Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hukmu Ya Kuswali Juu Ya Mazulia Yenye Picha Za Misikiti
Hukmu Ya Kuswali Juu Ya Mazulia Yenye Picha Za Misikiti
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya mazulia yenye picha za Misikiti je inafaa kuswalia?
JIBU:
Tunaloona ni kwamba haifai kumwekea Imaam Mazulia au Miswala yenye picha za Misikiti kwa sababu itamshughulisha kuitazama na hivyo itaathiri Swalaah yake. Na ndio maana Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akiswali akiwa amevaa joho lenye alama alama, akawa akitazama alama zake, basi alipomaliza alisema:
“Pelekeni joho langu hili kwa Abuu Jahm na nileteeni (badala yake) nileteeni nguo isiyo na kutoka kwa Abuu Jahm, kwani (hilo joho lenye alama alama) limenipotezea umakini wangu katika Swalah.” [Hadiyth ya mama ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa katika Al-Bukhaariy na Muslim].
Na ikiwa Imaam hatoshughulishwa labda kutokana na kuwa yeye ni kipofu, au hiyo ni kawaida kwake hata haimshughulishi, basi hatuoni kuwa kuna ubaya kuswalia.
Na Allaah Ndiye mwenye kuleta Tawfiyq.
[Majmuw' Fataawa Shaykh bin ‘Uthaymiyn (12/362)]