Al-Lajnah Ad-Daaimah: Majini Kujua Ghayb

Majini Kujua Ghayb

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, majini wanajua ghayb? Tunaomba mtubainishe haraka muwezavyo.

 

 

JIBU:

 

Elimu ya ghayb ni katika mambo makhsusi ya Ar-Rubuwbiyyah (Tawhiyd ya Uola). Kwa hivyo hakuna mwenye kujua ghayb za mbingu wala ardhi isipokuwa Allaah.

Anasema Allaah (Ta'aalaa):

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ

Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu [Al-An’aam 6:59]

 

Na Anasema (Jalla Jalaaluhu):

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ

Sema: “Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. [An-Naml 27: 65]

 

Na majini hawajui ghayb na dalili ni kauli ya (Ta’alaa):

فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ الْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِ إِلَّا دَابَّةُ الْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنسَأَتَهُ ۖ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ ﴿١٤﴾

Basi Tulipomkidhia mauti, hakuna kilichowajulisha kifo chake isipokuwa mdudu wa ardhi akila fimbo yake. Basi alipoanguka ikawabainika majini kwamba lau wangelikuwa wanajua ya ghayb, basi wasingebakia katika adhabu ya kudhalilisha. [Sabaa 34: 14]

 

Na anayedai kuwa anajua ghayb basi yeye ni kafiri.

Na anayemsadiki mwenye kudai kuwa anajua ghayb, naye ni kafiri pia kwa sababu wanakanusha Qur-aan.

 

Wa bi-LLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah - Fatwa (18645)]

 

Share