002-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: ILAAH

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

إله

002-ILAAH

 

 

 

ILAAH:   Muabudiwa wa haki.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾

Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi Niabuduni.” [Al-Anbiyaa 21: 25]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

“Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.” [Al-Baqarah: 2: 163]

 

Ilaah ni mwenye kustahiki kuabudiwa na Mwenye kuabudiwa kwa mapenzi, kwa kujidhalilisha Kwake, kwa kumkhofu, kwa kutaraji, kwa kumtukuza kwa utiifu kwa sababu Yeye Ndiye Anayeabudiwa.

 

Hivyo kila chenye kuabudiwa chini ya ‘Arshi Yake hadi ardhini ni batili; Amesema Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “Laa Ilaaha Illa Anta” (Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe) ndani yake kuna kuthibitisha upweke Wake, Uungu Wake, na Uungu unathibitisha wema Wake kwa waja Wake. Ilaah Ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa, na kwa sababu Anastahiki kuabudiwa, Yeye ni kama Alivyojisifu kwa Sifa Zake ambazo zinalazimu apendwe mapenzi yote, kilele cha mapenzi, na kunyenyekewa Kwake kilele cha kumnyenyekea, na ‘ibaadah inakusanya kilele cha mapenzi, kwa lengo la kunyenyekewa. [Daqaaiq At-Tafsyir (2/364)]

 

Na jina la Ilaah linatofautiana maana yake na Ar-Rabb katika maeneo mengi, miongoni mwazo ni: Kuwa Ar-Rabb maana yake inarejea kwenye kupwekeka katika kuumba na uendeshaji. Ama Ilaah, Ambaye Anastahiki kuabudiwa na ambaye nyoyo zinamtukuza na wananyenyekea Kwake kwa mapenzi na kumtukuza, Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa kila aina zake na kuenea kwake.

 

Ama tofauti kati ya Allaah na Ilaah ni kuwa Ilaah ni wasifu ambao washirikina walimshirikisha kwao Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kuabudu miongoni mwao;  jua, mwezi na sayari, na hawakufanya hivyo kwa kutumia jina la Allaah, na hawakujiita kwayo yeyote. [Al-Asmaa ya Al-Qurtubiy (uk. 368)]

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

فَلَوْلَا نَصَرَهُمُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ قُرْبَانًا آلِهَةً ۖ بَلْ ضَلُّوا عَنْهُمْ ۚ وَذَٰلِكَ إِفْكُهُمْ وَمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٨﴾

Basi kwa nini wasiwanusuru wale waliowafanya badala ya Allaah kuwa ni miungu ya kikurubisho (Kwake)? Bali wamewapotea, na huo ndio uongo wao na yale waliyokuwa wakiyatunga [Al-Ahqaaf 46 :28]

 

 

 

 

 

Share