Imaam Ibn Baaz: Kubusu Mkono Au Kuweka Mkono Kifuani Baada Ya Kuamkiana
Kubusu Mkono Au Kuweka Mkono Kifuani Baada Ya Kuamkiana
Imaam Bin Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Naona baadhi ya watu baada ya kupeana mikono kuamkiana wanabusu mikono yao au wanaweka mkono kifuani kudhihirisha mapezi zaidi. Je, inahurusiwa? Tunufaishe Jazaaka Allaahu khayraa.
JIBU:
Tunavyojua, kitendo hicho hakina asili katika Shariy’ah ya Kiislam na haikuamuriwa kubusu mkono au kuweka kifuani baada ya kupeana mikono katika kuamkiana, bali ni bid’ah ikiwa anaamini kuwa kufanya hivyo kunamkurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).
[Imaam bin Baaz, Bid’ah Wa Muhdathaat Wa Maa Laa Aswla Lahaa (Uk. 477)]