Al-Lajnah Ad-Daaimah: Mwanamke Anayefariki Wakati Wa Kuzaa Anazingatiwa ni Shahidi

 

Mwanamke Anayefariki Wakati Wa Kuzaa Anazingatiwa ni Shahidi

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, ni kweli kuwa mwanamke ambaye amekufa wakati wa kujifungua anazingatiwa ni Shahidi?

 

 

JIBU:

 

Mwanamke yeyote ambaye atakufa wakati wa kujifungua au wakati wa ujauzito ni Shahidi in shaa Allaah. Katika Hadiyth iliyosimuliwa na 'Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ni yupi ambaye anahisabika ni Shahidi miongoni mwenu?" Maswahaba wakasema: Ni yule anayepigana na akauawa katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Shahidi miongoni mwa Ummah wangu (Ummah wenye msingi wa 'Aqiydah moja) watakuwa wachache. Ambaye ameuliwa kwa sababu ya (kuinua utajo wa) Allaah ni Shahidi; ambaye amekufa kwa ugonjwa wa tauni ni Shahidi, ambaye amekufa kwa maradhi ya tumbo ni Shahidi, na ambaye amekufa wakati wa ujauzito ni Shahidi. [Ahmad, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan na wengineo].

 

 

Kwa hivyo, mwanamke ambaye amekufa wakati wa ujauzito ni Shahidi.

 

 

Imepokelewa kwa mapokezi mengine yaliyosimuliwa na Rashid bin Hubaysh (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa 'Ubaadah bin Swaamit wakati alipokuwa mgonjwa na akasema: "Je, unajua ni yupi Shahidi katika Ummah wangu?" Watu wakawa kimya. 'Ubaadah akasema: Nisaidieni nikae. Wakamsaidia kumuweka juu. Kisha akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, ni mtu mgonjwa ambaye anataraji thawabu kwa Allaah kwa subira? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Shahidi miongoni mwa Ummah wangu watakuwa wachache. Kufa kwa ajili ya (Dini) ya Allaah ni ushahidi, kufa kwa ugonjwa wa tauni ni ushahidi; kuzama (kwenye maji) ni ushahidi, kufa na magonjwa tumbo ni ushahidi, na ikiwa mwanamke atakufa wakati wa kujifungua basi mtoto wake atamvuta kwa kamba ya kitovu hadi Jannah (Peponi). [Ahmad katika Musnad, Abuu Daawuwd katika Sunnan].

 

Na katika mapokezi mengine yanayofanana kutoka kwa Imaam Muslim katika Kitaab Al-Imaarah, ml. 51, mj. 3, uk. 1521.

 

 

Kuna ushahidi mwingi unaoonyesha thawabu kubwa kwa mwanamke ambaye amekufa wakati wa kujifungua au wakati wa ujauzito.

 

Na yeye ni mmoja miongoni mwa mashahidi katika Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

Hata hivyo, daraja ya juu kabisa ya shahidi ni ile ambayo mtu ameuliwa katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 

Allaah Atujaalie mema. Swalah na Salaam ziwe juu ya Rasuli Muhammad (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na familia yake, na Maswahana zake (Radhwiya Allaahu 'anhum).

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah, fatwa namba 20030]

 

 

Share