Shaykh Swaalih Aali Ash-Shaykh - Kusoma Alama Za Nyota
Kusoma Alama Za Nyota
Shaykh Swaalih Aali Ash-Shaykh (Hafidhwahu Allaah) amesema:
“Yeyote anayesoma ukurasa (kwenye magazeti, majarida, mitandao) wenye kuweka alama za nyota, na akawa anafuatilia (anajua) ni ipi alama ya nyota ya wakati aliozaliwa, au anajua nyota ambayo ni maalum kwake, na kisha akawa anasoma maelezo yaliyowekwa kwenye alama ya nyota hiyo, basi ni sawa na aliyemwendea mpiga ramli au mtabiri (akamtaka amtabirie au amwangalizie). (Basi, mtu huyo) haikubaliwi Swalaah yake kwa siku arobaini.
Na ikiwa atayasadikisha hayo yaliyoelezwa kwenye hiyo alama ya nyota na akayaamini, basi atakuwa amekufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Na ikiwa atalipeleka nyumbani kwake gazeti hilo (lenye hizo alama za nyota), basi ni sawa kampeleka mpiga ramli au mtabiri nyumbani kwake.”
[Tamhiyd Sharh Kitaab At-Tawhiyd, uk. 349]