01-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Maana Ya Dhulma Na Shirki

   

 إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

01- Maana Ya Dhulma Na Shirki

 

Alhidaaya.com

 

Maana ya dhulma ni kuweka kitu mahali pasipo pake. Hivyo anayeabudu au kumwomba asiyekuwa Allaah atakuwa ameilekeza ‘ibaadah yake kwa asiyestahiki.

 

Maana ya shirki ni kumwekea Allaah mshirika katika Ar-Rubuwbiyyah (Uola) Wake au Uluwhiyyah (‘Ibaadah) Yake au Asmaa na Swifaat Zake.

 

عَنْ عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: لَمَّا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ، شَقَّ ذَلِكَ عَلَى النَّاس وَقَالُوا: أَيُّنَا لَمْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ؟! فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إنَّه لَيْسَ كَمَا تَعنُون! ألَمْ تَسْمَعوا ما قال الْعبْد الصَّالح؟  يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌإنَّما هُو الشِّرْك))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Ilipoteremshwa Aayah hii: Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; [An-An’aam: 82] Iliwatatiza watu  wakasema: “Nani katika sisi hajadhulumu nafsi yake?” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Si kama vile mnavyomaanisha! Hamsikii pale mja mwema aliposema:  “Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno!” [Luqmaan: 13] Hakika hiyo ni shirk.)) [Ahmad na riwaayah zinazofanana katika Al-Bukhaariy na wengineo]

 

 Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema: “Hakika kila Alichokikataza Allaah kinarejea katika dhulma na kila Alichokiamrisha kinarejea katika uadilifu, na ndio maana Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Anasema:

لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ

Kwa yakini Tuliwapeleka Rusuli Wetu kwa hoja bayana, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na Miyzaan (shariy’ah) ili watu wasimamie kwa uadilifu. [Al-Hadiyd: 25]

 

Akajulisha kwamba Ametuma Rasuli na Ameteremsha Kitabu na shariy’ah kwa ajili ya watu wasimamie uadilifu”  [Majmuw’ Al-Fataawa li Ibn Taymiyyah (18/157)]

 

Kumshirikisha Allaah aghlabu ni katika Uluwhiyyah Yake kwa kumwomba asiyekuwa Allaah, au kuelekeza aina yoyote ya ‘ibaadah kwa asiyekuwa Allaah kama kuchinja, kuweka nadhiri, kuapa, kukhofu na kutaraji, kutawakkal, istighaathah (kuomba uokozi au kinga) au kujikurubisha na yeyote au chochote kile kisichokuwa Allaah.

 

Vile vile kumlinganisha Allaah na viumbe. Anasema Allaah:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾

Enyi watu! Mwabuduni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

 

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua. [Al-Baqarah: 21-22]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 وَجَعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلُّوا عَن سَبِيلِهِ

Na wakamfanyia Allaah walinganishi ili wapoteze (watu) na njia Yake. [Ibraahiym: 30]

 

Na Anasema pia (سبحانه وتعالى):

قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٩﴾

Sema: “Je, hivi nyinyi mnamkufuru Yule Aliyeumba ardhi kwa siku mbili, na mnamfanyia waliolingana Naye? Huyo Ndiye Rabb wa walimwengu.” [Fusw-Swilat: 9]

 

 

Share