092 - Al-Layl

 

  اللَّيْل

 

092-Al-Layl

 

092-Al-Layl: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa usiku unapofunika.

 

 

 

 

وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa mchana unapodhihirika mwanga wake.

 

 

 

 

 

وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣﴾

3. Na Naapa kwa Aliyeumba dume na jike.

 

 

 

 

إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ ﴿٤﴾

4. Hakika juhudi zenu bila shaka ni tofauti tofauti.

 

 

 

 

 

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾

5. Basi yule anayetoa (mali) na akamcha Allaah.

 

 

 

 

وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾

6. Na akasadikisha Al-Husnaa.[1] (Jazaa na Kalimah ya laa ilaaha illa Allaah). 

 

 

 

 

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾

7. Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi.[2]

 

 

 

 

وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza.

 

 

 

 

وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾

9. Na akakadhibisha Al-Husnaa[3] (Jazaa na Kalimah ya laa ilaaha illa Allaah). 

 

 

 

 

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾

10. Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.[4]

 

 

 

 

وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾

11. Na itamsaidia nini mali yake atakapoporomoka kuangamia (motoni)?!

 

 

 

 

إِنَّ عَلَيْنَا لَلْـهُدَىٰ ﴿١٢﴾

12. Hakika ni juu Yetu (kubainisha) mwongozo.

 

 

 

وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ ﴿١٣﴾

13. Na hakika ni Yetu Sisi Aakhirah na awali (dunia).

 

 

 

فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ ﴿١٤﴾

14. Basi Nimekutahadharisheni moto wenye mwako mkali mno.

 

 

 

 

لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى ﴿١٥﴾

15. Hatouingia kuungua isipokuwa muovu mkubwa.

 

 

 

الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٦﴾

16. Ambaye amekadhibisha na akakengeuka mbali.

 

 

 

 

 

وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿١٧﴾

17. Na ataepushwa nao mwenye taqwa imara zaidi.

 

 

 

الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾

18. Ambaye anatoa mali yake kujitakasa.

 

 

 

 

وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾

19. Na hali hakuna mmoja yeyote aliyemfanyia fadhila yoyote hata amlipe.[5]

 

 

 

 

إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾

20. Isipokuwa kutaka Wajihi wa Rabb wake Mwenye ‘Uluwa Aliyetukuka kabisa kuliko vyote.[6]

 

 

 

 

وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ﴿٢١﴾

21. Na bila shaka atakuja kuridhika.

 

 

[1] Kusadikisha Al-Husnaa:

 

Kauli za ‘Ulamaa:

 

Tafsiyr Al-Muyassar:

 

Akaamini Laa ilaaha illa-Allaah, maana ya neno hili na malipo yanayotarajiwa, basi Tutamwongoza, Tutamwezesha na Tutamrahisishia kuzifikia nyenzo za kheri na utengefu.  

 

Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):

 

Akaamini Laa ilaaha illa-Allaah, maana yake ikiwa ni pamoja na yote ya Dini anayopaswa kuyaamini, na malipo ya Aakhirah yanayotarajiwa kutokana na neno hilo.

 

Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله):

 

(i) Jazaa (ii)Thawabu (iii) Badali (iii) La ilaaha illa-Allaah (iv) Aliyoneemeshwa na Allaah (v) Swalaah, Zakaat, Swawm, Swadaqa ya Fitwr.

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله):

 

Akaamini maneno bora kabisa ambayo ni maneno ya Allaah (عزّ وجلّ) na kauli ya Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sababu maneno ya kweli na yaliyo bora kabisa ni Maneno ya Allaah (عزّ وجلّ).

 

[2] Kufanyiwa Yaliyo Mepesi:

 

Tunamfanyia mambo yake mepesi, na Tunamwepesishia kila jambo jema, na Tunamrahisishia kuacha maovu yote, kwa sababu amechukua hatua zinazopelekea hilo, basi Allaah (عزّ وجلّ)  Atafanya wepesi hilo kwa ajili yake. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[3] Kukadhibisha Al-Husnaa:

 

Kauli za ‘Ulamaa:

 

Tafsiyr Al-Muyassar:

 

Akakanusha neno la Laa ilaaha illa-Allaah, maana yake na malipo yanayotarajiwa kutokana nalo.

 

Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):

 

Ambayo Allaah (عزّ وجلّ) Amewajibisha Waja Wake kuyaamini ya ‘Aqiydah sahihi.

 

Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله):

 

Jazaa ya makazi ya Aakhirah.  

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله):  Kauli za Allaah (عزّ وجلّ) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

[4] Kuwepesishiwa Magumu:

 

Atatekeleza yaliyo na sifa mbaya ya kulaumiwa na atafanyiwa wepesi kutenda maovu na maasi popote alipo. Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[5] Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Bila Kutarajia Sifa, Fadhila Au Malipo Kwa Watu:

 

Aayah hii amekusudiwa Abu Bakr (رضي الله عنه) [Tafsiyr As-Sa’diy] na wengineo.

 

Kwa sababu Abu Bakr (رضي الله عنه) hakutaraji malipo au fadhila kutoka kwa watu bali alitaraji Radhi za Allaah Pekee. Na miongoni mwa aliyoyatenda Abu Bakr (رضي الله عنه) ni kuwakomboa Waislamu waliokandamizwa na kuadhibiwa na makafiri Quraysh wa Makkah katika mwanzo wa Uislamu. Kati ya watumwa hao aliowakomboa ni Swahaba mtukufu Bilaal bin Rabaah (رضي الله عنه) ambaye alikuwa Muadhini wa Waislamu. Hali kadhalika walikombolewa watumwa wanawake na wala hakujali kiasi cha mali alichokitoa na wala hakutaraji kusifiwa na watu wala malipo yao isipokuwa kutaka Radhi za Allaah. Rejea pia An-Nuwr (24:22) kwenye maelezo yake alipoendelea kumpa swadaqa jamaa yake Mistwah Bin Uthaathah, juu ya kuwa aliudhika naye, lakini alitii amri ya Allaah (عزّ وجلّ) ya kutaraji kughufuriwa madhambi yake.

 

[6] Al-A’laa:

 

Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Ana Uadhama Kuliko wote kuliko vyote, Yuko juu Kabisa juu ya viumbe Vyake vyote.

 

 

 

 

Share