Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kufuga Kucha Ni Kinyume Na Sunnah Ya Fitwrah

 

Kufuga Kucha Ni Kinyume Na Sunnah Ya Fitwrah

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya kufuga kucha?

 

 

JIBU:

 

Haijuzu kufuga kucha kwa sababu hivyo ni kinyume na Sunnah ya Fitwrah ambayo ameihimiza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tuitekeleze.

 

Kukata kucha ni mojawapo ya Sunnah ya Fitwrah pamoja na kunyofoa nywele kwapani na kunyoa nywele za sehemu za siri na kupunguza masharubu.

 

Na haya yanapaswa kufanywa (wakati wowote zinapokua) isipite zaidi ya siku arubaini kutokana na Hadiyth iliyosimuliwa na Muslim katika Swahiyh yake, imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba:

 

وُقِّتَ لَنَا فِي قَصِّ الشَّارِبِ، وَتَقْلِيمِ الأَظْفَارِ، وَنَتْفِ الإِبِطِ، وَحَلْقِ الْعَانَةِ، أَنْ لاَ نَتْرُكَ أَكْثَرَ مِنْ أَرْبَعِينَ يَوْماً

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alituwekea muda wa kukata masharubu, kukata kucha, kunyoa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za sehemu za siri kuwa tusiziache zaidi ya siku arubaini.”

 

Basi inawapasa wanawake (wenye tabia ya kufuga kucha ndefu) watubie kwa Allaah na waache ada hii ovu ya kukhalifu aliyoyaamrisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ

Na lolote analokupeni Rasuli (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم basi lichukueni, na analokukatazeni, basi achene [Al-Hashr 59: 7]

 

Na Anasema Subhaanahu:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾

Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo. [An-Nuwr 24: 63]

 

Wa bi-LLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah - Fatwa (19771)]

 

 

Share