Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kuacha Swalaah Ya Jamaa’ah Kwa Sababu Ya Kuwaonea Watu Hayaa
Kuacha Swalaah Ya Jamaa’ah Kwa Sababu Ya Kuwaonea Watu Hayaa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Mimi husikia Adhana ya Alfajiri, lakini siendi kuswali, na sababu ni kuwa ninawaonea watu hayaa, nnadhania kuwa watanifanyia istihzaai waseme: “Eh, kijana ni mswalihina!” Na hunijia fikra ya kiajabu, basi huamka baada ya shuruwq (jua kuchomoza) na ndio huswali. Je hivi inajuzu au sio?
JIBU:
Ni waajib kwako kwenda Masjid unapoingia wakati wa Swalaah za fardhi ili kuswali jamaa’ah, wala isikuzuie lolote lile kufanya hivyo kwa sababu ya kuogopa istihzai za watu kwako au fikra zozote zile za kiajabu kwani hizo ni katika wasiwasi wa shaytwaan anataka kukuzuia na yaliyokuwa ni waajib kwako ya kuswali Jamaa’ah.
Na imekuwa ni haraam kwako kuakhirisha Swalaah za fardhi mpaka utoke wakati wake.
Wa biLLaahit-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (5378)]