Kudhihirisha BismiLLaah Kwa Sauti Katika Baadhi Ya Misikiti

Kudhihirisha BismiLLaah Kwa Sauti Katika Baadhi Ya Misikiti

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

السلام عليكم....

Ndugu ktk iiman kuna jambo naomba ushauri ktk dini. Huku kwetu misikiti mingi ni ya makhurafi na huwa wanasomà "bismillaahi" ktk suurat fatiha ktk swala,... Na sisi huwa hatusomi bismillah ktk swala.

Na wengi ktk wao ni watu wa bidaa na wajinga.... Ña wamesema mtu asiyesoma bismillah ktk swala hatuswalishi. Hivyo yafaa kusoma bismillah ili wasiswalishe majaahil  ili kunusuru ibada ya swala??

Naomba hili swali lifike kwa shekh rabii au shekh khamiys au yeyote ktk mashekh.

 

بارك الله فيكم

 

 

JIBU:

 

Wa 'Alaykumus Salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh

 

Ilivyo katika Sunnah ni kutosoma Basmalah (BismiLLaahir Rahmaanir Rahiym) katika Suwratul-Faatihah kwenye Swalaah kwa sauti.

 

Hata hivyo, Wanachuoni wanaona baadhi ya nyakati Imaam anaweza kudhihirisha kwa sauti kama ambavyo wanasema kuwa baadhi ya nyakati Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo ingawa muda mwingi alikuwa hadhihirishi.

 

Na wanaona kuwa, kukiwa na maslahi fulani kama kufundisha watu au kuunganisha nyoyo za watu na kuleta umoja, basi Imaam anaweza kusoma kwa sauti.

 

 

Anasema Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

 

"... hata hivyo,  mtazamo sahihi ni kuwa (Basmalah) haisomwi kwa sauti, japokuwa inakubalika kusoma kwa sauti ikiwa itakidhi maslahi muhimu.

 

Hivyo, inajuzu Imaam kufanya hivyo -baadhi ya nyakati- kwa mfano, kufundisha watu wanaoswali nyuma yake. Inaruhusika kwa Mswaliji kusoma maneno machache kwa sauti ndani ya Swalaah baadhi ya nyakati, na inaruhusika kwa mtu kuacha linalopendeza kwa ajili ya kuunganisha nyoyo (za Waumini) na kuleta umoja na kukhofia kukimbiza watu katika lenye maslaha.

 

Mfano, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliacha kujenga upya Al-Ka'bah kwa ule msingi wa Ibraahiym ('Alayhis Salaam) kwa sababu Maquraysh walikuwa ndio mwanzo wametoka kwenye Jaahiliyyah (bado wageni katika Uislamu), na akakhofia kuwa wanaweza kukimbizwa na hilo. Akaonelea maslaha ya kuwakusanya pamoja na kuwaunganisha kuwa mbele kuliko juu ya yale ya kuijenga Al-Ka'bah kwa misingi yake ya asli ya Ibraahiym ('Alayhis Salaam).

 

 

Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema, alipomaliza Swalaah (wakati wa Hajj kwa kuswali rakaa nne badala ya mbili kama ilivyoswaliwa wakati wa Rasuli) nyuma ya 'Uthmaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) hali ya kuwa hakupendezewa na alilipinga hilo, akaulizwa kuhusu hilo (la kuswali rakaa nne ilhali hawafikiani nalo)? Akajibu: "Khilafu ni shari."

 

Na kwa hivyo, Maimaam kama Ahmad na wengine, wameeleza kama hayo kuhusiana na suala la Basmalah, kuswali Witr kwa kuunganisha rakaa tatu pamoja, na masuala mengine ambayo mtu anaweza kuacha yale yenye kupendeza kwa kuleta yale ambayo yataleta maslaha na kuunganisha watu pamoja au pia kwa ajili ya kuwafundisha watu Sunnah na mengine mfano wa hayo."

 

Mwisho wa kumnukuu Shaykh Al-Islaam.

 

[Majmuw' Al-Fataawa, mj. 22, uk. 436, 437]

 

 

Na akasema tena Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

 

"Kuacha kile kinachopendeza (kilicho bora) kwa kutowakimbiza watu. Kadhaalika, ikiwa mtu anayeona ni sahihi kusoma Basmalah kwa sauti, akaswalisha watu ambao hawakubaliani na kusoma Basmalah kwa sauti, akawafikiana nao na kuacha kusoma Basmalah kwa sauti (japo huo ndio msimamo wake, kwa lengo la kutoleta mvutano na mgawanyiko), na vilevile kinyume chake. Kwa hali hiyo atakuwa amefanya uzuri.

 

[Majmuw' Al-Fataawa, mj. 22, uk. 268, 269]

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) aliulizwa?

 

Ni nini hukmu ya kusoma Basmalah kwa sauti?

 

Akajibu:

 

"Rai iliyo sahihi zaidi ni kuwa Basmalah haiapaswi kusomwa kwa sauti, na ni Sunnah kuisoma kwa ukimya, kwa sababu si sehemu (si aayah) ya Suwratul-Faatihah.

 

Lakini ikiwa itasomwa kwa sauti baadhi ya nyakati, hakuna ubaya.

 

Bali hata baadhi ya Wanachuoni wanaonelea kuisoma kwa sauti baadhi ya nyakati kwa sababu limepokelewa kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alikuwa akisoma kwa sauti.

Lakini iliyothibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hasomi kwa sauti. Na hili ndio bora; kutosoma kwa sauti.

 

Lakini ikiwa (mtu, Imaam) atasoma kwa sauti kwa lengo la kuunganisha watu ambao madh-hab yao ni kusoma (Basmalah) kwa sauti, basi nataraji kuwa hakuna ubaya."

 

[Majmuw' Fataawa Ash-Shaykh Al-'Uthaymiyn, mj. 13, uk. 109]

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share