Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Haijuzu Kusema Al-Baaqiy ‘Ala-Allaah (Yaliyobaki Namuachia Allaah)
Haijuzu Kusema Al-Baaqiy ‘Ala-Allaah (Yaliyobaki Namuachia Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, ni Sahihi kusema ibara hii: “Nimetumia juhudi zangu zote, yaliyobaki namuachia Allaah?’’
JIBU:
Haya maneno hayafai, kwasababu huwa yanamaanisha kuwa mfanyaji alikuwa ameitegemea nafsi yake kwanza, baada ya kushindwa ndio akamuachia Allaah. Lakini kauli sahihi anatakiwa aseme: “Nimetumia juhudi zangu na ninaomba msaada wa Allaah.’’
[Fataawaa Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn – Mujallah Al-Hasbah Al-‘Adad (50) Uk. (17)]