Imaam Ibn Baaz: Sababu Zinazopelekea Katika Kujipamba Na Akhlaaq Za Kiislam
Sababu Zinazopelekea Katika Kujipamba Na Akhlaaq Za Kiislamu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Tunaomba kwa ukarimu wenu mtutajie baadhi ya sababu zitakazopelekea kupambika na akhlaaq (tabia) za Kiislamu
JIBU:
Yatakayopeleka katika hilo, ni kukithirisha kusoma Qur-aan na kuzingatia maana zake, na kujitahidi katika kujitengeneza kwa yale Aliyoyataja Allaah katika Qur-aan Kariym katika zile sifa za waja wema miongoni mwa Swaalihiyna, basi hayo ndiyo ambayo yatasaidia katika kujitengeneza kwa akhlaaq njema.
Na pia kuwa katika vikao vya waja wema na kusuhubiana nao, na kusoma Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zinazoongoza hayo.
Vile vile kuzingatia khabari za waliopita katika Siyrah ya Nabiy na katika historia ya Kiislamu kuhusu waja wema, haya yote yanasaidia katika akhlaaq njema na kuthibitika nazo.
Na kubwa zaidi ya hayo ni Qur-aan kwa kukithirisha kuisoma na kuzingatia maana zake kwa moyo uliohudhuria na raghba (shauku) ya kweli. Hii ndio kubwa kabisa litakalosaidia pamoja na kuchunga yaliyokuja katika Sunnah Swahiyh za Nabiyy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika hayo.
Na Allaah ni Mwenye Kuleta Tawfiyq
[Al-Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Al-Imaam Ibn Baaz]