Sharh Hadiyth 14 An-Nawawiy: Damu Ya Muislam Haimwagiki Ila Kwa Mambo Matatu
Sharh Hadiyth 14 An-Nawawy
Damu Ya Muislam Haimwagiki Ila Kwa Mambo Matatu
الحديث الرابع عشر
" لا يحل دم امريء مسلم إلا بإحدى ثلاث"
Hadiyth Ya 14: Damu Ya Muislamu Isimwage Isipokuwa Kwa Sababu Tatu
عن ابْنِ مَسْعُودٍ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ: الثَّيِّبُ الزَّاني، وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ، وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ)). رَوَاهُ الْبُخَارِيّ وَمُسْلِمٌ
Kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye alisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Damu ya Muislamu haipasi kumwagwa isipokuwa katika hali tatu: Mzinzi Muolewa (Mtu mzima aliyeoa/olewa), uhai kwa uhai (nafsi kwa nafsi) na kwa yule anaeeacha dini na akajifarikisha na jama’ah (kundi) (amejitenga na watu wa dini yake”. [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth hii inaelezea umuhimu na hadhi ya maisha ya Muislam kama ilivyo katika Shariy’ah ya Kiislamu.
Kwa ujumla roho ya Muislam haitolewi ila ikiwa atatenda uhalifu unaoleta madhara katika jamii. Uhalifu huo uwe mbaya sana hadi umfanye kuwa hastahiki tena kuishi. Uhalifu huu umetajwa kwa ujumla katika Hadiyth hii.
Makafiri wasioamini Aakhirah huwa ni vigumu kwao kuifahamu hukmu hii ya Kiislam ya kuuawa. Uislam, kuuawa kuna maana kuwamba ni kumalizika kwa maisha ya kidunia, lakini huyo anayeuliwa huenda akalipwa Jannah (Pepo) hivyo awe na maisha bora zaidi kuliko ya duniani na Muislamu hutegemea hivyo. Na ndio maana wakati wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mwanamke alimuendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akakiri madhambi yake ya uzinifu na akauawa kwa kupigwa mawe.
Hadiyth hii inaelezea kidogo na kuambatana na maelezo ya Hadiyth Namba 8 ifuatayo ambayo maisha ya mtu huwa ni ya usalama katika haki ya Uislam.
الحديث الثامن
"أمرت أن أقاتل الناس"
Hadiyth Ya 8: Nimeamrishwa Nipigane Na Watu
عن ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أنَّ رسُوَل الله صلى الله عليه وسلم قال: ((أُمِرْتُ أَنْ أُقاتِلَ النَّاسَ حتَّى يَشْهَدُوا أنْ لا إلَهَ إلاَّ اللهُ وأنَّ محمداً رسوُل اللهِ، ويُقِيمُوا الصَّلاَةَ، ويُؤتُوا الزَّكاةَ، فإذا فَعَلوا ذَلِكَ عَصَموا منِّي دِماءَهُمْ وأمْوَالَهُمْ إلا بِحَقِّ الإِسْلامِ، وحِسابُهُم على اللهِ تعالى)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye alisema kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washahidie hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na mpaka watakaposwali, na wakatoa Zakaah, na wakifanya hivyo, watakuwa wamepata himaya kwangu ya damu yao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislam. Na hesabu yao itakuwa kwa Allaah Ta’aalaa”. [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Muislam lazima aheshimu maisha, mali na heshima ya Muislam mwenzake kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijjatul-Widaa' (Hijja ya ya mwago)
((أيها الناس ان دماءكم وأموالكم حرام عليكم الى أن تلقوا ربكم كحرمة يومكم هذا في شهركم هذا في بلدكم هذا, ألا هل بلّغت؟ اللهم فاشه
“Enyi Watu, damu zenu (kuua), mali zenu (kunyang’anya, kuiba) ni haraam kwenu hadi mtakapokutana na Rabb wenu…”
Maisha ya Muislam yana heshima mbele ya Allaah.
Ingawa Muislam anapaswa kuheshimika kama ilivyo katika Shariy’ah, lakini kwa hali nyingine, huenda akafanya kitendo kiovu hadi kikamfanya kuwa hastahiki tena kuishi.
Hali Tatu Zilizotajwa Zinazostahiki Kuuliwa Muislamu
1- الثَّيِّبُ الزَّاني
At-ThayyibAz-Zaaniy
Mzinzi Muolewa (Mtu mzima Aliyeoa/Olewa)
Mzinifu ni mwenye kutenda zinaa yaani kutenda kitendo cha ndoa cha haraam. Adhabu yake ni kama ifuatayo:
-Mzinifu aliyeoa au kuolewa – kupigwa mawe hadi afariki.
-Asiyeoa au kuolewa – kupigwa mijeledi (bakora) 100 hadharani kisha mwanaume ahamishwe nje ya mji kwa muda wa mwaka mmoja.
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametuwekea njia ya halaal ya kutimiza matamanio ya kinafsi na kujitosheleza, nayo ni ndoa. Kisha pia Ameonya kuwa Muislam asikaribie kabisa zinaa, na Ametuwekea njia mbali mbali za kumhifadhi mtu asifikie kuingia katika kitendo hicho, njia hizo ni:
i-Hijaab
ii-Kutokuchanganyika wanawake na wanaume. Na kutokaa mwanamke faragha na mwanamume wasio maharimu.
Ametuonya tusikaribie kabisa zinaa Anaposema:
وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٣٢﴾
Na wala msiikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya kabisa. [Al-Israa: 32]
Pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametupa sifa za Waja Wa Ar-Rahmaan ambao ni wale wasiofanya uovu huu pamoja na nukta ya pili ya kuua.
وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٦٦﴾وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا ﴿٦٧﴾وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَامًا ﴿٧٢﴾ وَالَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا ﴿٧٣﴾ وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾ أُولَـٰئِكَ يُجْزَوْنَ الْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً وَسَلَامًا ﴿٧٥﴾ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٧٦﴾
Na waja wa Ar-Rahmaan ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaam! Na wale wanaokesha usiku kwa ajili ya Rabb wao wakisujudu na kusimama. Na wale wanaosema: Rabb wetu! Tuepushe adhabu ya Jahannam. Hakika adhabu yake ni yenye kugandamana daima; isiyomwacha mtu. Hakika hiyo (Jahannam) ni mahali paovu mno pa kustakiri na mahali pa kuishi. Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo. Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu. Ataongezewa adhabu maradufu Siku ya Qiyaamah, na mwenye kudumu humo akiwa amedhalilika. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. Na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye anatubia kwa Allaah tawbah ya kweli. Na wale ambao hawashuhudii uongo, na wanapopita kwenye upuuzi hupita kwa heshima. Na wale ambao wanapokumbushwa Aayaat za Rabb wao, hawapinduki kuzifanyia uziwi na upofu. Na wale wanaosema: Rabb wetu! Tutunukie katika wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu, na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa. Hao ndio watakaolipwa maghorofa ya juu (Jannah) kwa kuwa walisubiri, na watapokelewa humo kwa maamkizi na amaniNi wenye kudumu humo. Uzuri ulioje wa mahali pa kustakiri na makazi ya kushi daima. [Al-Furqaan: 63 - 76]
2- وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ
Nafsi (uhai) kwa nafsi (uhai)
Mwenye kumuua mwenzake bila ya Shariy’ah naye anapaswa kuuliwa.
Hii iko wazi kabisa katika Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٨﴾ وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧٩﴾
Enyi walioamini! Mmeandikiwa shariy’ah ya kisasi kwa waliouawa; Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa ihsaan. Hiyo ni takhafifu kutoka kwa Rabb wenu na rahmah. Na atakayevuka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo. Na mtapata katika kisasi (kuokoa) uhai enyi wenye akili ili mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 178 - 179]
Lakini kuna visivyohesabiwa katika Shariy’ah hii mojawapo imetajwa katika Aayah yenyewe nayo ni:
Ya Kwanza: Jamaa za mtu aliyeuliwa wanaweza kuchukua fidia ya pesa (blood-money) kutoka kwa muuaji.
Ya Pili: Ni baba anapomuua mtoto.
‘Ulamaa wengi wao wameona kwamba baba asiuliwe kwa kitendo hicho. Rai hii imesimuliwa na 'Umar ibnul-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu). Na Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo inasema:
لاَ يُقادُ الوَالِدُ بالْوَلَد
“Hakuna adhabu/malipo kwa baba kwa sababu ya mwana” [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad na wengineo]
Lakini Imaam Maalik ambaye hakuitambua Hadiyth hii kaona kwamba ikiwa baba amemuua mwana makusudi, bila ya makosa yoyote, basi naye auliwe.
Ya Tatu: Ni hali ya mtu aliye huru anapomuua mtumwa.
Hii ni rai ya wengi wa ‘Ulamaa. Abu Haniyfah na wafuasi wake wamaona kwamba ikiwa mtu atamuua mtumwa wake mwenyewe, asiuliwe, lakini mtu akimuua mtumwa wa mtu mwengine basi auliwe.
Ama wengine wameona kuwa mtu huru akimuua mtumwa yeyote basi naye auliwe.
Ya Nne: Muislamu anapomuua asiye Muislamu.
Aayah nyingine zinazohusiana na kipengele hicho:
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً ۚ وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ إِلَّا أَن يَصَّدَّقُوا ۚ فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٩٢﴾ وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا ﴿٩٣﴾
Na haiwi kwa Muumin amuue Muumin ila kwa kukosea tu. Na atakayemuua Muumin kwa kukosea basi aachilie huru mtumwa Muumin na atoe diya kwa kuifikisha kwa ahli zake, isipokuwa watolee wenyewe swadaqah. Na ikiwa ni miongoni mwa watu wa maadui zenu naye ni Muumin, basi (aliyeua) aachilie huru mtumwa Muumin. Na ikiwa ni miongoni mwa watu ambao kuna mkataba baina yenu na baina yao; basi wapewe diya kuifikisha kwa ahli wake na aachiliwe huru mtumwa Muumin. Asiyepata, afunge Swiyaam miezi miwili mfululizo; kuwa ni tawbah kwa Allaah. Na Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote. Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo na Allaah Atamghadhibikia na Atamlaani na Atamuandalia adhabu kuu. [An-Nisaa: 92 - 93]
3. وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ
Yule Anaeacha Dini Na Akajifarikisha Na Jama’ah (Kundi) (Amejitenga Na Watu Wa Dini Yake).
Mtu akisilimu au akiwa ni Muislamu harusiwi tena kutoka. Dini si kitu cha mchezo, mtu kuingia na kutoka atakavyo. Mwenye kutoka katika Uislam huitwa “Murtad” na hukmu yake ni kuuliwa. Kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
من بدل دينه فاقتلوه
Mwenye kubadilisha dini yake (ya Kiislamu) muueni. [Al-Bukhaariy 6922, Abu Dawuud 4329, At-Tirmidhiy 1483].
Maelezo Mengineyo Ya Hadiyth Hii:
Mauaji yatekelezwe na wahusika wa serikali na sio mtu binafsi; mfano kaka aliyeuliwa ndugu yake asitoke kwenda kulipiza kisasi mwenyewe bila ya kupelekwa kesi yake mahakamani kisha tena Hakimu (Qaadhi) ndiyo atoe hukmu. Ikiwa mtu atafanya hivyo basi naye itapasa apewe adhabu, lakini sio adhabu ya kuuliwa kwa vile kamuua mtu ambaye alistahiki kuuliwa.
Hilo la mwenye kubadili na kuuliwa, lina maelezo mengi na ufafanuzi mrefu ambao mnaweza kuupata katika makala ya Kuritadi iliyomo katika kiungo kifuatacho:
Kurtadi (Kutoka Katika Dini)
Faida Tunazopata Katika Hadiyth Hii:
Maisha Ya Muislam ni ya thamani na yanalindwa na sheria. Hakuna mwenye haki ya kuchukua maisha yake Muislam hadi awe amefanya jarima ambayo itahitajia adhabu ya kuuawa.
Kufanya uzinifu, uuaji, na kuritadi ni madhambi makubwa kabisa katika sharia ya Kiislam, sheria ambayo inalinda maisha na uhai wa mtu. Hivyo, sheria hiyo itakuwa kali na kumuadhibu adhabu inayostahi yeyote atakayefanya madhambi hayo yasiyostahi nafasi ya mtu huyo katika jamii safi yenye nidhamu na ustaarabu.
Moja ya malengo ya adhabu ya kifo ni kulinda utakatifu na maisha ya Waislam, Kama ambavyo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anavyosema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٨﴾وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧٩﴾
Enyi walioamini! Mmeandikiwa shariy’ah ya kisasi kwa waliouawa; Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa ihsaan. Hiyo ni takhafifu kutoka kwa Rabb wenu na rahmah. Na atakayevuka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo. 179. Na mtapata katika kisasi (kuokoa) uhai enyi wenye akili ili mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 178-179]
Na Allaah Anajua zaidi