Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kutayammam Kutokana Na Ihtilaam Kukhofia Baridi Ilhali Maji Yanapatikana

 

Kutayammam Kutokana Na Ihtilaam (Kutokwa Manii)

Kwa Kukhofia Baridi Ilhali Maji Yanapatikana

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Siku moja aliamka kabla Swalaah ya Alfajiri na alikuwa amepatwa na ihtilaam (ameota na kutokwa manii), na ilikuwa siku hiyo ni baridi kali mno. Akaenda shule akafanya tayammum akaswali, kisha akarudi nyumbani na njiani akataka kurudi afanye ghuslu (aoge kuondosha ile janaba) lakini hakufanya. Akaenda shule aliporudi Adhuhuri pia hakufanya ghuslu. Nini hukmu yake?  

 

 

JIBU:

 

Ama kuhusu yaliyotokea hayo, basi ni lazima arudie kuswali Swalaah mbili ambazo ameziswali bila ya kufanya ghuslu kwa ajili ya janaba kwa sababu alikuwa mjini na angeliweza kupata maji. 

 

Ama alipoamka akakhofia baridi, basi inaruhusiwa kufanya tayammum lakini kama angekuwa na uwezekano ya kupasha maji moto, basi ingewajibika kwake kufanya ghuslu. Na kama angekuwa safarini, na hakuwa na njia ya kupasha maji moto, angeruhusika kufanya tayammum na kusingekuwa na dhambi kwake. Lakini madamu alipata maji, basi ni lazima afanye ghuslu.

 

 

[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn, Fataawa Islaamiyyah (2/89)]

 

 

Share