093 - Adh-Dhuhaa

 

   الضُّحى

 

093-Adhw-Dhwuhaa

 

093-Adhw-Dhwuhaa: Utangulizi Wa Suwrah

 

 Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa dhuha (jua linapopanda).[1]

   

 

 

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.

 

 

 

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).[2]

 

 

وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ ﴿٤﴾

4. Na bila shaka Aakhirah ni kheri zaidi kwako kuliko ya awali (dunia).

 

 

 

وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ ﴿٥﴾

5. Na bila shaka Rabb wako Atakupa na utaridhika.

 

 

 

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾

6. Je, kwani Hakukukuta yatima, Akakupa makazi?

 

 

 

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾

7. Na Akakukuta hujui lolote (kuhusu Kitabu wala Iymaan), kisha Akakuongoza?

 

 

 

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Na Akakukuta mhitaji, Akakutosheleza?

 

 

 

فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾

9. Kwa hivyo basi yatima usimuonee.

 

 

وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾

10. Na ama mwombaji, basi usimkaripie.

 

 

 

وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ ﴿١١﴾

11. Na ama Neema ya Rabb wako, basi ihadithie.[3]

 

 

 

 

 

 

[1] Dhuhaa:

 

Ni wakati wa mwanzo wa mchana jua linapopanda, au mchana wote kwa mkabala wa usiku.

 

[3] Kutambua Na Kushukuru Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى):

 

Zinajumuisha neema za Dini na za kidunia. Elezea yaani, mhimidi na msifie Allaah kwazo kwa kuzitaja makhsusi ikiwa kuna faida kufanya hivyo. Vinginevyo, elezea Neema za Allaah kwa ujumla, kwani kwa kuzielezea huko, kunamfanya mtu kuendelea kushukuru zaidi, lakini pia kunazisukuma nyoyo kumpenda zaidi Allaah Mneemeshaji, kwani kawaida ya maumbile ya nyoyo za binaadam ni kumpenda yule anayezifadhili na kuzitendea wema. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Na hakika Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) ni nyingi mno wala hawezi mtu kuzitafakari zote na kuzihesabu kama Anavosema:

 

وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ   ﴿٣٤﴾

Na Akakupeni kila mlichomuomba. Na mkihesabu Neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni. [Ibraahiym (14:34)]

 

Rejea Suwrah hiyo ya Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah za mbinguni, ardhini, nafsini na kadhaalika pamoja na faida nyenginezo na rejea mbalimbali.  

 

Na bonyeza viungo vifuatavyo kupata duaa za kukiri na kushukuru Neema za Allaah (عزّ وجلّ), kuomba kutokutoweka neema hizo na kuomba kuzidishiwa:

 

024-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kusaidiwa Kumdhukuru Na Kumshukuru Allaah Na Kumwabudu Vizuri

 

 

030-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kusaidiwa, Kunusuriwa, Kupangiwa, Kumshukuru Na Kumdhukuru Allaah

 

 

038-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kukunjuliwa Baraka, Rahmah, Fadhila, Rizki, Neema Ya Kudumu...

 

 

30-Du’aa Toka Kwenye Qur-aan Tukufu Na Sharh Yake: Kuzinduliwa Kuzihisi Na Kuzishukuru Neema

 

 

 

Share