Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Maamkizi Ya Kiislamu (Assalaam ‘Alaykum) Kwa Sauti Ndio Sunnah
Maamkizi Ya Kiislamu (Assalaam ‘Alaykum) Kwa Sauti Ndio Sunnah
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaahu) amesema:
“Katika adabu za kutoleana Salaam ni kunyanyua sauti wakati wa kusalimiana iwe ni kwa sauti ya wazi, na wala isiwe kwa sauti ya chini, kiasi kwamba hata anayesalimiwa hasikii. Basi na salimieni Salaam yenye kusikika, na iwe wazi, na hii ndio Sunnah.
[Mandhwumat Uswuwl Al-Fiqhi Wa-Qawaaidihi uk 187]