084 - Al-Inshiqaaq

 

  الإِنْشِقَاق

 

084-Al-Inshiqaaq

 

 

 

084-Al-Inshiqaaq: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾

1. Mbingu itakaporaruka.[1]

 

 

 

 

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٢﴾

2. Na ikamsikiliza na kumtii Rabb wake na ikawajibikiwa kufanya hivyo.

 

 

 

 

وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ﴿٣﴾

3. Na ardhi itakapotandazwa sawa (bila mwinuko wala mwinamo).

 

 

 

 

وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ﴿٤﴾

4. Na ikatupilia mbali vile vilivyomo ndani yake na ikawa tupu.

 

 

 

 

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٥﴾

5. Na ikamsikiliza na kumtii Rabb wake na ikawajibikiwa kufanya hivyo.

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ ﴿٦﴾

6. Ee binaadam! Hakika wewe unajikusurukusuru mno kuelekea kwa Rabb wako kwa juhudi na masumbuko, basi utakutana Naye.

 

 

 

 

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ ﴿٧﴾

7. Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia.[2]

 

 

 

 

فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴿٨﴾

8. Huyo atahesabiwa hesabu nyepesi.[3]

 

 

 

 

وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿٩﴾

9. Na atageuka kwa ahli zake akiwa mwenye furaha.

 

 

 

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ ﴿١٠﴾

10. Na ama yule atakayepewa kitabu chake nyuma ya mgongo wake.[4]

 

 

 

 

فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا ﴿١١﴾

11. Huyo ataomba kuteketea.

 

 

 

 

وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا ﴿١٢﴾

12. Na ataingia moto uliowashwa vikali mno aungue.

 

 

 

 

إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿١٣﴾

13. Hakika yeye alikuwa katika ahli zake mwenye kufurahi.

 

 

 

 

إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ﴿١٤﴾

14. Hakika yeye alidhani kwamba hatorudi kwenye asili yake.

 

 

 

 

بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا ﴿١٥﴾

15. Sivyo hivyo (bali atarudi tu)! Hakika Rabb wake Amekuwa Mwenye Kumuona daima.

 

 

 

 

فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ ﴿١٦﴾

16. Basi Naapa kwa wekundu wa kukuchwa jua.

 

 

 

 

وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ ﴿١٧﴾

17. Na Naapa kwa usiku na ambavyo umekusanya (na kugubika).

 

 

 

 

وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ ﴿١٨﴾

18. Na Naapa kwa mwezi unapokuwa mbalamwezi kamili.

 

 

 

 

لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ ﴿١٩﴾

19. Bila shaka mtapitia hatua baada ya hatua.[5]

 

 

 

 

فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾

20. Basi wana nini hawaamini?!  

 

 

 

 

وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩﴿٢١﴾

21. Na wanaposomewa Qur-aan, hawasujudu.[6]

 

 

 

 

بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ ﴿٢٢﴾

22. Bali wale waliokufuru wanakadhibisha.

 

 

 

 

وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ ﴿٢٣﴾

23. Na Allaah Anajua zaidi yale wanayoyakusanya ya siri.

 

 

 

 

فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٤﴾

24. Basi wabashirie adhabu iumizayo.

 

 

 

 

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٢٥﴾

25. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema, hao watapata ujira usiokatika.

 

 

 

 

[1] Miongoni Mwa Matukio Ya Siku Ya Qiyaamah:

 

Kuanzia mwanzo wa Aayah hadi namba (5) ni miongoni mwa matukio ya Siku ya Qiyaamah. Rejea At-Takwiyr (81:1) kwenye faida inayohusiana.

 

[2] Watakaopewa Vitabu Vyao Kuliani Mwao:

 

Kuanzia Aayah hii namba (7) na zinazofuatia (8-9), zinataja hali za watu watakaopewa vitabu vyao kuliani. Rejea Al-Haaqqah (69:19-24).

 

[3] Waumini Watakaopewa Vitabu Vyao Kuliani Watafanyiwa Hesabu Nyepesi:

 

Hesabu nyepesi itakuwa ni mazungumzo mepesi ya matendo yake mbele ya Allaah (عزّ وجلّ).  Allaah (عزّ وجلّ) Atamfanya akiri madhambi yake mpaka atapodhani kuwa ameangamia basi hapo Humfanyia hesabu nyepesi. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Na hesabu nyepesi ni ambayo Allaah  (سبحانه وتعالى) Hatomsaili mja kuhusu madhambi yake, bali Atamghufuria bila ya kumuuliza, kwani atakayesailiwa na Allaah kuhusu madhambi yake, basi huyo ataangamia. Imethibiti hivyo katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏"‏ لَيْسَ أَحَدٌ يُحَاسَبُ إِلاَّ هَلَكَ ‏"‏ ‏.‏ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلَيْسَ اللَّهُ يَقُولُ حِسَابًا يَسِيرًا قَالَ ‏"‏ ذَاكِ الْعَرْضُ وَلَكِنْ مَنْ نُوقِشَ الْحِسَابَ هَلَكَ ‏"‏ ‏.‏

 

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna yeyote atakayehesabiwa isipokuwa ataangamia.”  Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, si Allaah Anasema:  Hesabu Nyepesi? Akasema: “Hiyo ni kudhihirishiwa tu madhambi yake, lakini atakayesailiwa hesabu yake, basi ataangamia.” [Muslim Kitabu Cha Jannah, Sifa za Neema Zake na Watu Wake] 

 

Na Hadiyth ifuatayo inathibitisha kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Atasitiri madhambi ya mja Wake na Atamghufuria, kwa hivyo Hatomsaili:

 

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ صَفْوَانَ بْنِ مُحْرِزٍ، أَنَّ رَجُلاً، سَأَلَ ابْنَ عُمَرَ كَيْفَ سَمِعْتَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ فِي النَّجْوَى قَالَ ‏ "‏ يَدْنُو أَحَدُكُمْ مِنْ رَبِّهِ حَتَّى يَضَعَ كَنَفَهُ عَلَيْهِ فَيَقُولُ عَمِلْتَ كَذَا وَكَذَا‏.‏ فَيَقُولُ نَعَمْ‏.‏ وَيَقُولُ عَمِلْتَ كَذَا وَكَذَا‏.‏ فَيَقُولُ نَعَمْ‏.‏ فَيُقَرِّرُهُ ثُمَّ يَقُولُ إِنِّي سَتَرْتُ عَلَيْكَ فِي الدُّنْيَا، فَأَنَا أَغْفِرُهَا لَكَ الْيَوْمَ ‏"‏‏.‏

Amesimulia Swafwaan Bin Muhriz (رضي الله عنه):  Mtu mmoja alimuuliza Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما):  Je, umemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema nini kuhusu an-najwaa (kunong’onezana baina ya Allaah na mja Wake Muumini Siku ya Qiyaamah)? Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mmoja wenu atakuja karibu na Rabb Wake mpaka Atamfinika na pazia Yake, Atamwambia: Je, ulifanya kadhaa na kadhaa? (Mja) Atasema: Naam.  Kisha Allaah Atasema: Je, ulifanya kadhaa na kadhaa? Atasema: Naam. Kwa hiyo, Allaah Atamfanya akiri (makosa yake), kisha Atasema: Hakika Nilikusitiria duniani (madhambi yako) na leo nakughufuria.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Adabu (78), Kitabu Cha Tawhiyd (97)]

 

Na pia kuhusu hesabu nyepesi ni Hadiyth ifuatayo:

 

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي مَرْيَمَ، قَالَ أَخْبَرَنَا نَافِعُ بْنُ عُمَرَ، قَالَ حَدَّثَنِي ابْنُ أَبِي مُلَيْكَةَ، أَنَّ عَائِشَةَ، زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم كَانَتْ لاَ تَسْمَعُ شَيْئًا لاَ تَعْرِفُهُ إِلاَّ رَاجَعَتْ فِيهِ حَتَّى تَعْرِفَهُ، وَأَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏"‏ مَنْ حُوسِبَ عُذِّبَ ‏"‏‏.‏ قَالَتْ عَائِشَةُ فَقُلْتُ أَوَ لَيْسَ يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى   ‏فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا  قَالَتْ فَقَالَ ‏"‏ إِنَّمَا ذَلِكَ الْعَرْضُ، وَلَكِنْ مَنْ نُوقِشَ الْحِسَابَ يَهْلِكْ ‏"‏‏.‏

Amesimulia Ibn Abu Mulaykah (رضي الله عنه): Kila wakati (Mama wa Wumini) ‘Aaishah aliposikia jambo ambalo hakulielewa, alikuwa akiuliza tena mpaka afahamu. ‘Aaishah alisema: “Wakati mmoja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Yeyote atakayeitwa kusailiwa (na Allaah) amali zake Siku ya Qiyaamah hapana shaka ataadhibiwa.” Nikasema:  Je, Allaah (سبحانه وتعالى) Hakusema:

فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴿٨﴾

Atahesabiwa hesabu nyepesi. [Al-Inshiqaaq (84:9)]

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika hii inamaanisha uwasilishaji wa hesabu tu lakini mtu yeyote atakayesailiwa kuhusu hesabu yake ataangamia.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Ilmu (3)] 

 

[Al-Bukhaariy Kitabu Cha Ilmu (3)]

 

[4] Watakaopewa Vitabu Vyao Kushotoni Mwao:

 

Rejea Al-Haaqqah (69:25-37) kwenye maelezo yao.

 

[5] Kupitia Hatua Baada Ya Hatua:

 

Yaani hatua nyingi tofauti (za mwanaadam) kuanzia manii hadi pande la damu linalonin’ginia, kisha kinofu cha nyama, kisha kupulizwa roho, kisha kuzaliwa na utoto, kisha kufikia umri wa utambuzi, halafu kuanza kusajiliwa mema yake na mabaya yake pamoja na maamrisho na makatazo baada ya kubaleghe. Kisha baada ya yote hayo, mwanaadam hufariki, halafu atakuja kufufuliwa ili alipwe matendo yake. Hatua hizi mbalimbali ambazo mwanaadam hupitia, zinaashiria kwamba Allaah Pekee Ndiye Anayestahiki kuabudiwa, Yeye Ni Mmoja Pweke, na Ndiye Mwenye kudabiri mambo ya Waja Wake kwa Hikma Yake na Rehma Yake, na kwamba mja ni faqiri, na hana uwezo chini ya Uendeshaji wa Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[6] Sajdatut-Tilaawah: Sijdah Ya Kisomo.

 

Anapofika mtu Aayah hii anatakiwa asujudu.  Rejea Al-A’raaf (7:206) kwenye maelezo na faida kadhaa.

 

 

Share