Al-Lajnah Ad-Daaimah: Hukmu Ya Kujenga Jengo La Sinema (Thieta) Au Kuendesha Kazi Zake
Hukmu Ya Kujenga Jengo La Sinema (Thieta ) Au Kuendesha Kazi Zake
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Muislamu anaruhusiwa kujenga jengo la sinema au kuendesha kazi zake humo?
JIBU:
Muislamu haruhusiwi kujenga jengo la sinema (thieta) au kuendesha kazi zake kwa ajili ya nafsi yake wala kwa ajili ya mtu mwengine kwa sababu ya burudani zilizo haramishwa humo. Kama inavyojulikana siku hizi duniani, zinaonyeshwa filamu chafu na picha za wasichana ambazo zinachochea uchu na zinashajiisha uasharati na uharibifu wa akhlaaq. Juu kuna michanganyiko ya wanawake na wanaume ambao si mahaarim zao. (walioharamishwa kuwaoa)
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa, mj. 26, uk. 277, (3501)]