066 - At-Tahriym
التَّحْرِيم
066-At-Tahriym
066-At-Tahriym: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١﴾
1. Ee Nabiy! Kwa nini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako! Na na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[1]
قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ ۚ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴿٢﴾
2. Allaah hakika Amekuwekeeni shariy’ah ya ukomboaji wa viapo vyenu, na Allaah Ni Mawlaa[2] wenu, Naye Ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّـهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ﴿٣﴾
3. Na pale Nabiy alipompa mmoja wa wake zake jambo la siri, na huyo mke alipoipasha habari na Allaah Akamdhihirishia (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم), akataarifu baadhi yake na akaacha nyingine. Basi alipomjulisha hayo, akasema: Nani aliyekujulisha haya? Akasema: Amenijulisha Mjuzi wa yote, Mwenye Ujuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ﴿٤﴾
4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (basi ni kheri kwenu), kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (kwa yanayomchukiza Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mawlaa wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia.[3]
عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾
5. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ibaada, wanaofunga Swiyaam[4] au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ﴿٦﴾
6. Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu pamoja na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanaulinda Malaika washupavu wasio na huruma, shadidi, hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.[5]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَعْتَذِرُوا الْيَوْمَ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٧﴾
7. Enyi waliokufuru! Msitoe nyudhuru Leo! Hakika mtalipwa yake mliyokuwa mkiyafanya.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٨﴾
8. Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha[6] (kwelikweli), asaa Rabb wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: Rabb wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu Ni Muweza.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٩﴾
9. Ee Nabiy! Pambana na makafiri na wanafiki kwa Jihaad (ya vita na hoja), na kuwa mshupavu kwao, na makazi yao ni Jahannam. Na ubaya ulioje mahali pa kuishia!
ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ ۖ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ﴿١٠﴾
10. Allaah Amewapigia mfano wale waliokufuru mke wa Nuwh na mke wa Luwtw. Wote wawili walikuwa chini ya waja wawili miongoni mwa Waja Wetu Swalihina, wakawafanyia hiana (katika Dini), basi (Manabii hao) hawakuwafaa chochote mbele ya Allaah, na ikasemwa: Ingieni motoni pamoja na wenye kuingia.
وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿١١﴾
11. Na Allaah Amewapigia mfano wale walioamini mke wa Firawni, aliposema: Rabb wangu! Nijengee nyuma Kwako kwenye Jannah, na Niokoe na Firawni na vitendo vyake, na Niokoe na watu madhalimu.[7]
وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ﴿١٢﴾
12. Na Maryam binti wa ‘Imraan ambaye amehifadhi tupu yake, Tukampulizia humo (katika nguo yake) kupitia kwa Ruwh Wetu (Jibriyl), na akasadikisha Maneno ya Rabb wake, na Vitabu Vyake, na akawa miongoni mwa watiifu na wanyenyekevu.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Kuanzia Aayah hii ya kwanza hadi Aayah namba (5), bonyeza kiungo kifuatacho:
Na pia rejea Al-Ahzaab (33:28) kwenye Sababu za Kuteremshwa Aayah zinazohusiana na za Suwrah hii ya At-Tahriym.
[2] Mawlaa: Mlinzi, Msaidizi.
Mawlaa ina maana nyingi: Mwenye kumiliki, msaidizi, mtu wa karibu kabisa, mtu aliyeacha mtumwa huru, na aliyeachiliwa huru, na maana ya mnusuruji. Lakini haipasi mja kumwita bwana wake Mawlaana kwa sababu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza hivyo katika Hadiyth iliyopokelewa na Imaam Muslim. [Imaam Ibn Baaz – Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb]
Na katika Qur-aan imetajwa kwa maana mbalimbali na zote zinategemea muktadha yake, kwani hata moto umetajwa kwa maana ya mawlaa, Rejea Al-Hadiyd (57:15).
Maana nyenginezo katika Qur-aan ni sayyid (bwana anayeendesha mambo ya mtu), mnusuruji, rafiki mwandani, mpenzi wa karibu, mlinzi, msaidizi, mwenye kumiliki, na kama alivyotaja Imaam Ibn Baaz hapo juu.
Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[3] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Aayah hii namba (4) na namba (5), bonyeza kiungo kifuatacho:
066-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tahriym Aayah 4-5: إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا
Rejea pia Al-Ahzaab (33:53) kwenye Sababu ya Kuteremshwa Aayah inayohusiana na za Suwrah hii ya At-Tahriym.
[5] Muumini Kujikinga Na Moto Pamoja Na Ahli Zake:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anatoa tahadharisho muhimu kabisa kwa Muumini kujikinga na moto pamoja na ahli zake. Na kujikinga na moto kutapatikana kwa kufuata na kutekeleza Amri Zake Allaah (سبحانه وتعالى) pamoja na amri za Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kujiepusha na makatazo yao. Miongoni mwa Kauli Zake nyengine Allaah (سبحانه وتعالى) za matahadhrisho ambayo yamejumuishwa na tahadharisho la moto wa Jahannam ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ifuatayo:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٢٩﴾ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَانًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾
“Enyi walioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatwilifu, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuwarehemuni. Na atakayefanya hivyo kwa uadui na dhulma, basi Tutamuingiza motoni. Na hilo kwa Allaah ni jepesi mno.” [An-Nisaa (5:29-30)]
Na miongoni mwa Hadiyth, ni ifuatayo ya amrisho la kutoa swadaqa au kusema maneno mazuri ambayo yanasababisha pia kujikinga na moto:
عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ فَإِنْ لَمْ تَجِدْ فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ)) متفق عليه
Amesimulia ‘Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ogopeni moto japo kwa (kutoa swadaqa) nusu tende, na usipopata basi kwa (kutamka) neno jema.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na njia mojawapo kubwa ya kujiepusha na moto ni kutimiza Swalaah pamoja na kuwaamrishwa ahli pia kusimamisha nguzo kuu hii ya Swalaah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ۖ لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكَ ۗ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَىٰ ﴿١٣٢﴾
“Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha uvumilivu juu ya mazito yake. Hatukukalifishi riziki bali Sisi Ndio Tunaokuruzuku. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa.” [Twaahaa (20:132)]
Rejea huko kupata faida nyenginezo zinazohusiana na maudhui hii ya kuamrisha ahli Swalaah.
[6] Tawbah Ya Nasuha:
Ni kutubia kikwelikweli kwa Allaah (عزّ وجلّ) kutokana na madhambi na Tawbah hii ya kikwelikweli ina mashari yake yafuatayo: (i) Kuomba maghfirah (ii) Kuacha hayo maasi (iii) Kujuta (iv) Kuweka niya (azimio) kutokurudia tena maasi hayo (v) Kama mtu amedhulumu haki ya mwengine, basi ni kuirudisha hiyo haki.
Rejea Rejea Huwd (11:3) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali. Pia An-Nisaa (4:110), Nuwh (71:10), Adh-Dhaariyaat (51:18).
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida za kuhusu maudhui ya Tawbah:
002-Riyaadhw Asw-Swalihiyn: Mlango Wa Tawbah
01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuomba Maghfirah
19-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha: Istighfaar (Kuomba Maghfirah) - كِتابُ الإسْتِغْفار
031-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swalaah: Swalaah Ya Tawbah
129-Hiswnul-Muslim: Kuomba Maghfirah Na Kutubia
Sayyidul Istighfaar Du’aa Bora Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Na Fadhila Za Kuomba Tawbah
007-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Maghfirah Na Tawbah
[7] Wanawake Watano Waliobora Kabisa Ulimwenguni:
Rejea Aal-‘Imraan (3:42) kwenye Hadiyth ambayo ametajwa Aasiyah mke wa Firawni na Maryam mama yake Nabiy Iysaa (عليه السّلام) ambao wametajwa katika Aayah mbili hizi (11-12) za Suwrah hii ya Atw-Twalaaq. Na katika Suwrah Aal-‘Imraan akatajwa pia ‘Aaishah (رضي الله عنها).
Na jumla ya wanawake bora kabisa ulimwenguni waliosifiwa kufikia daraja la ukamilifu ni watano, nao ni: (i) Aasiyah (aliyekuwa mke wa Firawni). (ii) Maryam mama yake Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). (iii) Khadiyjah Bint Khuwaylid. (iv) Faatwimah Bint Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). (v) ‘Aaishah mke wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
Na katika Hadiyth ifuatayo, wametajwa tena Aasiyah na Maryam, na pia ametajwa Khadiyjah Bint Khuwaylid (رضي الله عنها) na Faatwimah bint Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " حَسْبُكَ مِنْ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ مَرْيَمُ ابْنَةُ عِمْرَانَ وَخَدِيجَةُ بِنْتُ خُوَيْلِدٍ وَفَاطِمَةُ بِنْتُ مُحَمَّدٍ وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ " . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ صَحِيحٌ .
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanakutosheleza katika wanawake wa ulimwengu: Maryam bint ‘Imraan, Khadiyjah bint Khuwaylid Faatwimah bint Muhammad na Aasiyah mke wa Firawni.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hii ni Hadiyth Swahiyh na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy Uk au namba (3878)]
Rejea pia Suwrah Maryam (19:16) kwenye faida nyenginezo kuhusu mwanamke huyu mtukufu.