Imaam Ibn Baaz: Hakuna Dalili Ya Kunyanyua Mikono Baada Ya Swalaah Za Faradhi

Hakuna Dalili Ya Kunyanyua Mikono BaadaYa Swalaah Za Faradhi

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Amesema Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah):

 

“Haijasihi kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba yeye alikuwa akinyanyua mikono yake baada ya Swalaah ya Faradhi.

 

Wala haijasihi (haijathibiti) hilo kwa Maswahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum), kwa tunavyofahamu.

 

Na wanayofanya baadhi ya watu katika kunyanyua mikono yao baada ya Swalaah ya Faradhi, ni bid’ah; haina asili.

 

 

[Al-Fataawaa Lil-Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaahu Ta’aalaa, mj. 1, uk. 74]

 

 

Share