Mboga Mchanganyiko Ya Kukaanga Na Uyoga Kwa Sosi ya Soya
Mboga Mchanganyiko Ya Kukaanga Na Uyoga Kwa Sosi ya Soya
Vipimo
Bakuli la kwanza:
Kitunguu kilokatwakatwa slesi - 1
Tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha kulia
Thomu (garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha kulia
Karoti ilokatwa slesi nyembamba - 1
Uyoga (mushrooms) katakata vipande vipande - 1 kikombe
Koliflawa (cauliflower) katakata - ¼ ya uwa moja
Bakuli la pili:
Njegere za kijani (green peas) - 1 kikombe
Maharage ya kijani - 1 kikombe kimoja
Brokoli (broccoli) katakata vipande - ½ ya uwa moja
Figili mwitu (celery) katakata - 1 mche
Vinginevyo:
Sosi ya soya (soy sauce) - 3 vijiko vya kulia
Sukari - 1 kijiko cha chai
Unga wa mahindi mlaini (Corn starch) - 1 kijiko cha chai
Kidonge cha supu - 1
Mafuta - 3 vijiko cha kulia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka karai la kukaangia mboga (Wok) katika moto, tia mafuta yashike moto.
- Mimina vitu katika bakuli la kwanza, ukaange na ukoroge katika moto wa kiasi mpaka mboga zake humo ziive nusu yake. (kiasi dakika 3)
- Weka sosi ya soya, sukari, kidonge cha supu changanya vizuri ibakie motoni kiasi dakika moja
- Mimina vitu vya bakuli la pili na korogoa. Acha vipikike kiasi dakika 2.
- Katika kibakuli kidogo, weka cornstarch utie maji kiasi kijiko kimoja cha kulia uchagane vizuri. Tia katika mboga. Zima moto, kisha pakua katika sahani utie juu yake vitunguu vya majani (springi onions) au chives (aina ya vitunguu kama spring onions) au dill (aina ya kotmiri mwitu)
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)