Saladi Ya Kabeji Na Pilipili Mboga (Hoho) Na Karoti
Saladi Ya Kabeji Na Pilipili Mboga (Hoho) Na Karoti
Vipimo na Namna ya Kutayarisha
Kabeji likatekate jembamba -- ½ (Nusu) size ya kiasi
Karoti ikate kate - 2
Pilipili mboga la kijani (capsicum) - 2
Nyanya/tungule - 2 katakata
Sosi Ya saladi
Siki ya Tufaha (apple cider vinegar) - 1 vijiko vya supu
Mafuta ya halizeti (olive oil) - 3 vijiko vya supu
Chumvi – Kiasi
Pilipili nyekundu ya unga - ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya vitu vyote katika bakuli
2. Wakati wa kula, tia sosi (dressing)
Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kufurahika)