴾
61. Na kama Allaah Angeliwachukulia watu kwa dhulma zao, Asingeliacha juu ya ardhi kiumbe chochote, lakini Anawaakhirisha mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Basi utakapofika muda wao hawatoakhirisha saa na wala hawatotanguliza.
وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ مَا يَكْرَهُونَ وَتَصِفُ أَلْسِنَتُهُمُ الْكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ الْحُسْنَىٰ ۖ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ النَّارَ وَأَنَّهُم مُّفْرَطُونَ﴿٦٢﴾
62. Na wanamfanyia Allaah yale wanayoyachukia (wao wenyewe), na ndimi zao zinaeleza uongo kwamba watapata mazuri kabisa. Hapana shaka kwamba watapata moto na watatelekezwa humo.
تَاللَّـهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ الْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٦٣﴾
63. Ta-Allaahi![13] Kwa yakini Tulipeleka (Rusuli) kwa nyumati za kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), shaytwaan akawapambia vitendo vyao. Na yeye leo ni rafiki yao mlinzi, nao watapata adhabu iumizayo.
وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٦٤﴾
64. Na Hatukukuteremshia Kitabu (Qur-aan) isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana, na pia ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini.
وَاللَّـهُ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٦٥﴾
65. Na Allaah Ameteremsha kutoka mbinguni maji Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaosikia.
وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِ مِن بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَائِغًا لِّلشَّارِبِينَ﴿٦٦﴾
66. Na hakika kuna mazingatio kwenu katika wanyama wa mifugo. Tunakunywesheni katika yale yaliyomo matumboni mwao yaliyo baina ya kinyesi na damu; (nayo ni) maziwa safi ya ladha ya kuburudisha kwa wanywaji.
وَمِن ثَمَرَاتِ النَّخِيلِ وَالْأَعْنَابِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿٦٧﴾
67. Na katika matunda ya mitende na mizabibu mnafanya kutokana nayo vinywaji vikali vya ulevi (kabla ya kuharamishwa)[14] na riziki nzuri. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wanaotia akilini.
وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ﴿٦٨﴾
68. Na Rabb wako Amemtia ilhamu nyuki kwamba: Jitengenezee nyumba katika majabali, na katika miti, na katika wanavyojenga.
ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٦٩﴾
69. Kisha kula katika kila matunda, na fuata njia za Rabb wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita). Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbali mbali, ndani yake mna shifaa (ya magonjwa) kwa watu. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotafakari.
وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّاكُمْ ۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ قَدِيرٌ﴿٧٠﴾
70. Na Allaah Amekuumbeni, kisha Anakufisheni. Na yuko miongoni mwenu anayerudishwa katika umri mbaya na dhaifu zaidi awe hajui tena kitu chochote baada ya (kuwa na) ilimu. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa yote, Muweza wa yote.
وَاللَّـهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الرِّزْقِ ۚ فَمَا الَّذِينَ فُضِّلُوا بِرَادِّي رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَاءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ﴿٧١﴾
71. Na Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengineo katika riziki. Basi wale waliofadhilishwa hawagawi riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika hiyo (riziki). Je, basi wanakanusha Neema za Allaah?
وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ اللَّـهِ هُمْ يَكْفُرُونَ﴿٧٢﴾
72. Na Allaah Amekufanyieni wake katika jinsi yenu, na Amekufanyieni kutokana na wake zenu wana na wajukuu, na Amekuruzukuni vizuri. Je, basi wanaamini ya batili na wanakufuru Neema za Allaah?
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَهُمْ رِزْقًا مِّنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ شَيْئًا وَلَا يَسْتَطِيعُونَ﴿٧٣﴾
73. Na wanaabudu pasi na Allaah wasiowamilikia (uwezo wa) riziki ya kitu chochote kutoka mbinguni na ardhini, na (hakika) wala hawawezi.
فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٧٤﴾
74. Basi msimpigie mifano Allaah. Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.
ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَمَن رَّزَقْنَاهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ هَلْ يَسْتَوُونَ ۚ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٧٥﴾
75. Allaah Amepiga mfano wa mtumwa anayemilikiwa hana uwezo juu ya chochote, na mtu (huru) ambaye Tumemruzuku kutoka Kwetu riziki nzuri, naye akawa anaitoa kwa siri na dhahiri. Je, wanalingana sawa? AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah)! Bali wengi wao hawajui.[15]
وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٧٦﴾
76. Na Allaah Amepiga mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote, naye ni mzigo mzito kwa anayemsimamia mambo yake, na popote anapomuelekeza haleti kheri. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka?
وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلَّا كَلَمْحِ الْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٧٧﴾
77. Na ni ya Allaah ghaibu ya mbingu na ardhi. Na haikuwa amri ya Saa (Qiyaamah) isipokuwa kama upepeso wa jicho au karibu zaidi.[16] Hakika Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
وَاللَّـهُ أَخْرَجَكُم مِّن بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئًا وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۙ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿٧٨﴾
78. Na Allaah Amekutoeni kutoka matumboni mwa mama zenu mkiwa hamjui lolote, na Amekujaalieni kusikia na kuona na nyoyo ili mpate kushukuru.
أَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ مُسَخَّرَاتٍ فِي جَوِّ السَّمَاءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا اللَّـهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٧٩﴾
79. Je, hawaoni ndege wanavyotiishwa katika anga la mbingu, hakuna anayewashika isipokuwa Allaah. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaoamini.
وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّن بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ الْأَنْعَامِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَا أَثَاثًا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ﴿٨٠﴾
80. Na Allaah Amekufanyieni majumba yenu yawe maskani. Na Amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama wa mifugo mahema ambayo mnayahisi mepesi siku ya kusafiri kwenu na siku ya kupiga kwenu kambi, na kutokana na sufi zao na manyoya yao, na nywele zao (Amekujaalieni) fanicha na vifaa vya kutumia mpaka muda fulani.
وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَالًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْجِبَالِ أَكْنَانًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَابِيلَ تَقِيكُمُ الْحَرَّ وَسَرَابِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ﴿٨١﴾
81. Na Allaah Amekufanyieni vivuli katika Alivyoumba, na Akakujaalieni katika majabali mapango, na Amekujaalieni mavazi yanakukingeni na joto na mavazi (ya chuma) yanakukingeni katika vita vyenu. Hivyo ndivyo Anavyotimiza Neema Yake juu yenu ili mpate kujisalimisha.
فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿٨٢﴾
82. Wakikengeuka, basi hakika ni juu yako ubalighisho wa bayana.
يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ اللَّـهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ الْكَافِرُونَ﴿٨٣﴾
83. Wanazijua Neema za Allaah, kisha wanazikanusha, na wengi wao ni makafiri.
وَيَوْمَ نَبْعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا ثُمَّ لَا يُؤْذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ﴿٨٤﴾
84. Na Siku Tutakapohudhurisha shahidi kwa kila ummah, kisha waliokufuru hawatoruhusiwa (kutoa nyudhuru) na wala hawatapewa nafasi ya kujitetea (kwa Allaah).
وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ ظَلَمُوا الْعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ﴿٨٥﴾
85. Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, basi hawatopunguziwa wala hawatopewa muhula.
وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ أَشْرَكُوا شُرَكَاءَهُمْ قَالُوا رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ شُرَكَاؤُنَا الَّذِينَ كُنَّا نَدْعُو مِن دُونِكَ ۖ فَأَلْقَوْا إِلَيْهِمُ الْقَوْلَ إِنَّكُمْ لَكَاذِبُونَ﴿٨٦﴾
86. Na wale waliomshirikisha (Allaah) watakapowaona washirika wao watasema: Rabb wetu! Hawa ni washirikishwa wetu ambao tulikuwa tunawaomba badala Yako. Hapo hapo watatamka kuwarudi: Hakika nyinyi ni waongo!
وَأَلْقَوْا إِلَى اللَّـهِ يَوْمَئِذٍ السَّلَمَ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٨٧﴾
87. Na watajisalimisha kwa Allaah Siku hiyo. Na yatawapotea waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).
الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ زِدْنَاهُمْ عَذَابًا فَوْقَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يُفْسِدُونَ﴿٨٨﴾
88. Wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, Tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa sababu ya ufisadi waliokuwa wakiufanya.
وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿٨٩﴾
89. Na Siku Tutakapohudhurisha shahidi kwa kila ummah anayetokana na wao wenyewe awatolee ushuhuda. Na Tutakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uwe shahidi juu ya hawa (ummah wako).[17] Na Tumekuteremshia Kitabu kikiwa ni kielezo bayana cha kila kitu, na ni mwongozo, na rehma, na bishara kwa Waislamu.
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ﴿٩٠﴾
90. Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu, na ihsaan, na kuwapa (msaada) jamaa wa karibu, na Anakataza machafu, na munkari, na baghi[18] (udhalimu). Anakuwaidhini ili huenda mkapata kukumbuka.
وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا الْأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللَّـهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ﴿٩١﴾
91. Na timizeni Ahadi ya Allaah mnapoahidi, na wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, na hali ya kuwa mmekwishamfanya Allaah Kuwa Mdhamini wenu. Hakika Allaah Anajua yale mnayoyafanya.
وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ اللَّـهُ بِهِ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ﴿٩٢﴾
92. Na wala msiwe kama yule mwanamke aliyezongoa uzi wake vipande vipande baada ya (kuusokota na) kuwa mgumu, mnafanya viapo vyenu kuwa njia ya kudaganyana baina yenu[19], kwa kuwa ati ummah mmoja una nguvu zaidi kwa idadi na utajiri kuliko ummah mwengine. Hakika hapana ila Allaah Anakujaribuni kwavyo. Na bila shaka Atakubainishieni Siku ya Qiyaamah yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.
وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَلَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٩٣﴾
93. Na kama Allaah Angelitaka Angelikufanyeni ummah mmoja, lakini Humpotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye. Na bila shaka mtaulizwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
وَلَا تَتَّخِذُوا أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ فَتَزِلَّ قَدَمٌ بَعْدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُوا السُّوءَ بِمَا صَدَدتُّمْ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَلَكُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٩٤﴾
94. Na wala msifanye viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu ukateleza mguu baada ya kuthibitika kwake na mkaonja uovu wenu (duniani) kwa sababu ya kuzuia kwenu Njia ya Allaah. Na mtapata (Aakhirah) adhabu kuu.[20]
وَلَا تَشْتَرُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ إِنَّمَا عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٩٥﴾
95. Na wala msibadilishe Ahadi ya Allaah kwa thamani ndogo. Hakika yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kwenu, mngelikuwa mnajua.
مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ اللَّـهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٦﴾
96. Mlivyo navyo nyinyi vinatoweka, na vilivyoko kwa Allaah ni vya kubakia. Na kwa yakini Tutawalipa wale waliovuta subira ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.
مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾
97. Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, hakika Tutamhuisha uhai mzuri,[21] na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.
فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴿٩٨﴾
98. Unaposoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.[22]
إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٩٩﴾
99. Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na kwa Rabb wao wanatawakali.
إِنَّمَا سُلْطَانُهُ عَلَى الَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُ وَالَّذِينَ هُم بِهِ مُشْرِكُونَ﴿١٠٠﴾
100. Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya rafiki mwandani na ambao wao wanamshirikisha (Allaah) naye.
وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٠١﴾
101. Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine,[23] na Allaah Anajua zaidi Anayoyateremsha, husema: Hakika wewe ni mtungaji (uongo). Bali wengi wao hawajui.
قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿١٠٢﴾
102. Sema: Ameiteremsha Ruwh[24] Al-Qudus (Jibriyl) kutoka kwa Rabb wako kwa haki ili iwathibitishe wale walioamini, na ni mwongozo na bishara kwa Waislamu.
وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ﴿١٠٣﴾
103. Na kwa yakini Tunajua kwamba wao wanasema: Hakika hapana isipokuwa mtu anamfundisha (Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم Qur-aan). Lugha wanayomnasibishia nayo ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu bayana.[25]
إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ لَا يَهْدِيهِمُ اللَّـهُ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١٠٤﴾
104. Hakika wale wasioamini Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) za Allaah, Allaah Hatowahidi, na watapata adhabu iumizayo.
إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ﴿١٠٥﴾
105. Hakika wanaotunga uongo ni wale ambao hawaamini Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) za Allaah. Na hao ndio waongo.
مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿١٠٦﴾
106. Atakayemkufuru Allaah baada ya imaan yake - isipokuwa yule aliyekirihishwa (kukanusha) na huku moyo wake umetua juu ya imaan - lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao juu yao ni ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kuu kabisa.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿١٠٧﴾
107. Hivyo ni kwa sababu wao wamestahabu uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah, na kwa kuwa Allaah Haongoi watu makafiri.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٠٨﴾
108. Hao ni wale ambao Allaah Amepiga chapa juu ya nyoyo zao, na masikio yao, na macho yao. Na hao ndio walioghafilika.
لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿١٠٩﴾
109. Hakuna shaka kwamba wao Aakhirah ni wenye kukhasirika.
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِن بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٠﴾
110. Kisha hakika Rabb wako, kwa wale waliohajiri baada ya kutiwa matesoni, kisha wakafanya Jihaad na wakavuta subira, hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[26]
يَوْمَ تَأْتِي كُلُّ نَفْسٍ تُجَادِلُ عَن نَّفْسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿١١١﴾
111. Siku itakapokuja kila nafsi huku ikijitetea yenyewe, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyofanya, nao hawatodhulumiwa.
وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ آمِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ اللَّـهِ فَأَذَاقَهَا اللَّـهُ لِبَاسَ الْجُوعِ وَالْخَوْفِ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ﴿١١٢﴾
112. Na Allaah Amepiga mfano wa mji (wa Makkah) uliokuwa katika amani na utulivu, inaufikia riziki yake maridhawa kutoka kila mahali, kisha ukakufuru Neema za Allaah. Basi Allaah Akauonjesha funiko la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakitenda.
وَلَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْهُمْ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ وَهُمْ ظَالِمُونَ﴿١١٣﴾
113. Na kwa yakini aliwajia Rasuli miongoni mwao wakamkadhibisha, basi ikawachukuwa adhabu hali ya kuwa ni madhalimu.
فَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا وَاشْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ﴿١١٤﴾
114. Basi kuleni katika vile Alivyokuruzukuni Allaah vya halali vizuri, na shukuruni Neema za Allaah ikiwa mnamwabudu Yeye Pekee.
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٥﴾
115. Hakika (Allaah) Amekuharamishieni nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake ghairi ya Allaah. Lakini atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ﴿١١٦﴾
116. Na wala msiseme kwa ndimi zenu zinazopambia uongo: Hii halali na hii haramu ili mumtungie uongo Allaah. Hakika wale wanaomtungia uongo Allaah hawafaulu.
مَتَاعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١٧﴾
117. Ni starehe ndogo (tu duniani), na watapata adhabu iumizayo.
وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا مَا قَصَصْنَا عَلَيْكَ مِن قَبْلُ ۖ وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿١١٨﴾
118. Na wale Mayahudi Tuliwaharamishia yale Tuliyokusimulia kabla (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Hatukuwadhulumu, lakini walikuwa wanajidhulumu nafsi zao wenyewe.
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٩﴾
119. Kisha hakika Rabb wako, kwa wale waliotenda uovu kwa ujahili, kisha wakatubu baada yake, na wakatengeneza walivyoharibu, hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٠﴾
120. Hakika Ibraahiym alikuwa mwenye akhlaaq na maadili yote mema[27], mtiifu kwa Allaah, aliyeelemea haki, na hakuwa miongoni mwa washirikina.[28]
شَاكِرًا لِّأَنْعُمِهِ ۚ اجْتَبَاهُ وَهَدَاهُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿١٢١﴾
121. Mwenye kushukuru Neema Zake, (Naye Allaah) Akamteua na Akamuongoza kuelekea njia iliyonyooka.
وَآتَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ﴿١٢٢﴾
122. Na Tukampa duniani mazuri. Na hakika yeye Aakhirah bila shaka ni miongoni mwa Swalihina.
ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٣﴾
123. Kisha Tukakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba fuata mila ya Ibraahim aliyeelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.
إِنَّمَا جُعِلَ السَّبْتُ عَلَى الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٢٤﴾
124. Hakika As-Sabt[29] imefanywa kwa wale waliokhitilafiana kwayo. Na hakika Rabb wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wanakhitilafiana kwayo.
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ﴿١٢٥﴾
125. Lingania waje katika Njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. Na jadiliana nao kwa njia bora yenye kunasibiana na hali. Hakika Rabb wako, Yeye Anamjua zaidi aliyepotea Njia Yake, Naye Anawajua zaidi waliohidika.
وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ﴿١٢٦﴾
126. Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa. Na mkivuta subira, basi bila shaka hivyo ni bora zaidi kwa wenye subira.[30]
وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُ فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ﴿١٢٧﴾
127. Na vuta subira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na haiwi subira yako isipokuwa kwa Msaada na Tawfiyq ya Allaah. Na wala usiwahuzunikie, na wala usiwe katika dhiki kutokana na njama wanazozifanya.
إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ﴿١٢٨﴾
128. Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni wenye kufanya ihsaan.
[1] Maana Za Ruwh Katika Qur-aan:
Ruwh katika Qur-aan ina maana kadhaa ambazo zimo katika Suwrah na Aayah mbalimbali miongoni mwazo ni:
(i) Wahy: Yaani Qur-aan kama ilivyo katika Suwrah hii ya An-Nahl (16:2), na pia Ash-Shuwraa (42:52).
(ii) Jibriyl (عليه السّلام): Ni kama katika Suwrah hii ya An-Nahl (16:102) na pia Ash-Shu’araa (26:193), Maryam (19:17), Al-Baqarah (2:87) (2:253) na Al-Qadr (97:4).
(iii) Roho ya mwanaadam: Ni katika Suwrat Al-Israa (17:85).
[2] Miongoni Mwa Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى):
Kuanzia Aayah hii (16:5) hadi (16), Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja baadhi ya Neema Zake. Hali kadhaalika katika Suwrah hii Neema nyenginezo za Allaah (سبحانه وتعالى) zimetajwa katika Aayah, (65-69), (72), (80-81). Na Suwrah hii inajulikana pia kama ni Suwrah ya Neema. Rejea pia Al-Muuminuwn (23:17). Rejea pia Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah.
[3] Neema Ya Maji Na Hewa:
Miongoni mwa neema kubwa humo ni vitu viwili ambavyo mwanaadam hawezi kuishi bila ya uwepo wake. Allaah (عزّ وجلّ) Amevijaalia vitu hivi viwili vipatikane bure, kwa maana hata masikini aweze kuvipata! Navyo ni hewa tunayovutia pumzi, na maji Anayoyateremsha Allaah (سبحانه وتعالى) kutoka mbinguni kama mvua kwa ajili ya kunywa na kuotesha mimea na matumizi mengineyo yaliyo muhimu kwa binaadam. Na pia maji yanayopatikana katika tumbo la ardhi, baharini, kwenye maziwa na katika mito.
[4] Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Mambo Matatu:
Rejea Al-An’aam (6:97), Asw-Swaaffaat (37:10), Al-Mulk (67:5).
[5] Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى) Haiwezekani Kuzihesabu Zote:
Aayah kama hii imekariri katika Suwrah Ibraahiym (14:34). Rejea humo ambako kuna uchambuzi wa Neema za Allaah.
[6] Twaghuti: Rejea Al-Baqarah (2:256), An-Nisaa (4:51).
[7] Zingatio Na Tahadharisho Kwa Makafiri Watembee Maeneo Mbalimbali Ya Ardhi:
Zingatio na tahadharisho hili ili wapate kujionea wenyewe, na wapate kutambua hatima mbaya za waliokadhibisha kabla yao. Rejea Aal-‘Imraan (3:137).
[8] Ahl Adh-Dhikr "أَهْلُ الذِّكْرِ" (Watu wa Ukumbusho):
Ni watu waliopewa Vitabu Nyuma. Ni watu wenye ilimu ambao wameteremshiwa Vitabu na hoja bayana [Tafsiyr As-Sa’diy] (kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah inayofuatia).
[9] Kila Kitu Kinamsujudia Allaah (عزّ وجلّ):
Aayah hii namba (48) na inayofuatia (49) inataja viumbe na vitu kumsujudia Allaah. Rejea pia Ar-Rahmaan (55:6) kwenye rejea nyenginezo zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsujudia Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[10] Uthibitisho Kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko Juu Ya Viumbe Vyake Vyote:
Hao Malaika wanamuogopa Rabb wao Ambaye Yuko juu yao kwa Dhati Yake, utendeshaji nguvu Wake na ukamilifu wa Sifa Zake na wanafanya anayoamrishwa ya kumtii Allaah (سبحانه وتعالى). Katika Aayah hii, pana kuthibitisha sifa ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu ya viumbe Vyake vyote, kama inavyonasibiana na Utukufu Wake na ukamilifu Wake. [Tafsiyr Al-Muyassar] Rejea pia Al-A’raaf (7:54) na Al-Mulk (67:16).
[11] (تَاللَّهِ) Ta-Allaahi, (وَاللَّهِ) Wa-Allaahi, (بِاللَّهِ) Bi-Llaahi, Ni Kuapa Kwa Jina La Allaah:
Ni Neno la kuapia kwa Jina la Allaah. Herufi tatu zinatumika kuapia kwa namna hii ambazo ni “Waaw” (الواو), “Baa” (الباء) na “Taa” (التاء). Wa-Allaahi, Bi-Llaahi, na Ta-Allaahi,. Na yote ina maana moja ya (Naapa kwa Allaah). Ta-Allaahi imekariri mara kadhaa katika Suwrah Yuwsuf (12:73), (12:5), (12:91), (12:95).
[12] Washirikina Waliwachukia Watoto Wa Kike Lakini Wakimsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Ana Mabinti!
Katika Aayah hii ya An-Nahl (57 hadi 59), washirikina wamemsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana watoto wa kike ilhali wao wenyewe waliwachukia wakawa wanawazika wazima wazima pindi wanapozaliwa. Rejea: At-Takwiyr (81:8-9), Asw-Swaaffaat (37:149-153), Al-Israa (17:40) na Az-Zukhruf (43:15-19).
[13] Ta-Allaahi: Neno La Kuapia Kwa Jina La Allaah. Rejea Aayah (16:56).
[14] Ulevi, Pombe Vimeharamishwa: Rejea Al-Maaidah (5:90).
Aayah hiyo tukufu inamaanisha kuwa juisi ya matunda ya mitende na mizabibu ina vitu viwili: Moja ni kile ambacho ni chakula safi na chenye afya kwa mwanaadam. Na kingine ni kile kinachogeuka kuwa ulevi baada ya kuchachuka. Lakini katika Aayah hiyo, ulevi, pombe ilikuwa kabla ya kuharamishwa kwake. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaharamsiha ulevi, pombe na Akabadilisha kwa twayyibaat (vilivyo halali vizuri) kama nabiydh ambayo ni ulowekaji wa zabibu, tende, asali, ngano na shayiri na kunywa kinywaji chake kabla ya kuchachuka. Na kuchachuka kikawaida kunatokea baada ya siku tatu kama ilivyothibiti katika Hadiyth:
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akilowekewa zabibu akawa anakunywa maji yake siku hiyo na kesho yake na siku inayofuatia hadi jioni ya siku ya tatu. Kisha aliamuru inywewe (kabla ya kumalizika siku) au imwagwe. [Muslim]
Inapochachuka haifai kuinywa kwa sababu hugeuka ulevi au pombe na hapo inakuwa haramu.
Amesimulia ‘Aaishah: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kila kinywaji kinacholevya ni haramu.” [Al-Bukhaariy]
[16] Hoja Na Dalili Ya Wazi Kuwa Kusimamisha Saa (Qiyaamah) Ni Jambo Jepesi Mno Kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Na Kwamba Watu Watafufuliwa:
Rejea Al-An’aam (6:158), Ash-Shuwraa (42:17-18), Al-Israa (17:49), Ghaafir (40:59).
[17] Kila Ummah Utahuduhurishwa Na Shahidi Wake:
Rejea Al-Baqarah (2:143), An-Nisaa (4:41), Al-Israa (17:71), Al-Hajj (22:78), Az-Zumar (39:69), Al-Jaathiyah (45:28).
[18] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:
Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.
[19] Kutimiza Ahadi Na Mfano Wa Anayetimiza Ahadi Kisha Akabatilisha Ni Kama Aliyesokota Uzi Kisha Akauzongoa.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anapiga mfano wa mwanamke aliyekuwa Makkah ambaye alikuwa kila alipousokota uzi wake kwa juhudi, alirudi kuufumua na kuuzongoa ukarudi kama ulivyokuwa. Mfano huu ni kama Muumini anayefunga ahadi na viapo kisha akavivunja bila kujali. Na Aayah hii inahusiana na Aayah mbili zilizotangulia (90-91). Inamaanisha kuwa mtu asije kuvunja ahadi inayofungamana kati yake na Rabb wake, amtii na atekeleze yote Anayoamrisha, na afanye wema na ihsaan baina yake na watu. Kadhalika, ajiepushe na maharamisho yote, ajiepushe na shirki, ajitahidi awezavyo kutimiza viapo na nadhiri, na achunge ahadi au mkataba aliowekeana na mtu mwingine kwa mujibu wa Kitabu na Sunnah. Hivyo basi, asije mtu akabatilisha viapo na ahadi zilizo baina yake na Rabb wake, au baina yake na mtu mwengine.
Kutimiza ahadi ni sifa mojawapo inayoweza kumpatia mtu kuingizwa katika Jannatul-Firdaw kama Alivyoeleza Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Al-Muuminuwn (23:1-11) na Al-Ma’aarij (7:23-35).
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya kuwa kuvunja ahadi ni katika sifa ya unafiki: Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Alama za mnafiki ni tatu: Anapozungumza husema uongo, anapotoa ahadi hukhalifu (hatimizi), na anapoaminiwa hufanya khiyana.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[20] Kuteleza Mguu Baada Ya Kuthibitika Kwake:
Wala msivifanye viapo mnavyoviapa kuwa ndio njia ya kuwahadaa, kuwadanganya au kuwatapeli wale mliowaapia, mkaja kuangamia baada ya kuwa (mlithibitika) kwenye amani. Ni kama yule ambaye nyayo zake ziliteleza baada ya kuwa zimekita. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Wala msivichukulie viapo vyenu, ahadi zenu na mafungamano yenu kwa kufuata matamanio yenu; mnapotaka mnatimiza na mnapotaka mnazivunja. Basi mkifanya hivyo (kwa kutowajibika ipasavyo na hayo), miguu yenu itateleza baada ya kuwa imethibitika katika njia iliyonyooka. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Maana Ya Kuzuia Njia Ya Allaah:
Kafiri aliyekaribia kuingia Uislamu, akaja kuona tabia mbaya za baadhi ya Waislamu kama hiyo ya viapo vya udanganyifu zikamchukiza, huyo hatouthamini tena Uislamu, kwa kuona kuwa hakuna tofauti kubwa kati ya Waislamu na makafiri katika maadili na muamala wao. Na kwa tabia hiyo na mambo mengineyo ya ovyo yanayofanywa na baadhi ya Waislamu, inakuwa ni sababu ya kuwakimbiza wasio Waislamu kuingia kwenye Uislamu. Dini ni muamala mwema.
[21] Hayaatan Twayyibah (Uhai Au Maisha Mazuri):
Uhai au maisha mazuri haimaanishi mtu kuwa na utajiri wa mali na watoto, au siha nzuri, au maisha yaliyomjalia mafao na starehe. Bali uhai mzuri ni utulivu wa moyo na nafsi ya Muumini katika yote ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Amemkadiria na Kumjaalia, naye akaridhika nayo, na akawa na imaan thabiti bila kutetereka na mambo ya kidunia yanayomsibu. Mfano ni Muumini maskini anayepatwa na mitihani na maradhi, lakini akaridhika na Majaaliwa hayo kutoka kwa Rabb wake, na akaendelea kuishi kwa utulivu katika maisha yake kwa kuridhika na kushikamana na imaan thabiti. Hakufuru wala hapunguzi imaan yake kwa sababu ya mitihani aliyojaaliwa. Kinyume chake ni watu wengi ambao wako katika maisha ya utajiri, mali, watoto, raha, siha, na nguvu za miili, lakini watu hao wana dhiki za moyo za kuyafanya maisha yao kuwa ya dhiki tupu! Basi hao ndio ambao hawana maisha au uhai mzuri.
[22] Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Dhidi Ya Shaytwaan Unapoanza Kusoma Qur-aan:
Inapaswa kusema:
أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم
Najikinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.
[23] Hukmu Ya An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa):
Rejea Al-Baqarah (2:106). Na bonyeza kiungo kifuatacho:
An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa)
[27] Neno La أُمَّةً Katika Qur-aan Lina Maana Kadhaa:
Maana zake mbali mbali na baadhi ya Aayah zinazothibitisha maana zake:
(i) Umati wa watu; Rejea Al-Qaswasw (28:23), Al-A’raaf (7:164). (ii) Nyumati za karne zilizopita; Rejea Yuwnus (10:47), An-Nahl (16: 36). (iii) Mtu mwongofu au kiongozi mwenye taqwa na maadili na tabia njema; Rejea Al-Baqarah (2:124), na pia Aayah hii inayomkusudia Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). (iv) Muda au kipindi fulani au zama; Rejea Huwd (11:8], Yuwsuf (12:45). (v) Sharia, Dini, manhaj au mila inayofuatwa; Rejea Az-Zukhruf (43:22-23).
[28] Fadhila Na Sifa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام):
Katika Aayah (120-123) za Suwrah hii An-Nahl, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsifia Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kwa sifa zifuatazo: Mwenye akhlaaq na maadili yote mema, mtiifu, Haniyfah (ameelemea katika haki), hakuwa katika washirikina, mwenye kushukuru Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), mwongofu na miongoni mwa Swalihina.
Na katika Suwrah nyenginezo, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsifia pia kwa sifa nyenginezo mbalimbali na Akamjaalia kuwa na fadhila tele.
Miongoni Mwa Fadhila Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام):
(i) Allaah (سبحانه وتعالى) Amemteua yeye Nabiy Ibraahiym na mwanawe Nabiy Ismaa’iyl (عليهما السّلام) waijenge Al-Ka’bah. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamteua Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) awatangazie watu kwenda kutekeleza Hajj. Hivyo basi, akawa yeye (عليه السّلام) na ahli wake ni mwongozo kwa watu katika utekelezaji wa manaasik (ibaada na taratibu) za Hajj na ‘Umrah. Rejea Al-Hajj (22:26-37). Na miongoni mwa manaasik hizo, ni kuswali katika Maqaam Ibraahiym baada ya kutufu Al-Ka’bah. Rejea Al-Baqarah (2:125). Pia, kusai baina ya Swafaa na Marwah, rejea Al-Baqarah (2:158) kama ni kigezo cha mkewe Haajar alipokuwa akihangaika kumtafutia maji mwanawe Ismaa’iyl (عليه السّلام). Na huko ndiko palipotokea mbubujiko wa maji ya Zamzam ambayo watu wanakunywa kwa niya tofauti kama alivyogusia hilo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Pia kuchinja mnyama baada ya yeye kupewa mtihani au majaribio makubwa, pindi alipoona njozini kuwa anamchinja mwanawe, naye kutokana na utiifu wake, akataka kutekeleza njozi hiyo akiamini kuwa ni Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى). Lakini kumbe ilikuwa ni mtihani na jaribio, hivyo akafaulu katika hili, na hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akambadilishia kwa kumteremshia kondoo kutoka mbinguni ili amchinje badala ya mwanawe. Rejea Asw-Swaaffaat (37:101-107). Pia kutupia vijiwe Jamaraat ambayo ni katika waajibaat za Hajji na Sunnah zake nyenginezo.
(ii) Ni kipenzi cha Allaah. Rejea An-Nisaa (4:125).
(iii) Ameitwa Baba wa Manabii: Kama ilivyokuwa hali ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام): Al-‘Ankabuwt (29:27). Na katika Al-Hadiyd (57:26), ametajwa yeye Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) pekee kuwa amejaaliwa kuwa na Unabii na kupewa Kitabu.
Imaam Ibn Kathiyr amesema kuhusu Aayah ya Suwrah Al-‘Ankabuwt: “Hii ni fadhila na baraka kubwa sana. Sio tu kwamba Allaah Alimfanya (Nabiy Ibraahiym) kuwa ni kipenzi Chake na kumfanya Imaam wa watu, bali pia Alijaalia Unabii na Kitabu kuwa katika dhuriya zake. Baada ya zama za Ibraahiym, hapakuwa na Nabii ambaye hakutokana na kizazi chake. Manabii wote wa Wana wa Israaiyl (Ya’quwb) walikuwa katika kizazi chake, kuanzia Ya’quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym hadi wa mwisho wao, `Iysa bin Maryam, ambaye alisimama kuwatangazia kaumu yake, bishara ya kuja kwa Nabii Mwarabu, Al-Qurashiy, Al-Haashimiy, Nabii wa mwisho wa Manabii wote, bwana wa wana wa Aadam katika dunia hii na Aakhirah, ambaye Allaah Alimteua kutoka kwa Waarabu safi wa asili kutoka kwa kizazi cha Ismaa’iyl bin Ibraahiym (عليهما السلام). Hakuna Nabii yeyote katika ukoo wa Ismaa’iyl isipokuwa yeye Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
(iv) Ameomba duaa kizazi chake kitoe Nabii wa mwisho; Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baada ya kujenga Al-Ka’bah. Rejea (2:129).
(v) Ibraahiym (عليه السّلام) ni Imaam wa Tawhiyd:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfanya kuwa ni Imaam wa watu wa kufuatwa katika Tawhiyd. Rejea Al-Baqarah (2:124). Na pia Ummah umeusiwa kufuata mila yake. Rejea Al-Baqarah (2:135), Aal-‘Imraan (3:95), An-Nisaa (4:125), Al-An’aam (6:161), na An-Nahl (16:123). Na pia, Amewausia wanawe na kizazi chake Uislamu. Rejea Al-Baqarah (2:130-132). Na pia Amefanya neno la Tawhiyd (laa ilaaha illa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake. Rejea Az-Zukhruf (43:28). Ingawa Rusuli wengineo wote wamekuja pia katika kulingania Tawhiyd, ila Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) amekuwa ni makhsusi kwa Tawhiyd. Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema alipoulizwa:
Kwa nini Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) amehusishwa zaidi na Tawhiyd, ilhali Manabii wote wengineo wamelingania Tawhiyd?
Akajibu: Manabii wote wamekuja na (kulingania) Tawhiyd. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾
“Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: Hakika hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, basi Niabuduni.” [Al-Anbiyaa (21:25)]
Lakini Ibraahiym ni baba wa Waarabu, na baba wa Waisrael, naye amelingania Tawhiyd khalisi, na Mayahudi na Manaswara wamedai kuwa ni wafuasi wake, na Waislamu ndio wafuasi wake. Kwa hiyo yeye (عليه السّلام) akahusishwa kuwa ni baba wa Manabii, na kwamba yeye ndiye mwenye Haniyfiyyah (sifa ya kuelemea haki na kujiweka kando na shirki). Na sisi tumeamrishwa kumfuata, kwa sababu sisi ndio tulio karibu zaidi Ibraahiym kama Anavyosema Allaah (عزّ وجلّ):
إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾
“Hakika watu walio karibu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata na huyu Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah Ni Mlinzi wa Waumini.” [Aal-‘Imraan (3:68)]
Na Akasema kuwaradi Mayahudi na Manaswaara:
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٦٧﴾
“Ibraahiym hakuwa Yahudi wala Naswara, lakini alikuwa mwenye kujiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki, Muislamu na hakuwa miongoni mwa washirikina.” [Aal-‘Imraan (3:67)]
[Liqaa-a Al-Baab Al-Maftuwh Swali namba (7/189).
(vi) Anatajwa katika kila Swalaah, kwenye Tashahhud, kwa Swalaah inayojulikana kama Swalaatul-Ibraahiymiyyah.
Na fadhila hii tukufu ni kutokana na sababu zilizotangulia kutajwa juu na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn. Pia kutokana na sababu zifuatazo kama walivyosema ‘Ulamaa: Kwamba (عليه السّلام) Ibraahiym ni babu (kizazi kilichoanzia kwa Ismaaiyl) wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
Na ‘Allaamah Badr Ad-Diyn Al-Hanafiy (رحمه الله) ana maelezo mengineyo katika kubainisha sababu ya hili. Amesema: “Ikiwa mtu atauliza: Kwa nini Ibraahiym (عليه السّلام) ameteuliwa yeye pekee kutajwa katika Swalaah badala ya Manabii wengine (عليهم السّلام)?
Nitajibu: Kwa sababu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaona katika usiku wa Mi’iraaj, Manabii na Rusuli wote, na akamtolea Salaam kila Nabii, na hakuna hata mmoja wao aliyesalimia ummah wake isipokuwa Ibraahiym (عليه السّلام) . Hivyo basi, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametuamrisha tumswalie kila mwisho wa Swalaah mpaka Siku ya Qiyaamah, kama malipo ya wema wake. Na imesemwa: Ibraahiym (عليه السّلام) alipomaliza kuijenga Al-Ka’bah, aliuombea Ummah wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: Ee Allaah! Atakayehiji Nyumba hii miongoni mwa Ummah wa Muhammad, basi Mpe amani kutoka kwangu. Pia akawaombea ahli zake na watoto wake kwa duaa hii. Hivyo basi tukaamrishwa tuwakumbuke katika Swalaah kama malipo ya wema wao.” Mwisho. Ufafanuzi wa Sunan Abi Daawuwd cha Al-‘Ayniy (4/260). Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
(vii) Kizazi chake kimepewa ufalme mkubwa: An-Nisaa (4:54).
(viii) Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta mbingu ya saba akielemea Bayt Al-Ma’muwr inayozungukwa na Malaika elfu sabiini. (Haya yapo katika Hadiyth ndefu iliyopokelewa na Imaam Muslim katika Kitaab Al-Iymaan, na wengineo).
(ix) Alijaaliwa Ar-Rushd (Uongofu) na Allaah (سبحانه وتعالى) Alimjua vyema: Al-Anbiyaa (21:51).
(x) Ni Nabii ambaye amemshabihi Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) [Al-Bukhaariy, Muslim]
(xi) Ni miongoni mwa Rusuli watano wa Ulul-‘Azmi: Al-Ahzaab (33:7).
(xii) Amewaombea Waislamu wawe wenye kuelekeza nyoyo zao kuipenda Makkah na Al-Ka’bah. Ibraahiym (14:37).
(xiii) Amewaombea duaa kizazi chake wasimamishe Swalaah, na Amewaombea Waumini maghfirah Siku ya Hesabu. Ibraahiym (14:40-41).
(xiv) Atakuwa wa kwanza kuvalishwa nguo baada ya kufufuliwa kutokana na vile washirikina katika kaumu yake walivyomuingiza motoni akiwa uchi baada ya kuvunja masanamu yao. Yapo haya kwenye Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi watu, hakika mtafufuliwa na Allaah hali ya kuwa hamna viatu, mpo uchi na bila kutahiriwa (na magovi). ”Kisha akasoma:
كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ
“Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena.” [Al-Anbiyaa (21:104)]
Tanabahini! Hakika mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na ‘Ulamaa wameeleza pia kuwa sababu ya kutangulizwa Ibraahiym kuvishwa nguo Siku ya Qiyaamah kabla ya wengine ni kuwa hapakuweko miongoni mwa watu wa mwanzo na wa baadae, waliomkhofu zaidi Allaah kuliko yeye. Hivyo basi, nguo zitamharakia ili kumhifadhi, na moyo wake upate kutulia.
Na sababu nyingine -kama ilivyoeleza Hadiyth- ni kuwa, inawezekana kwamba yeye alikuwa ni wa kwanza kuvaa suruali wakati anaposwali ili kupata sitara ya ziada isiyo na shaka na kulinda tupu yake isigusane na sehemu yake ya kuswalia, naye akafanya kama alivyoamrishwa, na akalipwa hilo kuwa wa kwanza kusitiriwa Siku ya Qiyaamah.
Kadhalika, inawezekana kuwa wale waliomtupa motoni, walimwacha uchi na wakamvua nguo zote mbele ya watu kama anavyofanywa mtu anayetekelezewa adhabu ya kifo. Hivyo atalipwa nguo zake Siku ya Qiyaamah, na atakuwa mtu wa kwanza kuvaa mbele ya halaiki, na haya ni malipo mazuri zaidi. [Al-Qurtwubiy katika At-Tadhkirah]
(xv) Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema kwamba yeye ni kiumbe bora kabisa: Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Alikuja mtu mmoja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Ee kiumbe bora kabisa!” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjibu: “Huyo ni Ibraahiym (عليه السّلام). [Muslim]
Sifa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام):
(i) Hakuwa mshirikina kabisa. Ametajwa kwa sifa hii katika Suwrah kadhaa kwenye Qur-aan ikiwemo Suwrah hii An-Nahl (16:120). Pia, kisa chake katika Al-An’aam (6:74-81) cha kutokuabudu nyota wala mwezi wala jua kinathibitisha sifa hii. Kadhalika, alimuomba Allaah Amuepusha yeye na wanawe wasiwe washirikina: Ibraahiym (14:35). Isitoshe, alimnasihi baba yake pia asiwe mshirikina lakini hakumsikiliza bali alimfukuzilia mbali: Maryam (19:41-48) na Ash-Shu’araa (26:69-89).
(ii) Alikuwa ni mtimizaji ahadi: An-Najm (53:37).
(iii) Ni mwenye huruma mno na mvumilivu: At-Tawbah (9:114).
(iv) Ni mvumilivu sana, mnyenyekevu mno kwa Allaah, na mwingi wa kurejea Kwake. Huwd (11:75).
(v) Mkarimu mno: Huwd (11:69), na Adh-Dhaariyaat (51:24-26).
(vi) Mwenye utukufu: Rejea Tanbihi namba 1 ya Aayah namba (4) katika Suwrah Yuwsuf.
(vii) Mnyeyekevu, kwani aliomba duaa baada ya kujenga Al-Ka’bah: Al-Baqarah (2:128). Al-Ka’bah ni Nyumba Tukufu kabisa katika Vitukufu vya Allaah katika Mji Mtukufu kabisa. Lakini juu ya utukufu huu, alikuwa na wasiwasi juu ya kutaqabaliwa kitendo hiki, kwa maana hakuwa na kibri kuwa madamu amejenga kitu kitukufu kabisa cha Allaah, basi awe amesifika au ni mtu bora kabisa.
(viii) Ana kisa muhimu cha uthibitisho wa Tawhiyd iliyojikita moyoni mwake wakati alipoingizwa motoni na watu wake kwa sababu aliyavunja masanamu waliyokuwa wakiyaabudu: Al-Anbiyaa (21:51-70), na Asw-Swaaffaat (37:83-99).
(ix) Mwenye moyo uliosalimika: Asw-Swaaffaat (37:84).
(x) Swiddiyq (mkweli wa kidhati): Maryam (19:41).
(xi) Mwenye akhlaaq na mfano wa maadili mema: Al-Mumtahinah (60:4).
(xii) Amekhitariwa duniani, na Aakhirah ni miongoni mwa Swalihina: Al-Baqarah (2:130).
(xiii) Mwenye nguvu na busara: Swaad (38:45). Na katika busara zake, alimwambia mwanawe Ismaa’iyl abadilishe kizingiti chake badala ya kumwambia moja kwa moja “mwache mkeo.” Hii ni kutokana na malalamiko ya mke huyo kuhusu maisha yao na shida zao. Kisha akamtaka athibitishe kizingiti chake, akimaanisha aendeleze ndoa yake na mkewe mwengine (asimtaliki), mke wa pili ambaye hakulalamika shida zao za kimaisha. Maelezo ya hili yapo katika Hadiyth ndefu ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) iliyopokelewa na Al-Bukhaariy, Kitaab Ahaadiyth Al-Anbiyaa.
Pia katika busara zake ni kumtaka mfalme Namruwd aliyejifanya kuwa yeye ni Mola na mwabudiwa, alichomoze jua kutoka Magharibi badala ya Mashariki, lakini mfalme huyo akabakia kinywa wazi ameduwaa. Rejea Al-Baqarah (2:258) kwenye maelezo bayana katika faida ya Aayah hiyo.
Pia katika busara yake nyengineyo ni vile alivyovunja masanamu kisha akatundika shoka ya sanamu lilokuwa kubwa lao. Kaumu yake walipomuuliza nani aliyevunja masanamu yetu, alijibu: “Waulizeni wakiwa wanaweza kunena!” Akikusudia pia kama kweli wanastahiki kuabudiwa ikiwa hawawezi kujihami wenyewe kusingiziwa uvunjaji wa masanamu yao. Rejea Al-Anbiyaa (21:57-63), na Asw-Swaafaat (37:88-96)
(xiv) Alikhofia familia yake wasije kuabudu masanamu. Naye mwenyewe tokea utotoni alichukia ibaada ya shirki na masanamu. Na alikhiari Dini kuliko dunia, napo ni pale alipowaacha familia yake katika bonde la Makkah ambako hapakuwa na chochote, na alitaja sababu yake kuwa ili wasimamishe Swalaah: Ibraahiym (14:35-37).
Hizo ni baadhi ya fadhila na sifa za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) , na bila shaka zinapatikana nyenginezo katika Kitabu na Sunnah.
[29] As-Sabt: Rejea Al-Baqarah (2:65).