Imaam Ibn Baaz: Anayetukana Dini Au Kufanya Istihzai Anakuwa Kafiri
Anayetukana Dini Au Kufanya Istihzai Anakuwa Kafiri
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
“Anayetukana Dini (Uislamu) au kufanya istihzai katika mas-ala ya Dini, anakuwa ni kafiri kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ﴿٦٥﴾ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ ۚ إِن نَّعْفُ عَن طَائِفَةٍ مِّنكُمْ نُعَذِّبْ طَائِفَةً بِأَنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ﴿٦٦﴾
Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake? Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu. [At-Tawbah: 65-66)
[Shariytw Hukmu Man Lam Yukaffir Al-Kaafir]