089 - Al-Fajr
الْفَجْر
089-Al-Fajr
089-Al-Fajr: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالْفَجْرِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa Alfajiri.
وَلَيَالٍ عَشْرٍ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa masiku kumi.[1]
وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa shufwa na witri.
وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ ﴿٤﴾
4. Na Naapa kwa usiku unapopita.
هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ ﴿٥﴾
5. Je, katika hayo pana haja ya kiapo kwa mwenye akili?
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ ﴿٦﴾
6. Je, hukuona vipi Rabb wako Alivyowafanya kina ‘Aad?[2]
إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ ﴿٧﴾
7. Wa Iram[3], walio warefu na wenye nguvu (kama nguzo ndefu)?
الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ ﴿٨﴾
8. Ambao hawakuumbwa mfano wao katika ardhi.
وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ ﴿٩﴾
9. Na kina Thamuwd ambao walichonga miamba mabondeni?
وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ ﴿١٠﴾
10. Na Firawni mwenye askari washupavu na nguvu kubwa.[4]
الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ ﴿١١﴾
11. Ambao wote hao wamevuka mipaka kuasi katika nchi.
فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ ﴿١٢﴾
12. Wakakithirisha humo ufisadi.
فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ ﴿١٣﴾
13. Rabb wako Akawamiminia mjeledi wa adhabu.
إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ ﴿١٤﴾
14. Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Anaziona nyenendo zao zote.
فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ ﴿١٥﴾
15. Basi binaadam pale Rabb wake Anapomtia mtihanini, Akamkirimu na Akamneemesha, husema: Rabb wangu Amenikirimu.
وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ ﴿١٦﴾
16. Ama Anapomtia mtihanini, Akamdhikishia riziki yake, husema: Rabb wangu Amenidunisha.
كَلَّاۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ ﴿١٧﴾
17. Laa hasha! Bali hamuwakirimu mayatima.[5]
وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿١٨﴾
18. Na wala hamhamasishani katika kulisha maskini.[6]
وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا ﴿١٩﴾
19. Na mnakula urithi ulaji wa kiroho bila kusaza kitu.
وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا ﴿٢٠﴾
20. Na mnapenda mali penzi kubwa la kupita kiasi.
كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا ﴿٢١﴾
21. Laa hasha! Pale ardhi itakapo vunjwavunjwa na kupondwapondwa.
وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ﴿٢٢﴾
22. Na Atakapokuja Rabb wako pamoja na Malaika walio safusafu.[7]
وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾
23. Na italetwa siku hiyo Jahannam. Siku hiyo binaadam atakumbuka. Lakini kutamfaa nini kukumbuka huko?!
يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي ﴿٢٤﴾
24. Atasema: Ee, laiti ningelikadimisha (mazuri) kwa ajili ya uhai wangu (wa Aakhirah).
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ ﴿٢٥﴾
25. Basi siku hiyo hakuna yeyote atakayeadhibu kama Kuadhibu Kwake.
وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ ﴿٢٦﴾
26. Na wala hakuna yeyote atakayefungisha (madhubuti) kama kufungisha Kwake (waovu).
يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾
27. (Mwema ataambiwa): Ee nafsi iliyotua!
ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾
28. Rejea kwa Rabb wako ukiwa umeridhika na mwenye kuridhiwa (na Allaah).
فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾
29. Basi ingia katika kundi la Waja Wangu.
وَادْخُلِي جَنَّتِي ﴿٣٠﴾
30. Na ingia Jannah Yangu.
[1] Masiku Kumi Anayoyaapia Allaah (سبحانه وتعالى):
Baada ya kuapia kwa Alfajiri, Allaah (عزّ وجلّ) Anaapa kwa masiku kumi ambayo kwa mujibu wa rai iliyo sahihi, ni nyusiku kumi za mwezi wa Ramadhwaan na mchana wa masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah. Hizi ni siku ambapo matendo mengi ya ibaada hufanyika ambayo hayafanyiki nyakati nyingine. Katika kumi la mwisho la usiku wa Ramadhwaan, kunatokea Laylatul-Qadr ambao ni usiku bora kuliko miezi elfu, na siku hizo kumi ni siku za mwisho za mfungo wa Ramadhwaan ambayo ni moja ya nguzo za Uislamu.
Katika siku kumi za Dhul-Hijjah, kuna kisimamo cha ‘Arafah ambapo Allaah (عزّ وجلّ) Anawaghufuria waja, na hilo humhuzunisha mno shaytwaan. Shaytwaan haonekani kamwe kudhalilika vibaya na kushindwa zaidi kuliko Siku ya ‘Arafah anapoona Malaika wakiteremka na Rehma toka kwa Allaah kwa Waja Wake, na kwa sababu ya yale yanayotokea siku hiyo ya wingi wa matendo ya ibaadah ya Hajj na ‘Umrah. Basi hayo ni mambo matukufu mno yanayostahiki kuapiwa na Allaah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Bonyeza viungo vifuatavye vyenye faida muhimu kuhusu masiku hayo:
Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah - 01 - 10 Dhul-Hijjah
Siku Kumi Za Mwisho Za Ramadhwaan
[2] Kina ‘Aad Kaumu Ya Nabiy Huwd (عليه السّلام):
Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye maelezo kuhusu Makafiri Wa Nyumati Za Nyuma Na Aina Za Adhabu Zao:
[3] Iram:
‘Ulamaa wametaja maana zifuatazo za Iram: (i) Imaam As-Sa’diy: Kabila maarufu la Yemen [Tafsiyr As-Sa’diy]. (ii) Mujaahid na Qataadah: Ummah wa zamani yaani ‘Aad wa kwanza. (iii) Qataadah bin Du’aamah, As-Suddiy: Iram ni nyumba ya mamlaka ya ‘Aad. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[5] Amri Na Himizo La Kuwakirimu Yatima Na Fadhila Zake:
Miongoni mwa fadhila za kulea yatima ni kujaaliwa kuwa karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Jannah kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عن سهل بن سعد رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أَنَا وَكَافلُ اليَتِيمِ في الجَنَّةِ هَكَذا )) وَأَشارَ بالسَّبَّابَةِ وَالوُسْطَى ، وَفَرَّجَ بَيْنَهُمَا . رواه البخاري .
Amesimulia Sahl Bin Sa’ad (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mimi na mwenye kumsimamia yatima tuko Peponi kama hivi." Akaashiria kwa kidole cha shahada na cha kati na kupambanua baina yake. [Al-Bukhaariy]
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo kadhaa:
033-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwafanyia Upole Mayatima, Mabinti, Wanyonge wote, Maskini, Waliofilisika Pamoja na Kuwafanyia Hisani, Kuwahurumia, Kuwanyenyekea na kuwainamishia Bawa
220-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 220: وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ
Na uharamu wa kula mali za yatima na kuwfanyia ubaya ni katika viungo vifuatavyo:
033-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kula Mali ya Yatima
010-Aayah Na Mafunzo: Kula Mali Ya Yatima Ni Miongoni Mwa Mambo Saba Yanayoangamiza
06-Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An'aam: Kutokuikaribia Mali ya Yatima Ila Kwa Kukusudia Ihsaan
[6] Himizo La Kulisha Chakula Mafaqiri, Masikini Na Wahitaji:
Rejea Al-Insaan (76:8) kwenye faida tele. Na pia rejea Al-Qalam (68:17) kwenye kisa cha watu wa shamba waliozuia mafuqara na masikini wasipate swadaqa ya mazao ya shamba la baba yao baada ya kufariki kwake. Na pia kisa katika Hadiyth, cha mtu aliyekuwa akitoa swadaqa mazao yake, na faida nyenginezo.
[7] Malaika Watateremka Siku Ya Qiyaamah Safusafu Na Allaaha Pia Atateremka.
Rejea Al-Haaqqah (69:13-18), Al-Fajr (89:21-22), Al-Furqaan (25:25), Al-Baqarah (2:210), Al-An’aam (6:158).