Imaam Al-Hasan Al-Baswriy - Kusengenya Kuna Sura Tatu
Kusengenya Kuna Sura Tatu
Imaam Al-Hasan Al-Baswriy (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ghiybah (kusengenya) kuna sura tatu tofauti, zote ziko katika Kitabu cha Allaah Aliyetukuka:
1. Al-Ghiybah: Ni kumsema ndugu yako kwa kile alichonacho.
2. Al-Ifk: Kumsema ndugu yako kwa kile ulichofikishiwa (uvumi) chenye kumhusu.
3. Al-Buhtaan: Kumsema ndugu yako kwa lile asilo nalo (kumzulia).
[Tafsiyr Atw-Twabariy, mj. 16, uk. 335]
