Kukosa Rakaa Moja Katika Swalaah Ya Jamaa

Kukosa Rakaa Moja Katika Swalaah Ya Jamaa

SWALI:

UNATAKIWA UFANYE NINI PINDI UNAPOTOA SALAMU KATIKA SWALA EITHER YA RAKAA 4 KAMA ADHUHURI ,ILHAL ULICHELEWA NA UNADAIWA RAKAA MOJA?

 


JIBU:

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 
 Unapokosa rakaa moja au zaidi katika Swalaah ya Jamaa’ah hutakiwi kutoa salaam pale Imaam anapomaliza Swalaah, bali unatakiwa wewe usimame kutekeleza rakaa ulizozikosa ikiwa ni moja au mbili au tatu. Rakaa ulizoswali na Imaam zitahesabika kwako kuwa ni rakaa za mwanzo na hizo utakazokamilisha ndio zinazofuatia. Utamalizia na tashahhud na kutoa salaam.

 

Hali hii ya kukosa rakaa na kulipiza rakaa inaitwa Swalaatul-Masbuqw (Swalaah ya aliyetanguliwa au aliyechelewa rakaa na Imaam)

Na Allaah Anajua zaidi

Share