091 - Ash-Shams

 

الشَّمْس

 

091-Ash-Shams

  

091-Ash-Shams: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا ﴿١﴾

1. Naapa kwa jua na mwangaza wake.

 

 

 

وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa mwezi unapoliandama (jua).

 

 

 

وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا ﴿٣﴾

3. Na Naapa kwa mchana unapolidhihirisha.

 

 

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا ﴿٤﴾

4. Na Naapa kwa usiku unapolifunika.

 

 

وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا ﴿٥﴾

5. Na Naapa kwa mbingu na Aliyezijenga.

 

 

وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا ﴿٦﴾

6. Na Naapa kwa ardhi na Aliyeitandaza.

 

 

وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا ﴿٧﴾

7. Na Naapa kwa nafsi na Aliyeiumba Akainyoosha sawa.

 

 

 

فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا ﴿٨﴾

8. Kisha Akaitambulisha uovu wake na taqwa yake.[1]

 

 

 

قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا ﴿٩﴾

9. Kwa yakini amefaulu yule aliyeitakasa.[2]

 

 

وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا ﴿١٠﴾

10. Na kwa yakini amepita patupu aliyeifisidi.[3]

 

 

كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا ﴿١١﴾

11. Kina Thamuwd walikadhibisha (Rasuli wao) kwa upindukaji mipaka ya kuasi kwao.[4]

 

 

إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا ﴿١٢﴾

12. Pale alipochomoka haraka muovu wao mkuu.

 

 

فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّـهِ نَاقَةَ اللَّـهِ وَسُقْيَاهَا ﴿١٣﴾

13. Rasuli wa Allaah (Swaalih عليه السلام) akawaambia: (Tahadharini msije kumdhuru) Ngamia jike wa Allaah, na kuingilia zamu yake ya kunywa.

 

 

 

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا ﴿١٤﴾

14. Lakini walimkadhibisha na wakamuua. Basi Rabb wao Akawaangamiza kwa sababu ya dhambi zao, na Akayafanya mateketezi yao sawasawa kwa wote.

 

 

وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا ﴿١٥﴾

15. Na wala (Allaah) Hakhofu matokeo yake.

 

 

 

 

[1] Mwanaadam Ana Uhuru Wa Kuinusuru Nafsi Yake Au Kuiangamiza:

 

Hadiyth ifuatayo inataja kuwa ni chaguo la binaadam kuichunga nafsi yake akasalimika au kuiharibu akaangamia.

 

عن أبي مالكٍ الحارِثِ بنِ عاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رضي اللهُ عنهُ قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيَمانِ، والحمدُ لِلهِ تَمْلأُ الْمِيزَانَ، وسُبْحانَ اللهِ والحمدُ لِلهِ تَمْلآنِ - أو تَمْلأُ - ما بَيْنَ السَّمآءِ والأرضِ، والصَّلاةُ نورٌ، والصَّدَقَةُ بُرْهانٌ، والصَّبْرُ ضِيَاءٌ، والْقُرآنُ حُجَّةٌ لَكَ أو عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدو، فَبائعٌ نَفْسَهُ، فَمُعْتِقُها أَو مُوبِقُها))  رَوَاهُ مُسْلِمٌ   

Amesimulia Abuu Maalik Al-Haarith bin ‘Aaswim Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Twahaara ni nusu ya imaan, na AlhamduliLLaah inajaza mizani, na Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah inajaza baina ya mbingu na ardhi.  Na Swalaah ni nuru, na swadaqa ni burhani, na subira ni mwangaza, na Qur-aan ni hoja kwako au dhidi yako. Kila mtu anaianza siku yake akiichuuza nafsi yake, aidha huiokoa ikasalimika au akaiangamiza.” [Muslim]

 

Rejea Al-Insaan (76:3).

 

Rejea pia Aayah namba (9) ya Suwrah hii kwenye faida nyenginezo.

 

[2] Kuichunga Nafsi, Kuitakasa Na Kujaaliwa Taqwa Na Duaa Zake:

 

 Bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Mahitajio Ya Nafsi: Kuomba Maghfirah Na Kutubia Kwa Allaah (سبحانه وتعالى)

 

Asili Ya Roho Zetu

 

Faida Ya Taqwa (Uchaji Allaah)

 

Na pia bonyeza viungo vifuatavyo kupata duaa za kuomba kuitakasa nafsi na kuomba kujaaliwa taqwa:

 

041-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Taqwa Ya Nafsi Na Kuitakasa

 

 

021-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Hidaaya, Taqwa, Sitaha Na Kutosheka

 

 

013-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Shari Ya Nafsi, Kuthibitika, Maghfirah Ya Dhambi Za Kila Aina

 

 

044-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Ilhamu Ya Uongofu Na Kuomba Kinga Ya Shari Za Nafsi

 

 

045-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Dhidi Ya Moyo Usionyenyekea, Du'aa Isiyosikizwa, Nafsi Isiyoshiba, Elimu...

 

051-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Kushindwa Hila, Kuomba Taqwa Ya Nafsi,Kinga Ya Elimu Isiyonufaisha, Moyo Usionyeyekea, Nafsi ...

 

 

[3] Kuifisidi Nafsi:

 

Bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Majuto Ya Nafsi - 1

 

Majuto Ya Nafsi - 2

 

 

[4] Kina Thamuwd Kaumu Ya Nabiy Swaalih (عليه السّلام):

 

Kina Thamuwd ni watu wa Al-Hijr ambayo ni maeneo yapo baina ya Sham na Hijaaz. Kina Thamuwd hawa walipinga daawah ya Rasuli wao Nabiy Swaalih (عليه السّلام)  juu ya kutaka muujiza wa kuteremshiwa ngamia jike. Walipoitikiwa matakwa yao, walimuua ngamia wa Allaah.

 

Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye maelezo kuhusu Makafiri Wa Nyumati Za Nyuma Na Aina Za Adhabu Zao.

 

 

 

Share