008-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: ASW-SWAMADU
أسماء الله الحسنى وصفاته
Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake
الصَّمَدُ
008 - ASW-SWAMADU
ASW-SWAMADU: Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote.
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimsikia mtu akiomba katika du’aa yake:
اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أحَدٌ، فقال: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ وَإذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى))
“Allaahumma inni as-aluka bianniy ash-hadu Annaka Anta-Allaahu laa ilaaha illa Anta Al-Ahadu Asw-Swamadu, Alladhiy lam Yalid walam Yuwlad walam Yakun Lahuu kufuwan ahad”.
Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa kushuhudia kwamba hakika Wewe ni Allaah, hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Mmoja, Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, Ambaye Hakuzaa na wala Hakuzaliwa, Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”
Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, kwa yakini Ameomba kwa Jina Lake Tukufu kabisa ambalo Anapoombwa kwalo [du’aa] Anaitikia na Anapotakwa kwalo [jambo] Hutoa)) [Hadiyth ya Buraydah bin Al-Haswiyb Al-Aslamiyy kutoka kwa baba yake Radhwiya Allaahu ‘anhumaa – Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb (1640)]
Asw-Swamadu; As-Sayyid (Bwana) Aliyekamilika kwa ubwana Wake na Aliyekamilika katika aina zote za ubwana na utukufu mbinguni na ardhini. Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَلَهُ الْكِبْرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ
Na Adhama, Utukufu, Ujalali ni Wake Pekee mbinguni na ardhini. [Al-Jaathiyah: 37]
Asw-Swamadu: Ni Yeye Allaah (‘Azza wa Jalla) Mwenye sifa hii, ambayo haimstahiki yeyote asiyekuwa Yeye. Yeye Ndiye Anayekusudiwa na viumbe Wake wote; wana Aadam na majini, ulimwengu wa juu na wa chini, ni Yeye tu wa kukusudiwa.
Hakuzaa wala hakuzaliwa, hafi wala harithiwi, kwa sababu si anayezaliwa ili afe, wala hafi ili arithiwe. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee.
اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾
“Allaah ni Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote.
لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾
“Hakuzaa na wala Hakuzaliwa.
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾
“Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.” [Al-Ikhlaasw]
Na katika Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((قَالَ اللَّهُ كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ ، وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ ، فَأَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّايَ، فَقَوْلُهُ لَنْ يُعِيدَنِي كَمَا بَدَأَنِي وَلَيْسَ أَوَّلُ الْخَلْقِ بِأَهْوَنَ عَلَيَّ مِنْ إِعَادَتِه،ِ وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا وَأَنَا الْأَحَدُ الصَّمَدُ لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفْئًا أَحَدٌ)) البخاري والنسائ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Amesema: Bin Aadam amenikadhibisha na hana haki ya kufanya hivyo, na amenitukana na hana haki ya kufanya hivyo. Ama kunikadhibisha kwake ni kusema: Hatonirejesha (tena) kama Alivyoniumba (Hatonifufua kama vile Alivyoniumba). Na kuumba hakukuwa rahisi Kwangu kuliko kumfufua. Ama kunitukana kwake ni kule kusema: Allaah Ana mtoto wakati Mimi ni Ahad (Mmoja Pekee), Asw-Swamad (Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote), Sikuzaa wala Sikuzaliwa na hakuna chochote kinachofanana na kulingana Nami)) [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy]
Na Suwrah hiyo ya Al-Ikhlaasw ni Suwrah ambayo thawabu zake katika kuisoma ni sawasawa na thawabu za kusoma thuluthi ya Qur-aan kwa dalili zifuatazo:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لأَصْحَابِهِ: ((أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَقْرَأَ ثُلُثَ الْقُرْآنِ فِي لَيْلَةٍ؟)) فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَيْهِمْ وَقَالُوا: أَيُّنَا يُطِيقُ ذَلِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ فَقَالَ: ((اللَّهُ الْوَاحِدُ الصَّمَدُ ثُلُثُ الْقُرْآنِ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewaambia Maswahaba wake: ((Je, anaweza mmoja wenu asome thuluthi ya Qur-aan katika usiku mmoja?)) Likawa jambo gumu kwao wakasema: Tuwezeje sisi kufanya hivyo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Allaah, Al-Waahidu (Mmoja Pekee, Asw-Swamadu (Mkusudiwa wa yote) ni thuluthi ya Qur-aan)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ أَنَّ رَجُلًا سَمِعَ رَجُلًا يَقْرَأُ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ يُرَدِّدُهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ ، وَكَأَنَّ الرَّجُلَ يَتَقَالُّهَا أي يراها قليلة فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ الْقُرْآن))
Pia imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyyi (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mtu mmoja alimsikia mtu akisoma Qul-Huwa-Allaahu Ahad na akiikariri. Asubuhi yake akamwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamtajia hilo na alidhania kuwa ni kisomo kidogo tu. Lakini Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hiyo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan)) [Al-Bukhaariy (6643)]
Asw-Swamadu; Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni As-Sayyid Anayetiiwa; amri zake zinatekelezwa katika ardhi yake na mbingu yake, haipitishwi amri isipokuwa kwa idhini Yake. Yeye (‘Azza wa Jalla) ni Mwenye shani ya juu na uwezo. Yeye ni mwenye wasaa wa sifa na ukubwa ambao haukusaza sifa ya ukamilifu ila amesifika nayo, kwa upeo wake na ukamilifu wake.
Asw-Swamadu ni Ambaye Hali wala Halishwi. Anasema:
قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٤﴾
Sema: “Je, nimfanye mlinzi asiyekuwa Allaah; Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayelisha na wala halishwi?” [Al-An’aam: 14]
Asw-Swamadu Ambaye Hana mwisho abadan Atabakia daima baada ya kutoweka viumbe Vyake vyote.
Mambo yote yanaishia Kwake, wala haikidhiwi jambo bila Yeye. Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ
Sema: “Hakika amri yote ni ya Allaah.” [Aal-‘Imraan: 154]
وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٢٣﴾
Na ni ya Allaah (Pekee) ghayb ya mbingu na ardhi, na Kwake hurudishwa mambo yote; basi mwabudu Yeye na tawakali Kwake. Na Rabb wako si Mwenye kughafilika na yale myatendayo. [Huwd: 123]