061 - Asw-Swaff

 

   الصَّف

 

061-Asw-Swaff

 

061-Asw-Swaff: Utangulizi Wa Suwrah

 

 Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿١﴾

1. Vimemsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi[1], Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾

2. Enyi walioamini!  Kwa nini mnasema yale msiyoyafanya?[2]

 

 

 

 

كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾

3. Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.

 

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ﴿٤﴾

4. Hakika Allaah Anapenda wale wanaopigana katika Njia Yake safusafu kama kwamba wao ni jengo lililoshikamana barabara.

 

 

 

 

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِي وَقَد تَّعْلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ ۖ فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٥﴾

5. Na pale Muwsaa alipoiambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnaniudhi na hali mmekwishajua kwamba hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu?[3] Basi walipopotoka, Allaah Akapotosha nyoyo zao, na Allaah Haongoi watu mafasiki.

 

 

 

 

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٦﴾

6. Na pale ‘Iysaa mwana wa Maryam aliposema: Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat, na mwenye kubashiria kuja kwa Rasuli baada yangu jina lake Ahmad.[4]  Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: Hii ni sihiri bayana.

 

 

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰ إِلَى الْإِسْلَامِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٧﴾

7. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo na hali yeye analinganiwa katika Uislamu? Na Allaah Haongoi watu madhalimu.

 

 

 

 

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿٨﴾

8. Wanataka kuizima Nuru ya Allaah kwa midomo yao, lakini Allaah Ni Mwenye Kuitimiza Nuru Yake japo makafiri watachukia.

 

 

 

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٩﴾

9. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.[5]

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿١٠﴾

10. Enyi walioamini! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo?

 

 

 

 

تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿١١﴾

11. Mumuamini Allaah na Rasuli Wake, na mfanye Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zenu, na nafsi zenu. Hivyo ndiyo bora kwenu mkiwa mnajua.

 

 

 

 

يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٢﴾

12. (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito na masikani mazuri katika Jannaat za kudumu milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa mno.

 

 

 

 

وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٣﴾

13. Na jengine mlipendalo, (nalo ni) nusura kutoka kwa Allaah na ushindi wa karibu. Na wabashirie Waumini.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنصَارَ اللَّـهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ ۖ فَآمَنَت طَّائِفَةٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ وَكَفَرَت طَّائِفَةٌ ۖ فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ﴿١٤﴾

14. Enyi walioamini! Kuweni wasaidizi wa Allaah kama alivyosema ‘Iysa mwana wa Maryam kwa wafuasi wake watiifu: Nani watakuwa wasaidizi wangu kwa ajili ya Allaah? Wafuasi watiifu wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Allaah. Basi likaamini kundi miongoni mwa wana wa Israaiyl na likakufuru kundi jingine. Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi.  

 

 

 

[1] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):

 

Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).

 

[3] Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) Aliudhiwa Mno Na Watu Wake:

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amemuombea duaa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kwa kuudhiwa kwake na watu wake:

 

حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي سُلَيْمَانُ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ قَسَمَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم قَسْمًا فَقَالَ رَجُلٌ إِنَّ هَذِهِ لَقِسْمَةٌ مَا أُرِيدَ بِهَا وَجْهُ اللَّهِ‏.‏ فَأَخْبَرْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَغَضِبَ حَتَّى رَأَيْتُ الْغَضَبَ فِي وَجْهِهِ وَقَالَ ‏ "‏ يَرْحَمُ اللَّهُ مُوسَى، لَقَدْ أُوذِيَ بِأَكْثَرَ مِنْ هَذَا فَصَبَرَ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abuu Waail kuwa ‘Abdullaah (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aligawa mgao (baina ya Waumini). Mtu mmoja akasema: “Mgao huu haukufanywa kumridhisha Allaah.” Nikamjulisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) [kuhusu jambo hilo], akaghadhibika mpaka nikaona ghadhabu zake usoni mwake, akasema: “Allaah Amrehemu (Nabiy) Muwsaa (عليه السّلام), hakika aliudhiwa kwa zaidi ya hili, hata hivyo akavuta subira.” [Al-Bukhaariy Kitaabu Cha Duaa (80)]

 

[4] Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametajwa Katika Bibilia Kuwa Atakuja Kuwa Nabii Wa Mwisho, Na Ahmad Ndiye Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): 

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ametajwa katika Vitabu vilivyotangulia vya mbinguni, na Allaah (سبحانه وتعالى) Amethibitisha katika Kauli Zake:

 

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾

“Na pale Allaah Alipochukua fungamano kwa Manabii (akawaambia): Ninayokupeni katika Kitabu na Hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi, basi ni lazima kumwamini na kumnusuru. (Kisha Allaah) Akasema: Je, mmekubali na mtashika fungamano Langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. (Allaah) Akasema: Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.” [Aal-‘Imraan (3:81).

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾

“Wale wanaomfuata Rasuli; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha mema na anawakataza munkari, na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vilivyo vibaya na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamnusuru na wakafuata Nuru (Qur-aan) ambayo imeteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.” [Al-a’raaf (7:157)]

 

Rejea katika Suwrah hiyo ya Al-A’raaf (7:157) kwenye ufafanuzi wake.

 

Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha jina la Ahmad:

 

عن جبير بن مطعم رضي الله عنه أن رسول اللهصلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ لِيْ أَسْمَاءً، أَنَا مُحَمَّدٌ، وَأَنَا أَحْمَدُ، وَأَنَا المَاحِي الَّذِي يَمْحُو الله بِيَ الكُفْرَ، وَأَنَا الحَاشِرُ الَّذِي يُحْشَرُ النَّاسُ عَلَى قَدَمَيَّ، وَأَنَا العَاقِبُ الَّذِي لَيْسَ بَعْدَهُ أَحَدٌ))

Amesimulia Jubayr Bin Mutw’im (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mimi nina majina kadhaa: Mimi ni Muhammad na mimi ni Ahmad, na mimi ni Al-Maahiy (mfutaji) ambaye Allaah Hufuta kufru kupitia kwangu, na mimi ni Al-Haashir (mkusanyaji) ambaye watu watakusanywa mbele ya miguu yangu (Siku ya Qiyaamah), na mimi ni Al-‘Aaqib (Wa mwisho) ambaye hakuna baada yake mtu (Nabiy).”   [Muslim]

 

Na pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amethibitisha Unabii wake kwa Mayahudi na Manaswara:

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ قَالَ ‏ "‏ وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لاَ يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلاَ نَصْرَانِيٌّ ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلاَّ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ‏"‏ ‏.‏

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, hatosikia mtu kuhusu mimi katika Ummah huu; Myahudi wala Mnaswara kisha asiamini kwamba nimetumwa na akafariki (katika ukafiri), ila atakuwa katika watu wa motoni.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na ifuatayo ni Fatwa aliyojibu Imaam Ibn ‘Uthaymiyn kuhusu shubha za watu wanaopinga kuwa jina la Ahmad halimaanishi ni Muhammad:

 

Jina La Ahmad Ni Sawa Na Muhammad:

 

Kuhusu Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٦﴾

Na pale ‘Iysaa mwana wa Maryam aliposema: Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat, na mwenye kubashiria kuja kwa Rasuli baada yangu jina lake Ahmad. Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: Hii ni sihiri bayana.

 

 

Swali: Alikuja mbabaishaji mmoja katika Manaswara akasema: Hakika Nabiy wetu (‘Iysaa) amesema: “Baada yake (atakuja Nabiy) jina lake Ahmad” na huyu aliepelekwa kutoka kwa Waarabu jina lake ni Muhammad, kwa hiyo huyu sio tuliyeahidiwa. Na sisi hivi sasa tunangojea mpaka aje Ahmad. Hivi jibu lake nini?

 

Jibu: Ahmad ni jina na Muhammad pia ni jina, na Nabiy (صلى الله عليه وسلم) ana majina mengi sana.

 

Hivyo basi, kwa nini limechaguliwa neno Ahmad kwenye bishara yake kwa Manaswara pasi na kutumia jina la Muhammad ambalo ndilo alilomuita Babu yake Abdul-Muttwalib?

 

Sikiliza ee ndugu yangu! Neno Ahmad ni jina la kufadhilisha (kuonesha ubora). Anakusudia kuwa ni mwenye kumshukuru sana Allaah kuliko viumbe wote, na mzuri zaidi kuliko wote kitabia. Hivyo basi, yeye ni Ahmad yenye maana ya Mahmuwd (mwenye kusifiwa), na Ahmad kwa maana ya Haamid (mwenye kuhimidi).

 

Ni jina la kufadhilisha kutokana na neno Haamid na Mahmuwd. Hakika limekuja jina hili kwa muundo huu ili wafahamu wale waliopewa bishara na Nabiy ‘Iysaa kuwa, huyu mtu ndiye mwenye haki zaidi ya kufuatwa, kwa sababu yeye ni mwenye kusifiwa zaidi ya watu wote. Jamani maneno yako wazi hapo au sivyo? (Wanadarasa wakajibu): “Naam yako wazi!” 

 

AlhamduliLlaah hawana hoja!  Sasa isikilize kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) iliyothibiti:  

(والذي نفسي بيده - أو قال : نفس محمد بيده - لا يسمع بي أحد من هذه الأمة)

“Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake.” Au kasema:  “Nafsi ya Muhammad imo Mkononi Mwake. Hatosikia mtu kuhusu mimi katika Ummah huu…”

 

Anakusudia Ummah unaolinganiwa, ambao anaoulingania Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na ambao ni ummah wa viumbe wote baada ya kutumwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

Hadiyth kamili ni hii ifuatayo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ قَالَ ‏ "‏ وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لاَ يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلاَ نَصْرَانِيٌّ ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلاَّ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ‏"‏ ‏.‏

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mkononi Mwake, hatosikia mtu kuhusu mimi katika Ummah huu; Myahudi wala Mnaswara kisha asiamini kwamba nimetumwa na akafariki (katika ukafiri), ila atakuwa katika watu wa motoni.” [Muslim] 

 

Amesema kweli Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), bila kiapo, kwani yeye ni mkweli na mwenye kusadikishwa. Na angalia jinsi alivyosema:

(لا يسمع بي يهودي ولا نصراني)

“Hatosikia mtu kuhusu mimi; Yahudi au Naswaara.”

 

Bila kusema na kufahamu kile nilichomlingania, ili asimamishiwe hoja lazima ajue hoja, kwa kusikia tu haiwi hoja mpaka afahamu, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ

Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake.

 

 Ili iweje?

لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ  

Ili awabainishie [Ibraahiym (14:4)]

 

Lau angetumwa Mwarabu kwa asiyekuwa Mwarabu, isingesimama hoja, na angetumwa Muajemi kwa Mwarabu isingesimama hoja. Lakini kwa Myahudi na Mnaswara kwa kule kusikia tu, wakasimamishiwa hoja.

 

Kwa nini?  Kwa sababu Mayahudi na Manaswara wanamfahamu zaidi, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyowafahamu watoto wao. Kwa kule kusikia kwao tu wanalazimika wamfuate. Na hata ikiwa hawamfahamu wakawa kama vile watu wa kawaida, italazimika wafanye uchunguzi wa kumfahamu, kwa kuwa walishafikishiwa na kupewa bishara (ya ujio wake), na zikatajwa sifa zake, ikawa wao wanamfahamu kama wanavyowafahamu watoto wao.  [Fataawa Al-Haram Al-Makkiy (01b-1420) Ibn ‘Uthaymiyn]

 

[5] Dini Ya Kiislamu Ndio Dini Itakayoshinda Dini Nyenginezo:

 

Aayah hii imetajwa katika Qur-aan kwenye Suwrah tatu. Rejea At-Tawbah (9:33),  Al-Fat-h (48:28).

 

عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزًّا يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلًّا يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ

Amesimulia Tamiym Ad-Daariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jambo hili (Uislaam) hakika litafika kila mahali palipoguswa na usiku na mchana. Allaah Hatoacha nyumba au makazi isipokuwa Allaah Ataingizi Dini hii kwa ‘izza (hadhi, utukufu na ushindi) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika. Allaah Atawapa utukufu watukufu kwa Uislaam na Atawadhalilisha wadhalili kwa Ukafiri.” [Ahmad]       

 

 عَنْ ثَوْبَانَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ: ((إِنَّ اَللَّهَ زَوَى لِيَ الأَرْضَ، فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا،  وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا. وَأُعْطِيتُ الْكَنْزَيْنِ الأَحْمَرَ وَالأَبْيَضَ. وَإِنِّي سَأَلْتُ رَبِّي لأُمَّتِي أَنْ لاَ يُهْلِكَهَا بِسَنَةٍ بِعَامَّةٍ، وَأَنْ لا يُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُّوا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ، فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ، وَإِنَّ رَبِّي قَالَ: يَا مُحَمَّدُ إِنِّي إِذَا قَضَيْتُ قَضَاءً فَإِنَّهُ لاَ يُرَدُّ، وَإِنِّي أَعْطَيْتُكَ لأُمَّتِكَ أَنْ لا أُهْلِكَهُمْ بِسَنَةٍ ِعَامَّةٍ، وَأَنْ لا أُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُّوا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ، وَلَوْ اِجْتَمَعَ عَلَيْهِمْ مَنْ بِأَقْطَارِهَا حَتَّى يَكُونَ بَعْضُهُمْ يُهْلِكُ بَعْضًا، وَيَسْبِيَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا))

Amesimulia Thawbaan (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Amenikusanyia ardhi (dunia) nikaona Mashariki yake na Magharibi yake. Na hakika Ummah wangu utaenea na kumiliki vyote vilivyo katika sehemu hizo nilokusanyiwa. Na nimepewa hazina mbili; nyekundu (Ufalme wa Kirumi) na nyeupe (Ufalme wa Kifursi). Hapo nikamuomba Rabb wangu Asijaalie Ummah wangu kuangamizwa kwa baa kuu la jumla na usitekwe na adui ajnabi atakayeuharibu mji mkuu wao na kuuangusha uongozi wao.  Rabb wangu Akajibu:  Ee Muhammad! Nikihukumu amri basi hakika hairudi. Nimekadiria kwamba Ummah wako hautahiliki mara moja kwa baa kuu la jumla na kwamba hautatekwa na adui ajnabi na kuharibu mji mkuu wao na kuuangusha uongozi wao, na hata kama maadui wa nchi zote wataungana dhidi yao, mpaka pale tu (Waislamu) watakapoanza kumalizana wenyewe kwa wenyewe na kutekana wao kwa wao.” [Muslim]

 

Bonyeza pia kiungo kifuatacho kwa faida ziyada:

 

57-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote

 

 

 

Share