Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwanamke Kupanda Gari Pamoja Na Shemeji

Mwanamke Kupanda Gari Pamoja Na Shemeji   

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Je, inajuzu mimi kupanda gari ya shemeji yangu (mume wa dada) anapokuja kunichukua kwa ajili ya kumtembelea dada yangu, hali ya kuwa shemeji yangu ananiulizia na kuongea nami; je, inaruhusika mimi kwenda naye?

 

 

JIBU:

 

Ikiwa kuna mtu mwengine pamoja nawe, kama dada yako, au mtu mwengine na kwa sharti kwamba shemeji yako ni mtu mwaminifu, basi hakuna ubaya (kupanda gari lake), lakini ikiwa ni pekee yake basi hivyo itakuwa ni kuwa faragha naye na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha mwanamme kuwa faragha na mwanamke asiyekuwa mahram wake.

 

 

[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (5811 11/249)]

 

 

Share